Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Siku zote huwa nawaambia hawa watoto humu hatujuani kwa sababu ya hizi I'D zetu. Ila tukishaingia huko PM na kutambulishana tunabaki kushangaana. Respect kila ID unayokutana nayo humu.
Hapa JF kuna jamaa niliandikiana nay PM kumbe ni DR wa muhimbili ..
Alinisaidia sana.. Hasa kwenye uzi kama huu wengi sana ni watu wakubwa manake wengi walipiga kitabu zamani sana na walikiwa vichwa so wako mbali now..
Zamani shule zilikuwa chache competition kubwa sana kwa hio vichwa ndio vilikuwa shule sio sa hivi hadi viazi vipo shule
 
Puza Fala,

Mwenyewe ndivyo alivyokuwa akijiita Tambaza na masela wake ndivyo tulivyomuita.

Puza alikuwa na split personality, moja boonge la mtemi halafu nyingine bonge la mtu wa kawaida hivi, kama fala, basi ukimkuta kakaa nyuma kule mesi na machizi kanyong'onyea anasikiliza story ukimwambia "Puza Fala" na yeye utamsikia "niambie kichaa wangu". Hapo kila mtu ana "Nom de Guerra". Jina la vita. Kuna Msoviet, Bedui. Mpalestina. Tyson. Buchiza. Carlos. Bokassa. Abacha. Mkonda, duuh, machizi kibao nawasahau majina wengine.Miaka 26 sasa.

Ila siku moja Puza alijichanganya anga za Herman, form one. Herman alimrusha Puza makata mbele ya darasa sitasahau mpaka leo. Puza alichezea kichapo bila kutegemea halafu ile issue ikawa imeishia pale pale kama haijatokea. Halafu ukimuangalia Herman mwenyewe aliyemchapa Puza kam mtoto mtoto tu hana jina wala mwili.

Nikasema kila mtemi ana mtemi wake.
Daah JF raha sana... Asanteni kiranga na vichwa vingine kwenye huu uzi...
 
Ha ha ha kitambo Sana daah...nakumbuka uuzwaji wa kiwanja cha mpira kutoka Tambaza kwenda muhimbili Primaly..mkaguzi wa Elimu sec Alexzander Ndeki akaja mkutanoni akamwaga data...,namkumbuka,Puza,Sagapower,Vimto..... Makamu WA shule Mr Wajimira,yule mzee aliyekuwa mkuu WA shule jina nimemsahau....baada ya fujo na Azania 1994,form wote tukasimamishwa shule mwaka nzima...mwaka uliofuata tukaperekwa shule za mikoani,...form one yetu ya 1993 ilikuwa na watu wakorofi Sana...
Mliletwa Karatu sec mkaibua issue kwa kumtwanga mwalimu baada ya kumfumania akimgegeda demu kwenye kichaka. Kilichofuata vijana wote waliotoka Tambaza mkamriwa kufungua matranka na wakakuta barua za mademu na maboyfriends.
 
Puza Fala,

Mwenyewe ndivyo alivyokuwa akijiita Tambaza na masela wake ndivyo tulivyomuita.

Puza alikuwa na split personality, moja boonge la mtemi halafu nyingine bonge la mtu wa kawaida hivi, kama fala, basi ukimkuta kakaa nyuma kule mesi na machizi kanyong'onyea anasikiliza story ukimwambia "Puza Fala" na yeye utamsikia "niambie kichaa wangu". Hapo kila mtu ana "Nom de Guerra". Jina la vita. Kuna Msoviet, Bedui. Mpalestina. Tyson. Buchiza. Carlos. Bokassa. Abacha. Mkonda, duuh, machizi kibao nawasahau majina wengine.Miaka 26 sasa.

Ila siku moja Puza alijichanganya anga za Herman, form one. Herman alimrusha Puza makata mbele ya darasa sitasahau mpaka leo. Puza alichezea kichapo bila kutegemea halafu ile issue ikawa imeishia pale pale kama haijatokea. Halafu ukimuangalia Herman mwenyewe aliyemchapa Puza kam mtoto mtoto tu hana jina wala mwili.

Nikasema kila mtemi ana mtemi wake.
Duh, bonge la memory, kipindi hicho Makonda wakiona Kaptula ya khaki wala hawasumbuki kuwazuia wanafunzi, kuna basi za Ubungo zile "Shella Beach" lile bench la nyuma lilikuwa special kwa wana Tambaza

Sitasahau Mechi ya Tambaza na Kino Muslim, pale kiwanja cha Muhimbili Primary, Mechi ilivunjika na Wanafunzi wa Kinondoni wakakimbizwa mpaka shuleni kwao Na lile bango la shule ya kinondoni likashushwa chini

Kino Muslim ndio shule pekee iliyokuwa na watoto wa kitaa na wahuni wa kweli na ndio shule hata Tambaza walikuwa wanaingia kwa kujihami
 
nimezaliwa miaka 7 baada ya Puza kujiua,naombeni nipite tu
runner.png
Kumbe ndio maana hatuelewani mara nyingine.

Ningezaa kwa kuwahi kuwahi Kiswahili Swahili wewe ungekuwa mwanangu wa tatu.

Yani wewe umri wako wa sasa ni mdogo kuliko umri wangu nilivyomuona Puza mara ya mwisho Tambaza.
 
Ha ha ha kitambo Sana daah...nakumbuka uuzwaji wa kiwanja cha mpira kutoka Tambaza kwenda muhimbili Primaly..mkaguzi wa Elimu sec Alexzander Ndeki akaja mkutanoni akamwaga data...,namkumbuka,Puza,Sagapower,Vimto..... Makamu WA shule Mr Wajimira,yule mzee aliyekuwa mkuu WA shule jina nimemsahau....baada ya fujo na Azania 1994,form wote tukasimamishwa shule mwaka nzima...mwaka uliofuata tukaperekwa shule za mikoani,...form one yetu ya 1993 ilikuwa na watu wakorofi Sana...
Mkuu wa shule unamuongelea Julius Mushi? Au nyie mlikuta Mushi kashaondoka?

Nasikia Julius Mushi alifariki.

Mzee anakwambia "You should never let me catch you without a good book".

Mr. Julius Mushi ukimwambia Tambaza wamefanya fujo wameua watu yeye anakugeuzia kibao, anakwambia "mimi wa kwangu walioumizwa wangapi na wako wapi?"

Nilivyomsikia anasema hivyo tu nikamsamehe unoko wake woote mshua yule. Alikuwa anakunja uso kama ananyonya limao, Mushi hacheki hata siku moja alivyo mkuda.
 
Ndio umeandika nini sasa. Social Media zina Umri wake ukishaona umegonga forty six na upo humu jua upstairs hauko vizuri. Wamama watu wazima wakivaa vimini au wababu waakipiga mlegezo na kutinga club mnaona mmomonyoko wa Maadili ila vizee kuja kushindana na vijana humu mnaona poa tuu. Busara zinahitajika kwenye familia yenu umri wa kujenga nchi umeshawapita tulieni majumbani na muwafundishe watoto na wajukuu zenu wasijekupotea kama mlivyopotea nyinyi
Waungwana huyu sio yule MPIGA MSULI wa chuo cha ushirika moshi aliyekimbiaga ID yake hapa?,maana anavyokomalia vitu visivyo muhusu ni kama yeye amekuja kivingine na ID nyingine,huyu wa kupuuzwa tu,tueendelee na yetu
 
Imekuchoma nini? Asilimia kubwa ya hao waliokuwa secondary miaka ya 80 wanapiga kelele kuwa maisha magumu serikali imewaletea umaskini. We jaribu kufuatilia comments zao uone.

Kama ulianza miaka ya 80 ulikuwa secondary na upo humu JF jua we ni maskini. Na hauwezi tena kuwa kama bill gates huu ni muda wetu sisi tuliozaliwa miaka hiyo nyie mkiwa secondary
we mkorofi
 
Je Puza asingejiuwa angekuwa mtu wa aina gani leo hii?
Angekuwa ni kiongozi mashuhuri au angekuwa jela?
Saa zingine inabidi tujiulize kuwa baada ya kifo tunaacha historia gani kwa kizazi kijacho.

Wakati Puza anahangaika na fujo kuna wanafunzi wengine ambao hawakuwa na majina pale Tambaza walikuwa wanahangaika na masomo na mungu si athumani wengine wamekuwa wanasheria, madaktari nk.

Napenda kujua hatima ya wababe wengine wa Tambaza kama akina Buchiza,Bedui, Emmanuel Mbwili, Tyson nk
 
Mkuu wa shule unamuongelea Julius Mushi? Au nyie mlikuta Mushi kashaondoka?

Nasikia Julius Mushi alifariki.

Mzee anakwambia "You should never let me catch you without a good book".

Mr. Julius Mushi ukimwambia Tambaza wamefanya fujo wameua watu yeye anakugeuzia kibao, anakwambia "mimi wa kwangu walioumizwa wangapi na wako wapi?"

Nilivyomsikia anasema hivyo tu nikamsamehe unoko wake woote mshua yule. Alikuwa anakunja uso kama ananyonya limao, Mushi hacheki hata siku moja alivyo mkuda.
Mkuu Kiranga,
kwa kiasi kikubwa mwalimu Mushi ndiye aliyeharibu spirit ya Tambaza, mimi nimekuwa pale chini ya Head Master Kalumuna na baadaye Mwl Julius Mushi (RIP)

Baada ya Kalumuna kuhamishiwa Makongo tukaletewa Mushi. - akitokea Forodhani Secondary, kwa mara ya kwanza tukaanza kushuhudia suspension na kufukuzwa wanafunzi shuleni, na wazazi kuitwa tukaanza kuchapwa parade na wazazi mbele ya shule.
Nakumbuka kipindi cha Kalumuna, mwanafunzi wake alikuwa hakamatwi kijinga na polisi/ vyombo vya usalama , iwapo itatokea mwanafunzi kakinukisha huko mtaani kwa kondakta atafika polisi atahoji huyu mwanafunzi alifanya hilo tukio saa ngapi? Akiambiwa ni say saa 4 atajibu hapana muda huo mwanafunzi wangu alikuwa darasani, na kesi inaishia hapo.
 
Mkuu Kiranga,
kwa kiasi kikubwa ndiye aliyeharibu spirit ya Tambaza, mimi nimekuwa pale chini ya Head Master Kalumuna na baadaye Mwl Julius Mushi (RIP)

Baada ya Kalumuna kuhamishiwa Makongo tukaletewa Mushi. - akitokea Forodhani Secondary, kwa mara ya kwanza tukaanza kushuhudia suspension na kufukuzwa wanafunzi shuleni, na wazazi kuitwa tukaanza kuchapwa parade na wazazi mbele ya shule.
Nakumbuka kipindi cha Kalumuna, mwanafunzi wake alikuwa hakamatwi kijinga na polisi/ vyombo vya usalama , iwapo itatokea mwanafunzi kakinukisha huko mtaani kwa kondakta atafika polisi atahoji huyu mwanafunzi alifanya hilo tukio saa ngapi? Akiambiwa ni say saa 4 atajibu hapana muda huo mwanafunzi wangu alikuwa darasani, na kesi inaishia hapo.
Mi naikumbuka Tambaza ya wapiga kitabu cha nguvu.Hayo mengine ya ubabe na kutifuana na makondakta na polisi hayakuwa na tija sana.
 
Upo sahihi, Tambaza ilikuwa na sura mbili, hio unayoikumbuka wewe na hii tunaijadiri sasa.

Huo ubabe wao ulikuwa unafanywa na hao hao wapiga kitabu.
Kuna tetesi kuwa wababe wengi wa enzi zile siku hizi wengi wameamua kuokoka na kumrudia bwana.
 
Back
Top Bottom