Mkuu unaikumbuka ile game ya UMISETA ilipigwa pale Azania sec. ground kati ya Azania na Tambaza mwaka 1988? Sikumbuki kama ule mchezo ulimalizika ila iliibuka fujo kubwa sana siku hiyo,tambaza walikimbizwa pale Azania ila mtaani kukawa na msako mkali wa kuwasaka wanafunzi wenye kaptula za kaki (karibu wiki nzima),msako ukiendeshwa na wale wa kaptula za kijivu....nikiwa form one sijasahau kile kizaa zaa cha mabomu ya chupa zilizojazwa petrol na sukari na utambi.....,vijana wa kijivu wakianza fujo walikuwa wanatoa mlio fulani wakiuita "mlio wa tembo"....,ila wakifika shule wanapiga kitabu na kufaulu vizuri tu.