Kwanini Orijino Comedy Dstv haina wafuatiliaji wengi?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari wana JF,

Hivi kwanini Orijino comedy dstv haina wafuatiliaji wengi ,Shida ni nini?

Kukosekana kwa Joti? Muda uliowekwe kwa ajili ya hicho kipindi?

Kwa kifupi hata viewers wa clips zao kwenye mitandao ni wachache shida nini?

Maana waigizaji wapo tena wazuri, kwa mnao fuatilia shida ni nini uwasaidie?
 
Utunzi wao umepoteza mvuto na walianza kupotea walipoingia TBC.
 
Una uhakika icho kin'gamuzi kina watumiaji wengi?
 
Tuulizane kwanza wangapi wanatumia DSTV?, pia wangapi wanaweza lipia vifurushi vya DSTV miongoni mwa hao watumiaji?.
Ukipata majibu hiyo ndo sababu.

Mwisho japo si kwa umhimu, huwa hawana vipengele vingi vinavyokosoa au kukumbusha serikali haki na uwajibikaji.
 
mchawi ni muda. Muda wao ushakwisha kufanya TV shows. Umma unaitaji kizazi kipya.
 
Watumiaji wa Dstv ni wengi lakini ufuatiliaji sio Mkubwa kama tamthiliya nyingine
 
Duh...hiyo takwimu umeitoa wapi? kama hutumii DSTV utaionaje show? hizo clips zao mitandaoni wamezipost lini wakati mkataba wao hauruhusu? ni watu tu wanarecord show na kurusha YouTube na ndo sababu utaona wala hazikai zinaondolewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…