Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa Kanisa Katoliki?

Kwa taarifa yako, sio kujua hayo mafumbo ya vitu na watu, ni kuwa kitabu chote cha Apokalpse ya Yohana nina weledi nacho ..

Vipi unataka tuelimishane...??
Hebu tuelimishe nasi tukuelimishe hiyo ndiyo itakayotoa mwanga kwa wasomaji wengi..!
 
Hebu wewe nieleze....Sitaki kurudia mara kumi kumi kitu kile kile.....

Wewe unafikiri hao wazee 24 na wale 4 ni nyanya zako wako dongobeshi...?
Mbona unatukana na una hasira...punguza hasira..rudi kwenye swali na elezea ili tukuelewe!!
 
Nadhani tuiangalie Biblia inasemaje..Theology isikufunge maana hiyo siyo Maandiko, Ukiisoma Biblia haijichanganyi imesema moja kwa moja...'Hakuna mtu anaweza kusimama badala ya Yesu Kristo ili kumfikia Mungu Baba..hiyo ni Biblia inasema, sasa kama Theology inataka kupindisha hilo haliwezi kuwa matakwa ya Kibiblia bali matakwa ya hao wanatheology na utashi wao wa kuelewa.
 
Laiti ungejua hata hiyo tafsiri unayoamini chanzo chake ni nini usingeangaika kumshangaa mwenzako....kwani nini unaamini tafsiri yako ni sahihi na huyu ni potofu? Mchungaji wako? Tumieni akili kwenye vitu vinavyohitaji akili tu!
Hebu tupe tafsiri yako ili kujenga uelewa zaidi na kama ni tofauti utapingwa tu..maana Biblia itabaki kuwa ilivyo na tafsiri za wanadamu zitabaki kuwa tafsiri...karibu
 
Naona hapa umeanza uchochezi kati ya wakatoliki na walutheri na bila kujua watu wameingia kichwa kichwa na kuanza kurushiana maneno.

Dhambi ya ubaguzi aliyoisema Nyerere ndio inaanzia hapo, mleta mada ameanza ameanzisha mada hii akijua kabisa nia yake kuchonganisha watu then akimaliza hapo anakuja na thread ya waislam na wakristo.

Akimaliza hapo kati ya wakristo na waislam anajua ameshapandikiza chuki kwa kumwaga sumu ya maneno, then wengine waje waseme kabila fulani na fulani ni wakuogopwa ni kama ukoma

Moderator nashauri maada hii ifutwe cc Invisible
 
Yesu aliacha kanisa katoliki lini? Wakristo wenzangu hamna tofauti na walevi.
Usitukane..We mjibu hoja yake ili kujenga uelewa nadhani ndiyo msingi wa forum hii!
Yesu alipokufa aliliacha Kanisa lisilo na jina, na pale Yerusalemu, Mitume walikuwa na kawaida ya kukutana na Kusali hata baada ya mtawanyiko alipokufa Stefano, wengi walitawanyika kwenda Asia ya Kati, Wengine wakaenda hadi Antiokia (uturuki ya sasa) na huko baada ya wengi Kuiamini Injili ya Yesu Kristo wakaamua kujiita Wakristo..Kwa hiyo Neno ukristo lilianza kuitwa mahali hapo (Mdo:11:26..)
Kwahiyo hakuna mahali ambapo Biblia inatuambia aliacha Kanisa la Catholic, au Sabato, au Lutheran au Pentecoste, au Assemblies of God au lolote unalolifahamu....Ukifahamu hilo tunaweza kuendelea zaidi ya hapo...Karibu
 
Nilichojifunza jamii ya Walokole wengi elimu ya Kimungu hawaijui. Ndio maana hata ukweli wakati mwingine wanaupinga.
Umekosea ndugu, Unataka Elimu gani ambayo itakuthibitishia kuwa jamii ya watu waliokoka wengi hawana Elimu ya Kimungu, Nadhani hoja yako uliyoiweka kwenye forum hii inahitaji michango ya wengi na usizuie uchangiaji wao, Kikubwa kinachoangaliwa hapa ni Je Biblia ndiyo msingi wa michango hiyo..? kama siyo Je madhara yake ni yapi? Maana unapopingwa na ulichosema inamanisha aidha wewe mwenyewe hujui ulichokisema msingi wake au unajua ila umejiapisha kutokubadilika.
 
Great..
 
Hebu tupe tafsiri yako ili kujenga uelewa zaidi na kama ni tofauti utapingwa tu..maana Biblia itabaki kuwa ilivyo na tafsiri za wanadamu zitabaki kuwa tafsiri...karibu
Umekariri ...kwa taarifa yako Biblia yenyewe haijipi mamlaka mnayoipa ....hivyo ukiamua kubaki na kuamini kilichoandikwa tu si mbaya ila yapo mengi hayakuandikwa. Kanisa Katoliki ndio lililofanya juhudi za kukusanya vitabu na kuvichambua vipi viwe sehemu ya Biblia kwa muongozo wa Roho Mtakatifu .....kazi hiyo haikuishia hapo ...bado Roho Mtakatifu analiongoza hata sasa kama walivyopata maono ya kuhifadhi neno la Mungu....Biblia yenyewe inakiri kwenye 1Timothy 3:15 " This is the church of living God, which is the PILLAR and FOUNDATION of the TRUTH" .....Kanisa muongozo mkuu ni Roho Mtakatifu na Biblia ni sehemu ya msingi wa imani....
 
Kwani kina nani wanamuomba Mungu kupitia njia tofauti na Yesu.....?ebu tuambie na utuzdhibitishie hilo.....!nakusubiri.
 
Great kwa lipi...?kwa upotoshaji...?Upagani wa Roman Catholic ni upi haswa.....?Je unazungumzia vile vitabu 7 vya Deuterocanony....?kama ndio unajua historia yake....?katika safari yako ya usomaji ulishawahi kuvisoma vile vitabu...?kama bado nenda kavisome kama tayari vitabu vile vinapinga ya Mungu.....?na mwisho unajua historia ya hivyo vitabu yani kwann havipo kwenye biblia ya Wayahudi/Waprotestant.....?
 
Kwani kina nani wanamuomba Mungu kupitia njia tofauti na Yesu.....?ebu tuambie na utuzdhibitishie hilo.....!nakusubiri.
Kama na wewe unaomba kupitia Yesu Kristo basi uko sawasawa na Biblia na hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo Biblia inasema Yn.14:6
Nadhani tusipindishe, Yako uliyoeleza nakubaliana nawe..Kwamba Kanisa linaongozwa na Roho Mtakatifu...Nakubaliana nawe kabisa..Lakini unaposema Biblia ni sehemu ya msingi wa imani...hapo tutataofautiana..Kwanini, Kwasababu Biblia siyo sehemu...hapana!! Ndiyo haswa Msingi kamili wa Imani ya Kikristo na Roho Mtakatifu anapokuelekeza kufanya anakuelekeza ufuate kilichoandikwa kwenye Biblia..na ndiyo Maana Maandiko yanasema wazi kuwa asiwepo mtu wa kuondoa hata yodi moja ya neno Katika Biblia ili ule Msingi usiyumbishwe na matakwa ya watu..na hii tunaishuhudia hata sasa kuoona waalimu, manabii, wachungaji wanapotosha kilichoandikwa kwenye Biblia na kuaminisha watu kuwa ndivyo ilivyo, Mifano ni mingi, tunaweza kupata forum nyingine kueleza.
 
Great...kwamba ameelezea vizuri...hebu elezea hivyo vitabu umevieleweje na vinatoa tafsiri gani..?
 
Nadhani tuiangalie Biblia inasemaje..
inasemaje kuhusu nini..??

Theology isikufunge maana hiyo siyo Maandiko,
Unajua maana ya Theology wewe...??? Ndio maana mnanyweshana detto na dawa za mbu huko makanisani kwenu...

We huu mjadala kaa nao mbali mno mno nenda kule jokes ndio kuna kufaa...
 
Wewe umeniuliza nini na mimi nimekujibu nini..? Nimekujibu ulichoniuliza....
Basi tusigombane katika haya, nadhani forum hii ni kwa ajili ya kueleweshana ili kujenga uelewa mzuri zaidi, inawezekana mmoja akawa na uelewa zaidi au mdogo lakini mwisho wa siku ataelewa naye..ukichukia unaweza ukatunyima hata yale mazuri ambayo bado hujayasema hapa, naamini hivyo.
 
inasemaje kuhusu nini..??

Unajua maana ya Theology wewe...??? Ndio maana mnanyweshana detto na dawa za mbu huko makanisani kwenu...

We huu mjadala kaa nao mbali mno mno nenda kule jokes ndio kuna kufaa...
Ndugu una uhakika gani kama mimi siijui theology au credentials zangu unazijua? Naona tusimamie Biblia inavyosema na wengine wapate kuelewa, usiwe na hasira, rudi kwenye nafasi yako vizuri, elezea nasi tutakusoma na kukuelewa, Kule kwenye jokes forum wala hutaweza kuniona maana siyo eneo langu. asante
 
Kama na wewe unaomba kupitia Yesu Kristo basi uko sawasawa na Biblia na hivyo ndivyo ilivyo na ndivyo Biblia inasema Yn.14:6
Kuna mtu alikataa...? Umeshawahi kuona jinsi sala za Katoliki zinavyoishia...?? Umeshawahi sikia maneno yanatamkwa mwishoni...??


Nadhani tusipindishe,
Nani anapindisha...??


..Lakini unaposema Biblia ni sehemu ya msingi wa imani
Sasa unadhani bila biblia huyo Yesu ungemjuaje...??
...hapo tutataofautiana..
Kwanini tutofautiane.. ??

Martin Luther sio aliondoa yodi moja ila aliondoa vitabu 7 vya Agano la Kale...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…