Kwanini Paul Kagame aangalie jeshi letu kwa dharau likionesha uwezo wake kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru?

Kama umeona ni upimbi basi jina pimbi unatakiwa uitwe wewe kwa upimbi ulio nao kichwani!
 
Na saivi anafanya mashambani ya anga kule Congo DRC kuwasaka waasi wa ADF.
 
Mimi nilifurahi sana yale madude kupita mbele yake najua zile ni outdated tu version Jeiwii wanazo dhana za kisasa zaidi ziko huko ndani ndani zimefichwa .

Kama analeta dharau ajaribu moto wake
 
Kubeba mzigo wa kilo zaidi ya 30 kisha unaruka ruka nao na ile ya kuvunja matofari kwa mikono sidhani kama ndio uwezo wa komandoo,isitoshe kwa nini haswa hawa special forces washirikishwe kwenye maparade???tena mbele ya wageni tena majirani zako??
 
Mtu pekee anaeweza kumu outsmart PK ni JK na mimi tu,, huyu jamaa tayari ana Blackhawk attack helcopters, na hii ni tabu kweli kweli,, inabidi angalau nasisi tutafute HIND..
In order to outsmart that guy, you must think like him,,, he is very smart
Sisi soon tutachukua Chinook
 
Wewe ndio itakuwa mjinga

Ushaambiwa taarifa nyingi za jeshi letu ni siri

Huwezi jua huko jeshini kuna zana gani za kisasa

Hizo ambazo outdated hazina madhara kabisa

Pale zililetwa kwa gwaride tu
 
Alichokiongea Masanja ni matokeo ya Siasa za kusifia kila kitu.Hakuwa na kitu kichwani zaidi ya kusifia mpaka akajikuta anaongea upuuzi
Magufuli aliwatia sumu wapumbavu wengi sana

Wengine ndio wana recover wengine wako critical mentally

Tuache tabia za kusifia sifia upumbavu.
 
Mimi nilikuwepo wakati wa vita ya Kagera,japo sikupigana.
Kagame namfahamu nnje ndani,ni mwanafunzi wetu.
Kagame alichojaliwa zaidi kama "individual" ni "akili kubwa ya kikatili". Kagame kuwa "exteme fighter" hakumfanyi kuwa na jeshi bora zaidi ya JWTZ.
 
Ulikuwepo ukupiga,ndo nini? Mbona ata mimi nilikuwepo sana tu.

PK sio tu alisoma Tz bali alipata pia mafunzo ya juu ya kijasusi marekani...ivyo ni mwl wetu na sio mwanafunzi tena.

JWTZ limechapwa mbaya uko Msumbiji na magaidi,PK kaombwa kuingiza jeshi lake uko ata wiki haijaisha habari ya magaidi imefifia kabisa uko Msumbiji
 
Waambie
 
Wewe ndie huna info za kutosha, au umeamua tu kusema uongo! Sio kweli kwamba eti PK ndie alimfurusha Amin! Vita ambavyo PK alipigana inaitwa Uganda Bush War na sio Kagera War!! Hii vita ilikuja baada ya Obotte kushinda kiti cha urais na Museven akakataa matokeo kwahiyo akaingia msituni, na kwahiyo alisaidia kumwondoa Obotte madarakani na sio Idd Amin!
Hakuna vita PK aliwahi kushindwa,
Vita ipi za kujivunia alizopigana na kudai eti hajawahi kushindwa?! Unazungumzia vita ya kupigana na wanamgambo ambao majority hawana any formal military trainings au unazungumzia vita dhidi ya jeshi dhaifu la DRC wasiolipwa hata mishahara?! Unazungumzia Vita Dhidi ya Wauaji wa Kihutu waliokuwa wanatumia mapanga, au vita ipi hasa?
ndje jasusi bora kabisa kuwahi tokea kusini mwa sahara...US wanajua,Nyerere,JK,JPM hawa wote na ubabe wao kwa 'slim' hawakuwahi kumchokoza
Kwahiyo huo ubora ni kwa sababu kasomea US, au?! Hivi kwa akili yako unaamini kabisa kwamba ni PK pekee ndie kasomea ujasusi US?! Au unamuona bonge la jasusi kwa sababu huwa anafanikiwa kuua wapinzani wake ?! Huo ubobevu wake unaupima kwa kutumia vigezo gani?!

On top of that, huyo Nyerere, JK na JPM waliwahi kumchokoza nani? Unadhani kila rais ni mpenda vita na kuua kama alivyo Kagame? Btw, pale vikaragosi wake wa M23 waliposambaratishwa alifanya nini?!
Wewe una taarifa sahihi sana za PK.

Jeshi letu lina idadi kubwa ya wanajeshi lakini halina ubora wowote ukilinganisha na la Rwanda.
Ubora wa Jeshi la Rwanda unaupima na nini?!
PK ni level nyingine kabisa acha atudharau km makomandoo wetu wanapigwa vibao na askari polisi hakuna namna,dharau lazima
Kwahiyo kwavile ni makomandoo unadhani wao ni watu wa vurugu?! Kwamba wakikutana na polisi, wanadindisha na kuanza kupiga majudo!! Au kwavile polisi waliwapiga makofi makomandoo kama unavyodai, ndo unataka kuaminisha watu kwamba polisi wetu ni bora kuliko makomandoo?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…