Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Dah nikiwa Airwing nilikua naskia story zake mpaka alipofariki
 
Duh, umenikumbusha Busianya mzee wa Fegi na anaongea kwa pozi na kujiamini sana, na ndie aliyetangaza Msiba wa Puza, maana Puza alijiua wakati wa likizo na tulipofungua tu yeye ndiye aliyetangaza
Pamoja na hayo yote hakuwahi kuwa Head master Tambaza, alikuwa second Master , maana baada ya Mushi kuchemsha Mziki wa TSS kijiti alipewa Mtela
Mkuu
Busanya alikuwa ni mwanamke, yeye alihamishiwa Forodhani kuwa Head mistress.
Huyo mvuta fegi alikuwa anaitwa Hawanga, yeye na Mushi ndio walishindwa kuihimili Tambaza, matokeo yake ndio tunayoyaona leo.
 
Sawa kaka majina yalinichanganya kidogo, umri nao umeenda haya tunayoyaongea yametokea miaka 27-30 iliyopita, ni vile nafsi haizeeki tu, maana nikifumba macho nayaona matukio kama yametokea jana tu, kweli bwana alikuwa anaitwa Hawanga na baada ya hapo Tambaza nadhani aliendaga Navy Kigamboni
 
Ha ha ha kitambo Sana daah...nakumbuka uuzwaji wa kiwanja cha mpira kutoka Tambaza kwenda muhimbili Primaly..mkaguzi wa Elimu sec Alexzander Ndeki akaja mkutanoni akamwaga data...,namkumbuka,Puza,Sagapower,Vimto..... Makamu WA shule Mr Wajimira,yule mzee aliyekuwa mkuu WA shule jina nimemsahau....baada ya fujo na Azania 1994,form wote tukasimamishwa shule mwaka nzima...mwaka uliofuata tukaperekwa shule za mikoani,...form one yetu ya 1993 ilikuwa na watu wakorofi Sana...
Nakumbuka group iliyoletwa Kwiro boys kutoka Tambaza tuliwapokea getini kwa kuwapiga kwenzi Na kuwarusha vichura sana, hatukutaka ujinga kabisa!!!
 
Mwaka 1988 mechi ya Tambaza na Azania ilipigwa uwanja wa magunia msasani ambapo wanafunzi wa Azania na mwalimu wao wa michezo rwegoshora waliangushiwa kipigo cha mbwa mwaka 1989 mechi hii ilipigwa ndani ya uwanja wa Azania refa rii akiwa kanali kipingu baada mechi Azania walilazimika kuvua kaptula za khaki na kutembea kwa miguu adi majumbani kwao ili kunusuru maisha yao!
Wapi kaka Pascal Mayala atupe michapo ya Tambaza ya akina shetani, no-mbungi, Okelo, chapa?
Huyu ni rwegoshora ambaye siku hizi ni mkaguzi hapo st Anne Marie? Maana naskia alifundisha Azania maths na Physics
 
Sawa kaka majina yalinichanganya kidogo, umri nao umeenda haya tunayoyaongea yametokea miaka 27-30 iliyopita, ni vile nafsi haizeeki tu, maana nikifumba macho nayaona matukio kama yametokea jana tu, kweli bwana alikuwa anaitwa Hawanga na baada ya hapo Tambaza nadhani aliendaga Navy Kigamboni
Kweli kaka

Ni muhimu kurekebishana - maana nasikia kwenye uhakiki wa vyeti unaulizwa hadi walimu wako waliokufundisha.
 
Mwaka 1988 mechi ya Tambaza na Azania ilipigwa uwanja wa magunia msasani ambapo wanafunzi wa Azania na mwalimu wao wa michezo rwegoshora waliangushiwa kipigo cha mbwa mwaka 1989 mechi hii ilipigwa ndani ya uwanja wa Azania refa rii akiwa kanali kipingu baada mechi Azania walilazimika kuvua kaptula za khaki na kutembea kwa miguu adi majumbani kwao ili kunusuru maisha yao!
Wapi kaka Pascal Mayala atupe michapo ya Tambaza ya akina shetani, no-mbungi, Okelo, chapa?
Mkuu uko vizuri sana kumbu kumbu!
 
Je Puza asingejiuwa angekuwa mtu wa aina gani leo hii?
Angekuwa ni kiongozi mashuhuri au angekuwa jela?
Saa zingine inabidi tujiulize kuwa baada ya kifo tunaacha historia gani kwa kizazi kijacho.

Wakati Puza anahangaika na fujo kuna wanafunzi wengine ambao hawakuwa na majina pale Tambaza walikuwa wanahangaika na masomo na mungu si athumani wengine wamekuwa wanasheria, madaktari nk.

Napenda kujua hatima ya wababe wengine wa Tambaza kama akina Buchiza,Bedui, Emmanuel Mbwili, Tyson nk
Wababe wa enzi hizo na kichwani zilikuwemo. Walichofanya ni mambo ya umri wao na mazingira yao. Yasemekana katika shule hizo kulikuwa na watoto wa kishua na watoto wa kitaa pia na kila mmoja alijiona ni sehemu ya familia hiyoo. Kulikuwa na tofauti kati ya shule hizo za wagumu na zile za mchanganyiko kama Forodhani na Kibasila. Ni watu wa maana katika jamii yetu na wala si wa hovyoo! !
 
Hapo Juma Bios na Lulindi Swahili, unamkumbuka mwalimu wa Siasa Manyasi?
Huyu Lulindi alikuwa burudani sana watu walikuwa wanazamia hadi kipindi chake anapokuwa darasa jingine!
 
Tambaza na KINONDON Muslim hapo palikuwa hapatoshi kabisa miaka hyo nikiwa muslim pale
 
Nimesoma comments zote maana kipindi cha vurugu za Tambaza nilikua shule ya msingi.
Tulikua tunalindwa na Polisi getini.
90-94 nilikua la pili hadi la 6

Mwalimu Lulindi mzee wa Porojo kanifundisha Civics O'level
 
Back
Top Bottom