Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Luka anasema:

BIBLIA TAFSIRI YA ULIMWENGU MPYA
Luka 1:
1 Kwa kuwa wengi wamechukua daraka la kukusanya habari za mambo ya hakika+tunayosadiki kikamili kati yetu,2 sawa na vile wale ambao tangu mwanzo+walikuwa mashahidi wa kujionea+ na watumishi wa ujumbe+walivyotuletea haya,3 mimi pia niliazimia, kwa sababu nimefuata kwa uangalifu mambo yote tangu mwanzo kwa usahihi, kukuandikia hayo kwa utaratibu wenye kufuatana,+mtukufu+Theofilo

Ukisoma hayo tu, utaelewa kuwa hapo hakuna kitabu cha Mungu. Labda uwe punguani.

Maana Luka hapo anakiri ameandika ili amfurahishe kiongozi "Theofilo" tu.
 
Kila andiko kwenye Biblia ni neno la Mungu yaani ni Mungu mwenyewe ....angalia unapofikiri unapinga Ukatoliki kumbe unampinga Mungu ....tukianza kuchagua andiko hili ni muono wa kibinadamu na hili ni Mungu tunaenda kubaya sana.....Yesu ni Mungu hivyo hatuombei bali yeye ndio mpaji ...ila Mapadre, wachungaji, watakatifu n.k wanaweza kutuombea kwa Mungu ....kama wewe ni Mkristo na huamini kuna maisha baada ya kifo basi ule ufufuko wa Yesu ulikuwa kazi bure ......kama Yesu alitokewa na Musa, Eliya kumtia moyo ....enzi zenu si mngesema ni wafu/ mizimu ile?
Mungu hajaandika kitu tafadhali wacha hadithi, ya mungu ni mengi sana hayaandikiki na hakuna anayeweza kuyaandika maana hayajui. Vitab hivi viliandikwa na watu wema wenye nia njema na wenye maono waliotaka kutatua tatizo la kijamii la wanajamii hisika/maalum
 
biblia hasa agano la kale tumeitoa kwa wayahudi. sasa wayahudi hawakuwa na hivyo vitabu saba vya kina Judith na Tobith. wakatoliki waliviongeza ndiyo sababu Luther aliviondoa.
Unajua biblia imekaa ikiwa complete tena yenye pumzi ya Mungu kwa Miaka zaidi ya 1500... Sasa ni mamlaka gani huyo Luther na aliyapata wapi kupunguza vitabu vya Agano la Kale...?

Miaka yote hiyo biblia imtunzwa aje mtu mmoja kwa siku moja kuondoa vitabu 7..

Hiv hujui kama siyo Calvin leo ungashupaza shingo yako ukitetea uharamia ambao Martin Luther aliotaka kuufanya kwenye vitabu vya Agano jipya....? Hivi hujui kama siyo Calvin leo Waprotestant mngekuwa na vitabu 24 vya Agano jipya. ? Hivi ungekuja kufanya utetezi gani hapa...?
 
Mungu hajaandika kitu tafadhali wacha hadithi, ya mungu ni mengi sana hayaandikiki na hakuna anayeweza kuyaandika maana hayajui. Vitab hivi viliandikwa na watu wema wenye nia njema na wenye maono waliotaka kutatua tatizo la kijamii la wanajamii hisika/maalum
Wewe hebu jiondoe hapa maana huna unachojua..
 
Ka
Wewe hebu jiondoe hapa maana huna unachojua..
kama ndo hivyo hata komputers, simu na ndege zimetengenezwa na Mungu. Maana watu waliondika bibilia na quran wanasema "wenyewe" wametumwa na Mungu hivyo ni Mungu kaandika, kwanini watu waliobuni hii JF nao wasiwe wametumwa na mungu hivyo iwe ni Mungu aliyeibuni jf?
 
Alafu ili kulibeza Kanisa Katoliki Walokole wengi wanambeza sana Bikira Maria....wanasahau Yesu ni Mungu kweli na Mtu kweli ....sijui wewe utajisikiaje watu wakimkejeli mama yako .....Pale anaposema vizazi vyote wataniita mbarikiwa bila Kanisa Katoliki kwa mwenendo wa makanisa ya sasa angeitwa mbarikiwa ili hilo neno litimie?
Mtu anapinga Bikira Maria kutuombea, lakini akiambiwa aombewe na AKINA MWINGIRA, KAKOBE, RWAKATALE etc etc faster wanaenda... siwaelewi.
 
Ni kwl hata mimi siku nkiona andiko linalosema bikra maria yupo hai na anatuombea siku hiyo ntarudi kama hiyo imani ya roma,ninae mjua yuko hai ni Kristo yesu peke yake yuko hai milele na ndo atakaekuja kunyakua kanisa n mtu haendi kwa baba bila kupitia kwake,na ndo muombezi wetu,Swala la kwnn alitumiwa kubeba mimba Roho mtakatifu au Mungu huweza kumtumia yoyote aliemuumba na ndo maana Balaki alipo mwambia mchawi balaamu awalaani wana wa israel,wakati balaamu anaenda kuwalaani wana wa israel alikuwa amepanda punda na siku hiyo Mungu alimtumia huyohuyo punda kutamka maneno kama mwanadamu,kwahyo hatuwez kusema punda ni mtakatifu anafaa kutuombea kisa alitumiwa na Bwana Mungu,Mungu anaweza kumtumia yoyote kwa ajili ya kazi yake maana vyote alivyoviumba viko ndani ya uwezo wake kuvitumia atakavyo,Kwhiyo mariam ni mtakatifu kwa sababu alimbeba mtakatifu na ni mbarikiwa kwa sababu alimbeba katika tumbo lake yule aliekuwa amebarikiwa hata neno linasema hata sisi tutakuwa watakatifu maana alie ndani yetu ni mtakatifu,kwhiyo maryam kumzaa Yesu alitumiwa tu lakini haimpi mamlaka ya yeye kuwa mwombezi wenu!! hana mamlaka hayo na wala hakuna mtume wala nabii ambaye amepewa mamlaka hayo ni kristo peke yake!! Hivi mbona neno liko wazi hizo biblia huwa mnasoma mkiwa timamu kwa kuongozwa na roho mtakatifu kwl?? au tatzo roho mtakatifu wenu huwa anakaa upande wa kulia ndo maana lakini akikaa moyoni mwako neno utalielewa vzuri sana.
Kwenye harusi ya kana wale watu walimwambia Bikira Maria afanye nn!? Na pale msalabani Yesu alimwambiaje yule mwanafunzi wake anayempenda!? Acha akili za kushikiwa ww.
 
mnanishangaza sana na kunistua kwa kweli, hivo vitabu mnavodai vilipunguzwa mara viliongezwa (yani kama vipimo vya mchele), si vyote mnadai viliandikwa na manabii na mitume wa Mungu au?

sasa huko kupunguza mara kupunguzwa ni kwambo hao waliandika kwa msaada wa Mungu(according to christians) walikosea au vipi?

Naona mnataka mniaminishe kuwa biblia ni mchakato wa binadam flan waliokuwa na mpango wa kupga dili tu na kuzishika brain zetu aisee.....!
 
Ehhe! Hebu niambie anarudi lini...?


Maana biblia yangu inaniambia hakuna ajuaye siku wa saa ya kuja mwana wa Adamu....
Yesu alisema, "hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu lile lilinenwa na nabii Daniel (asomaye na afahamu)... Paulo anasema " siku ya Bwana haiji hadi afunuliwe yule asi, ajiinuaye nafsi yake kama Mungu ambaye Bwana Yesu atamuua kwa pumzi yake". 2 wathesalonike 2:1-5. Hilo chukizo la uharibifu kama alivyonena Daniel ni Papa. Paulo aliiona nguvu hii pia ikitenda kazi kuanzia kwnye dola ya kirumi na kisha kanisa la rumi.Huyo asi muda si mrefu atafunuliwa pale atakapoungana na wafalme wa dunia hii ili kushinikiza ibada ya uongo dhidi ya Ibada ya Mungu. Hapo Michael atasimama upande wa watu wa Mungu Daniel 12:1. Huyo asi na wafuasi wake wataangamizwa na wateule watatwaliwa Mbinguni. Kwa mujibu wa Biblia siku hizo haziko mbali.
 
Wakuu mbona mnabishanana sana wakati wazungu walioleta dini/ madhehebu hayo wakila bata na kupiga hatua za maendeleo kila kukicha?, cha msingi Naona kila mtu abaki na iman yake kukosoana na kutokwa na mapovu namna hii utadhan tulikuwepo wakati biblia inaandikwa hakuna maana. Kila mmoja asidharau iman ya mingine na hakuna aliye bora kuliko mwenzake as long as wote mmeumbwa kwa mf na sura ya Mungu

Well said!!

Dini uliyo nayo leo ni urithi toka kwa jamii uliyokulia au inayokuzunguka. Hii ni pamoja na mila na desturi za kwenu.

Mara nyingi huwa binadamu anakubali na kutukuza values alizikuzwa nazo na mara nyingine yuko tayari hata kufa kwa ajili ya kuzilinda.

Wewe ni Muislam su Mkristo kwa sababu jamii inayokuzunguka ilikuaminisha katika Uislam ama Ukristo.

Yule ni myahudi ' judaism' kwa vile kukulia Israel/uyahudi.

Yule mhindu au dini za wachina na wajapani nk.

Kuponda dini, mila imani ya mwenzio si kuwa tu inajenga chuki na dharau miongoni mwa jamii, bali pia inasababisha unayejaribu kumuonyesha ubaya wa dini /mila au imani yake, aone ubaya wa dini yako wewe na azidi kuichukia dini yako na wewe mwenyewe!! Badala ya yeye kufuata unayoamini unazidi kumfukuza mbali zaidi.

Hivyo kuanika masuala ya imani mbalimbali hapa ambazo watu mbalimbali wanaziabudu sio jambo la mbolea!!

Ni upungufu wa busara!!

Amini ambacho wewe na akili yako na roho yako uneridhika nacho. Period.


Hakuna kitu kama Univesal faith au Universal religion!!!

Kwa akili za binadamu hakuna imani ambayo inakubalika au itakayokubalika kwa wote

Amani iwe kwenu!!
 
Biblia inasema Bikra Maria ataitwa mbarikiwa, na dunia itamsifu kuwa yeye ni mbarikiwa. Bikra Maria kwa mujibu wa kumbukumbu za kanisha hakufa, alipaazwa. Ujui historia, huyu mama ni the special, hata waprotestant wakimtupa sisi Wakatoliki tutaendelea kutimiza unabii kwa kumuita mbarikiwa
Umbumbumbu tu wa maandiko ndio unakutesa
 
Alafu hawa wasabato wameharibu Uzi kabisa, mtoa Uzi kata rufaa kwa mods maana wasabato wameshatutoa nje ya mada
 
Hii thread inahusu Padre Luther kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ambayo ndio mnayotumia Waprotestant ....tuambieni kwanini aliviondoa? Kwanini alitaka kuondoa hadi kitabu cha ufunuo hadi mwenzake Calvin alipoingilia kati (maana yake leo waprotestant msingekuwa na kitabu cha ufunuo kwenye Biblia yenu kama si juhudi za Calvin) ....mada za Bikira Maria, tunaabudu sanamu n.k fungueni uzi wake maana mshaharibu mada ....kama hujui historia waachie theologians waje kujibu hoja zetu .....nyie mliokariri vifungu vya Biblia hamuwezi kuja na majibu hayo maana hapa tunaichambua historia ya hiyo Biblia tunayoitumia ili ujue hicho unachoamini kimepatikanaje .....vifungu haviwezi kujibu hapo ....
 
Maria ametoka wapi kwenye Uzi huu....?watakatifu wametoka wapi...?tujikite kwenye mada kama unataka ya Maria anzisha Uzi alafu tutakuja.
 
Hii thread inahusu Padre Luther kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ambayo ndio mnayotumia Waprotestant ....tuambieni kwanini aliviondoa? Kwanini alitaka kuondoa hadi kitabu cha ufunuo hadi mwenzake Calvin alipoingilia kati (maana yake leo waprotestant msingekuwa na kitabu cha ufunuo kwenye Biblia yenu kama si juhudi za Calvin) ....mada za Bikira Maria, tunaabudu sanamu n.k fungueni uzi wake maana mshaharibu mada ....kama hujui historia waachie theologians waje kujibu hoja zetu .....nyie mliokariri vifungu vya Biblia hamuwezi kuja na majibu hayo maana hapa tunaichambua historia ya hiyo Biblia tunayoitumia ili ujue hicho unachoamini kimepatikanaje .....vifungu haviwezi kujibu hapo ....
Ukitaka kujua kuwa waroma ni vilaza wasomee mstari ya Biblia hawambulii kitu maana wao wamekaririshwa misale ya waumini tu. Hoja zozote zisizo pata support ya Biblia ni hoja mfu. Na si ajabu waroma kuabudu wafu na masanamu maana hawasomi Biblia.
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Kama wachungaji hawa wa kilokole ni darasa la saba ndiyo maana wanapotosha maandiko; Mtume Petro mnayemwita papa wa kwanza alikuwa darasa is ngapi?

Acha kuchanganya elimu yako ya darasani na uwezo wa Roho Mtakatifu.
 
Back
Top Bottom