MkuuJe Puza asingejiuwa angekuwa mtu wa aina gani leo hii?
Angekuwa ni kiongozi mashuhuri au angekuwa jela?
Saa zingine inabidi tujiulize kuwa baada ya kifo tunaacha historia gani kwa kizazi kijacho.
Wakati Puza anahangaika na fujo kuna wanafunzi wengine ambao hawakuwa na majina pale Tambaza walikuwa wanahangaika na masomo na mungu si athumani wengine wamekuwa wanasheria, madaktari nk.
Napenda kujua hatima ya wababe wengine wa Tambaza kama akina Buchiza,Bedui, Emmanuel Mbwili, Tyson nk
Wewe ni Tambaza family?
Nimemkumbuka Buchiza nimesmile, tulikuwa tunamuita Kisimba "juu mnene chini mwembamba", alikuwa na physic ya kivyake kila akipiga nondo anajaza kifuani chini anaslim!
Anyway, jamaa alikuwa mtoto wa mboga saba anakaa quarters/ maflat ya Bank/ kama siyo Bima pale Kisutu/zanaki, alikuwa akitongoza mademu walikuwa wanamuogopa sababu ya ule mwili, uvaaji wa kaptura kiasi fulani ulikuwa unamexpose na kuharibu haiba yake - miguu ilikuwa mwembamba na juu mnene mno, Ngoja niishie hapo kwanza maana hatufahamu yupo wapi asije kuwa ndiye afisa anayesimamia masuala cyber crime.