Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Biblia ni fasihi ya hali juu sana unatakiwa uombe msaada wa Mungu kabla hujaanza kuisoma,ila hatumtendei haki mwenye Uzi huu kwani nje ya Uzi kabisa.
 
Peleka ujinga wako mitaani huko....Kwanza kajifunze kuandika
 
wakatoliki na biblia wapi na wapi?? mi namuunga mkono luther....si mnaona nyie wenyewe mnavotofautiana kuna wale kama walokole na wengine tradional rc, mtu yeyote akisoma historia ya roma kwa muda mrefu ni rahisi sana kujitenga, upako mdogo mno.
Una muunga mkono kupunguza vitabu vya Biblia...???? Unayosababu iliyompelekea yeye kupunguza vitabu 7 vya AK....

Tupe sababu ya yeye pia kutaka kuondoa vitabu vya Ufunuo, Waebrania, na Yakobo....
 
Kuchangia siyo kuvuruga.Umegusa Imani. Bahati nzuri mada hii ya watu wa Imani moja. Katika Imani hii kila mchangiaji anagusa eneo moja tu kujenga au kubomoa.Ajengaye ni wa Kristo na anaye bomoa ni wa mwovu.
Mtihani wa hesabu kwanini utoe majibu ya Jiografia...????
 
Maria alipalizwa mbinguni pakikucha nitakuletea mstari labda ninukulu Ishara mkubwa ilionekana mbinguni Mwanamke aliyejipamba vzuri na taji la nyota kichwani mwake,ipo kkwenye Ufunuo asubuhi nitakupa vzuri zaidi
Mwanamke wa Ufunuo 12 ni Kanisa la Kristo,kitabu cha Ufunuo kinatumi lugha ya mfano. Mwanamke safi ni kanisa la Mungu linalotii amri zake, Kahab mkuu wa Ufunuo 17:5 ni kanisa lililoasi Amri za Mungu, ushahidi wa kibiblia unaonyesha kanisa hili ni Roman Catholic.Mnyama wa ufunuo 13 na 14 ni mamlaka ya kipapa.Utaona kuna mfanano mkubwa baina ya kahaba wa ufunuo 17 na mnyama w ufunuo 13 na 14.Hapa utaona kanisa la rumi likitumia nguvu za kisiasa kushinikiza ibada ya uongo."Wafalme wa nchi wamezini naye" . uzinzi hapa husimamia uasi wa Amri za Mungu. Kanisa la roma limeasi amri za Mungu na kuanzisha ibada iliyo kinyume na Mungu.Yaani wamebadili Sabato ya siku ya saba na kuifanya jumapili ambayo ni siku ya kwanza ya juma.wamebadili ubatizo kwa kunyunyiza maji badala ya kuzamishwa,Yesu hakunyunyiziwa maji alipokuwa mchanga bali alibatizwa akiwa mtu mzima ili nasi tufuate mfano wake. Kanisa la roma limeondoa amri ya pili inayokataza ibada ya sanamu na kanisa limejaa sanamu eti kwa majina ya watakatifu! Amri za Mungu katika kutoka 20 zimebadilishwa kama zinavyoonekana kwenye misale ya waumini.Wametimiza unabii wa Daniel 7:25." Naye ataazimu kubadili majira na sheria".
 
Mwanamke wa Ufunuo 12 ni Kanisa la Kristo,kitabu cha Ufunuo kinatumi lugha ya mfano. Mwanamke safi ni kanisa la Mungu linalotii amri zake
Toa ujinga wa kutuletea ngonjera za Ellen G White hapa.....Hivi unajua hata dhima ya Kitabu cha Apokalse ya Yohana...? Unajua kiliandikwa lini na kiliwahusu kina nani hasa...???

Tutolee ngonjera za makambi na lesson
 
Yaani wamebadili Sabato ya siku ya saba na kuifanya jumapili ambayo ni siku ya kwanza ya juma.
Hivi unaijua historia mpaka kufikia SDA kuanzs kutumia Jumamosi kama siku yao ya kukutana...??

Labda huwafahamu hawa watu....

Unahitaji kumjua vizuri William Miller, Joseph Bates, Hiram Edson na Ellen G White...

Ukiwajua vizuri hao wanaharakati na jinsi walivyofukuzwa kwenye makanisa yao ndio utajua kwanini huwa mnakutana kila Jumamosi...
 
 
Toa ujinga wa kutuletea ngonjera za Ellen G White hapa.....Hivi unajua hata dhima ya Kitabu cha Apokalse ya Yohana...? Unajua kiliandikwa lini na kiliwahusu kina nani hasa...???

Tutolee ngonjera za makambi na lesson
Upuuzi mtupu ulioandika, ndio maana Martin Luther alianza kulipinga kanisa la roma baada ya kuona limeacha kufuata Biblia na kujitangia misale, ndicho ufanyacho eti tusiifuate Biblia ila tuamini hadithi za kutunga za kwenye misale.badilikeni, Yesu anakuja.
 
Hiyo ndio sababu iliyomfanya aondoe vitabu 7 vya Agano la Kale....

Hiyo ndio sababu iliyomfanya atake kuondoa vitabu vya Ufunuo, Yakobo na Waebrania..

Hebu nipe sababu kama unaijua, uniambia aliviondoa kwa mamlaka ya nani...??
 



ZABURI 16:3, “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, hao ndio ninaopendezwa nao ”

1Petro1: 15 - 17
bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.

17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
 
Evidence plz ebu tuaminishe kwamba RC wametumia kitabu cha Ufunuo kinatumika hvyo unavyosema.

ZABURI 16:3, “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, hao ndio ninaopendezwa nao ”

1Petro1: 15 - 17
bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.

17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
 
ZABURI 16:3, “Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora, hao ndio ninaopendezwa nao ”
Haya jikite kwenya mada..

Tupe sababu za Martin Luther kupunguza vitabu 7 vya Agano la kale...

Pia tupe sababu zilizompelekea kutaka kuondoa vitabu vya Ufunuo, Yakobo na Waebrania...
 
Na unaposema "kipaumbele" unataka kumaanisha kitu gani hasa...? Kipaumbele ni nini..?

Kwamba kaburi lipo ila halijapewa kipaumbele cha kuandikwa kwenye biblia...??? Ni kipaumbele gani unataka kuzungumzia hapa..?
Sakata lote la Yesu Wayahudi hawalitambui sembuse Maria? enzi hizo hakukuwa na mwanamke aliyepewa hadhi kwenye jamii, kwenye dini wala kwenye bibilia zsidi ya kuwataja tu walichofanya kuwatendea wanaume maarufu kama vile kueazaa, kuwapa chakula na kuwaimbia au kiwatukuza wanaume hao
 
Mamlaka haya aliyapata kutoka kwa nani angali Biblia ilikuwa imeshakamilika...
biblia hasa agano la kale tumeitoa kwa wayahudi. sasa wayahudi hawakuwa na hivyo vitabu saba vya kina Judith na Tobith. wakatoliki waliviongeza ndiyo sababu Luther aliviondoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…