Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe si ulikoswakoswa kupigwa mtama karibu na Azania? Kama nakukumbuka hiviNikiwa form one Tambaza 1994 nilivuliwa viatu na kunyang'anywa pesa na mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Dictator akiwa na mwenzake aitwaye Bedui.Aliyetoa wazo la kufuta O level Tambaza ashukuriwe maana nilichaguliwa tena Tambaza A level 1998 shule ilikuwa imebadilika.Mabronso na masistadu walikuwa wa kutosha.
Huyu dogo ni wa kum-ignore,hakika uzi umempwelepweta,tumfananishe na mtu asiyejua kuogelea halafu akatupwa bahari ya pacific.Dogo wala usihangaike. Mimi nimekudharau tu. Maana hata word order kwenye sentence yako imekushinda. I won't argue with you
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Wewe si ulikoswakoswa kupigwa mtama karibu na Azania? Kama nakukumbuka hivi
.....acha kuua soo kipusti we chocolate!...
Huyu wajimila hakuwahi kuwa pugu miaka 91 to 93?Ni kweli, nimekumbuka.Baadae Wajimila (R.I.P)alienda Kibiti kuwa mkuu wa shule.
Siku hizi wanakula sana chips.. Wanakuambia zikausheemiaka hiyo azania na tambaza vijana walikua machachari na akili zao zilikua machachari ila sasa azania na tambaza zimepoa na vijana akili zao zimekua baridiii, matokeo yao yanatuumiza sana tuliosona ktk shule hizi huko nyuma
Dogo we kiazi sana aisee..humu ndani wapo kina nape mwigulu mbowe na wanasiasa wakubwa..Lazima tulete nyodo. Watu hatujazaliwa nyie mko secondary leo tupo wote JF tunachati. Kuna sehemu mtakuwa mmekosea lazima naelewa nw kwanini wengi humu hamuipendi CCM.
Dogo kwa vile yupo JF anajifananisha na kina nyani ngabu mwanakijiji nape mbowe dr slaa mwiguli etc..Kwan kua jf ni kua ni kwamba mtu ume lost...kijana kijana nadhan umekosea njia saiz yako ni fb...kwa taarifa yako watu wote makin wapo humu jf..vikojoz kama ww mmekuja humu kwa bahat mbaya!
Dogo anashindwa kutofautisha mnyama na mduduHahahahaaa,uachage utundu bathi,eti mnyama scorpion, scorpion mdudu bhanaa...
Huyo puza ndo mnyama.
Team wema huyoHuu muzik sio wake mwambie aende fb akapost picha yupo beach!
Dogo unaijua Jf kweli wewe team wemaImekuchoma nini? Asilimia kubwa ya hao waliokuwa secondary miaka ya 80 wanapiga kelele kuwa maisha magumu serikali imewaletea umaskini. We jaribu kufuatilia comments zao uone.
Kama ulianza miaka ya 80 ulikuwa secondary na upo humu JF jua we ni maskini. Na hauwezi tena kuwa kama bill gates huu ni muda wetu sisi tuliozaliwa miaka hiyo nyie mkiwa secondary
Huo mwaka Hata nilikuwa bado sijazaliwa,
Kwani Huyo Puza Anaingia kwa mnyama
SCORPION ?
Puza Fala,Kwa nini mkuu ? Funguka
Matola kumbe we mtoni kitambo eeKipindi hiki wakati kina Puza Wanajivunia ujinga hata mimi nilikuwa O level, ndio kilikuwa kipindi cha kwenda Zenj na passport, kwenda UK bila viza ilikuwa unakata tu ticket unakipa kitu, na walioingia UK kipindi hicho karibu wote sasa hivi wana uraia.
Michongo ya kwenda Marekani ilikuwa kwa summer Camp na Jambo lee kupitia boy scout hakika nimekumbuka zamani.
Kuna walimu waliniwekea bifu za kitoto kisa navaa mokasini za dukani maduka ya samora avenue wao wanavaa bora shoes.
Ila ilinishangaza zaidi kipindi chetu mafisadi walikuwa mafisadi kweli watoto zao walikuwa wanadrive magari kuja nayo shule kuanzia form one mpaka form four.
Kampani yangu ya kutokea mtaani ilikuwa wote wapo Tambaza mimi nilikuwa ni mmoja ya wanafunzi wachache tuliokuwa tunaingia Tambaza na uniform za shule nyingine na tulikuwa powa na msosi wa bure wa shule nilikuwa napiga bila kubaguliwa.
Namkumbuka mshikaji mmoja wanamuita kiuno jina lake nimemsahau alikuwa karibu na kina Saigon wa Diplomats huyu jamaa alikuwa anatisha kwenye kucheza na gari.
Wakati kina Puza wanatamba na usela mavi wao mimi nilijiongeza kwa watoto wa kishuwa tukitoka na mikoko ya madingi zao breki Forodhani secondary school kwa mademu wenye TBS.