Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Siku zote huwa nawaambia hawa watoto humu hatujuani kwa sababu ya hizi I'D zetu. Ila tukishaingia huko PM na kutambulishana tunabaki kushangaana. Respect kila ID unayokutana nayo humu.
Hapa JF kuna jamaa niliandikiana nay PM kumbe ni DR wa muhimbili ..
Alinisaidia sana.. Hasa kwenye uzi kama huu wengi sana ni watu wakubwa manake wengi walipiga kitabu zamani sana na walikiwa vichwa so wako mbali now..
Zamani shule zilikuwa chache competition kubwa sana kwa hio vichwa ndio vilikuwa shule sio sa hivi hadi viazi vipo shule
 
Daah JF raha sana... Asanteni kiranga na vichwa vingine kwenye huu uzi...
 
Mliletwa Karatu sec mkaibua issue kwa kumtwanga mwalimu baada ya kumfumania akimgegeda demu kwenye kichaka. Kilichofuata vijana wote waliotoka Tambaza mkamriwa kufungua matranka na wakakuta barua za mademu na maboyfriends.
 
Duh, bonge la memory, kipindi hicho Makonda wakiona Kaptula ya khaki wala hawasumbuki kuwazuia wanafunzi, kuna basi za Ubungo zile "Shella Beach" lile bench la nyuma lilikuwa special kwa wana Tambaza

Sitasahau Mechi ya Tambaza na Kino Muslim, pale kiwanja cha Muhimbili Primary, Mechi ilivunjika na Wanafunzi wa Kinondoni wakakimbizwa mpaka shuleni kwao Na lile bango la shule ya kinondoni likashushwa chini

Kino Muslim ndio shule pekee iliyokuwa na watoto wa kitaa na wahuni wa kweli na ndio shule hata Tambaza walikuwa wanaingia kwa kujihami
 
Mkuu wa shule unamuongelea Julius Mushi? Au nyie mlikuta Mushi kashaondoka?

Nasikia Julius Mushi alifariki.

Mzee anakwambia "You should never let me catch you without a good book".

Mr. Julius Mushi ukimwambia Tambaza wamefanya fujo wameua watu yeye anakugeuzia kibao, anakwambia "mimi wa kwangu walioumizwa wangapi na wako wapi?"

Nilivyomsikia anasema hivyo tu nikamsamehe unoko wake woote mshua yule. Alikuwa anakunja uso kama ananyonya limao, Mushi hacheki hata siku moja alivyo mkuda.
 
Waungwana huyu sio yule MPIGA MSULI wa chuo cha ushirika moshi aliyekimbiaga ID yake hapa?,maana anavyokomalia vitu visivyo muhusu ni kama yeye amekuja kivingine na ID nyingine,huyu wa kupuuzwa tu,tueendelee na yetu
 
we mkorofi
 
Alijiua mwenyewe..ila sababu ndo haijulikani...jamaa alikuwa mtemi sana..kaanza kuonyesha utemi toka yuko form one anadindishiana na form four
Naskia scorpion ni mdogo wake
 
Je Puza asingejiuwa angekuwa mtu wa aina gani leo hii?
Angekuwa ni kiongozi mashuhuri au angekuwa jela?
Saa zingine inabidi tujiulize kuwa baada ya kifo tunaacha historia gani kwa kizazi kijacho.

Wakati Puza anahangaika na fujo kuna wanafunzi wengine ambao hawakuwa na majina pale Tambaza walikuwa wanahangaika na masomo na mungu si athumani wengine wamekuwa wanasheria, madaktari nk.

Napenda kujua hatima ya wababe wengine wa Tambaza kama akina Buchiza,Bedui, Emmanuel Mbwili, Tyson nk
 
Mkuu Kiranga,
kwa kiasi kikubwa mwalimu Mushi ndiye aliyeharibu spirit ya Tambaza, mimi nimekuwa pale chini ya Head Master Kalumuna na baadaye Mwl Julius Mushi (RIP)

Baada ya Kalumuna kuhamishiwa Makongo tukaletewa Mushi. - akitokea Forodhani Secondary, kwa mara ya kwanza tukaanza kushuhudia suspension na kufukuzwa wanafunzi shuleni, na wazazi kuitwa tukaanza kuchapwa parade na wazazi mbele ya shule.
Nakumbuka kipindi cha Kalumuna, mwanafunzi wake alikuwa hakamatwi kijinga na polisi/ vyombo vya usalama , iwapo itatokea mwanafunzi kakinukisha huko mtaani kwa kondakta atafika polisi atahoji huyu mwanafunzi alifanya hilo tukio saa ngapi? Akiambiwa ni say saa 4 atajibu hapana muda huo mwanafunzi wangu alikuwa darasani, na kesi inaishia hapo.
 
Mi naikumbuka Tambaza ya wapiga kitabu cha nguvu.Hayo mengine ya ubabe na kutifuana na makondakta na polisi hayakuwa na tija sana.
 
Upo sahihi, Tambaza ilikuwa na sura mbili, hio unayoikumbuka wewe na hii tunaijadiri sasa.

Huo ubabe wao ulikuwa unafanywa na hao hao wapiga kitabu.
Kuna tetesi kuwa wababe wengi wa enzi zile siku hizi wengi wameamua kuokoka na kumrudia bwana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…