Kwanini Polisi walishindwa kuifichia aibu familia ya Mzee David Makerege? Yesu aliwaambia "asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza kumtupia jiwe"

Kwanini Polisi walishindwa kuifichia aibu familia ya Mzee David Makerege? Yesu aliwaambia "asiye na dhambi miongoni mwenu awe wa kwanza kumtupia jiwe"

Swala sio watu kuwepo mbona una ugumu kuelewa vitu vidogo tu, polisi wamepigiwa simu kuna marehemu walichokikuta si ni lazima watolee ufafanuzi na taarifa walichokikuta pale
Mtoto wa ndugu yangu alifia Hostel mwaka jana, mbona Polisi hawakuwaambia watanzania?
 
Tatizo ni weledi, hili swala polisi wangeweza ku deal nalo bila kulianika kwenye vyombo vya habari na kulifanya kubwa.
Mzee mstaafu wa miaka 80 wanaidhalilisha familia yake kabisa aisee. Sad indeed.
 
Hata kibiashara pia jina la hotel or logde linaharibiwa kiasi navyoona. Kuwa lodge ile kuna mtu alifia ndani. Haijakaa poa, sio?

Wafanye uchunguzi kimya kimya then ripoti wapatiwe viongozi wa familia, najua mitandao ipo lakini kasi ya kusambaa habari haiwezi kufananishwa na habari official kwenye press release ya RPC
Kama hiyo haitoshi mpaka chumba husika #22 hapo Mbezi garden kimetajwa pia kwenye ripoti
 
Tena na maandishi ya polisi ina maana kuna askari aliyachapa kwenye social media, so unprofessional na unethical
Badala ya kuungama wanaleta ubishi usio na faida. Wakumbuke wao pia wanao wazee wastaafu na ipo siku yatawakuta
 
Angekutwa na mzee mwenzake huenda wangemhifadhi! Swala ni wazee kuparamia umri mdogo! Nakumbuka mama Terry alizungumza sana kuhusu hili jambo ila siku hizi kakaa kimya. Pamoja na kumdhalilisha ni fundisho kwa jamii
 
Hivi ni lazima uchepuke ndiyo uwe mwanaume una umri gani kijana, hivi pia ni lazima wote tuchepuka ili kuendana na hoja zako, sio lazima kila mtu achepuke haijakua kanuni, wazee umri umewatupa watulie na wake zao, kama hana mke basi atafute wa size zao, ni sawa sawa na wewe kumendea watoto wa primary that's not fair
Kuna mtu hachepuki lakini anakula rushwa. Hii sio dhambi?
 
Back
Top Bottom