Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Duh! Mkuu umenikumbusha huyu jamaa jinsi alivyokuwa anawadhibiti makondakta wa daladala waliokuwa wanatunyanyasa madent wa miaka ile,manake jamaa alikuwa na mbavu na walikuwa wanamhanya hasa,niliwahi kushuhudia moja ya valangati zake pale ubungo minazi ambapo ndipo palipokuja kuwa kituo cha ubungo (wakati huo kituo cha ubungo kiko pale ubungo maji)jamaa aliwadhibiti kondakta na dereva wa daladala moja ikijulikana kwa jina la TORINO huku akitoa onyo kwa wanafunzi wasiingilie kwani atawamudu peke yake,na kweli aliwatuliza makonda wawili na dereva wao.Ila utakuwa umechanganya(?) sidhani kama kifo chake kilikuwa 1992,kama sio mwaka 1990 ilikuwa 1991 nadhani alikuwa kidato cha pili by then,pia umenikumbusha sonda boy bila kumsahau Okelo.
Long time, sana nakumbuka JADIDE,
 
Ulipigiwa kura nyingi za utukutu kwa sababu ya macho yako mekundu!!!!ah ha!!
Mimi nilkuwa sesssion two na red lebo, but nakumbuka madarasa ya commerce yalikuwa mawaili tu U na z, mengine kma R, T, M yalikuw sayansi....nakumbuka tulikuwa streams 6 za red na 6 green ndio kumbukumbu yangu. nikumbesheni wadau...!! zaman tuliokuwa wakali wa hesabu primary ndio tulkuwa Tambaza....madem zetu wa zanaki ya tukiitana "TambaZana" . Ukikutana na mtoto wa zanaki tabasam hilo....!! ndio kipind soda ya sprite ndio imetoka miaka ya 90 na tunakuja shule na mzinga wa konyagi na kujichimbia mitaa ya mazengo kuna viduka fulani tunamix na sprite, na sigara unanunua pakt linaisha lote siku hyo hyo....
Mushi ndio alikuja kuharibu ile shule akitokea forodhani, alikuwa anakugua mpka maua wakati mwenzake Kalumuna akikuta mtaani muda wa masomo, akikushika utamsikia "turudi shulen kijana" kwa sauti ya kihaya.....
Binafsi nilishalala lock-up msimbazi mara tatu....na katika zoez la kura za waarifu wa shule nilipata kura nyngi sana ..hadi mushi aliuliza unagombea ubunge wapi??/
Tilipigwa viboko sana mpka uokozi ulifanywa na mkuu wa majeshi meja kiaro kwa kuwa mwanae ernest tulikuwa nae,,,, mwenyekiti wa bodi mama kijakazi kihelula (marehemu) alikuja kumaliza mambo.

Tambaza ndio chanzo cha maarifa kwangu......sumit juu ndio place ya kula msuba.....!!!
 
Mkuu unaikumbuka ile game ya UMISETA ilipigwa pale Azania sec. ground kati ya Azania na Tambaza mwaka 1988? Sikumbuki kama ule mchezo ulimalizika ila iliibuka fujo kubwa sana siku hiyo,tambaza walikimbizwa pale Azania ila mtaani kukawa na msako mkali wa kuwasaka wanafunzi wenye kaptula za kaki (karibu wiki nzima),msako ukiendeshwa na wale wa kaptula za kijivu....nikiwa form one sijasahau kile kizaa zaa cha mabomu ya chupa zilizojazwa petrol na sukari na utambi.....,vijana wa kijivu wakianza fujo walikuwa wanatoa mlio fulani wakiuita "mlio wa tembo"....,ila wakifika shule wanapiga kitabu na kufaulu vizuri tu.
Nyau mkuu
 
1. Puza hakujinyonga but alikunywa dawa (sifahamu kama kunywa dawa nyingi ni kujinyonga).

2. Jamaa, hakuwa na murder case yoyote, he was mtukutu tu kama ilivyokuwa watukutu wengine pale shule.

3. Kama ulivyosema mwenyewe, hakuna anayefahamu hadi sasa ni sababu zipi zilizopelekea jamaa kujiua kwa kunywa na zile dawa (wengine walidai kuwa alipima akakuta ameathirika hivyo hakupenda kushuhudia yale mathila) - maana aliamka akafagia uwanja na kumwambia mother wake kuwa nasafisha/ fagia uwanja maana kesho rafiki zangu watafika hapa kupiga story and ndio akajiua.
"Nafagia uwanja,kesho rafik zangu watakuja kupiga story hapa"
Jamaa kweli alikuwa mtukutu!
 
Na alikuwa na mapenzi tambaza toka yuko primary Ubungo nakumbuka kulikuwa na tifu kati ta tambaza na wanafunzi wa shule moja ya sec jioni ubungo ambao walikuwa wana tumia majengo ya primary na sisi tulikuwa tuna jisomea jioni pale .
Wale wapuuzi wa za kuungaunga elimu wakawa wanasumbua dogo wa primary akiwemo puza ,wadau wa tambaza wakaingilia kati na kutia discipline kukawa hakuna masomo siku hiyo ,na puza akasema anaombea akifanya vyema awe tambaza na ikawa hivyo.
Umenikummbusha enzi za mwl Banda Ubungo NH
 
Nakumbuka siku ya kwanza tume report form I tukachapwa sana bakora na form II na kumwagiwa mikojo...then assembly akaja Head master Kalumuna akawauliza form II kama wametukaribisha na kutupokea vizuri! Na wao kwa pamoja wakajibu baadooo! Then K akasema..basi mtaendelea kuwakaribisha tena baadae...Form wakaendelea kushangilia kinoma! Form I tunajiuliza hii shule au kambi ya jeshi! Then Kuna form I mmoja baada ya kuchapwa na form II akaenda kwa mwalimu wa michezo Daffa kulalamika huku analia...jibu alilopewa Dafa ni" Changamka kinjuka wewee !!!Tambaza ulichagua mwenyewe!!! Hah ah! Mi kuona hivyo week nzima ya kwanza naishia kwa Daruweshi mtaa Aggrey nasingizia nasubiri kaptula za kaki!! It was memorable time I can't forget Tambaza!!!!
Kulikuwa na kikundi kinaitwa Barcelona na Huyu Puza alikuwa member au nachanganya habari?
nimekumbuka mbali sana. Siku moja mchana jamaa walikuja pale azania wakamwaga wali wote ambao tulikuwa tunajiandaa kula
 
Oyaa form two yupi aliyedundwa? To be honest katika kumbukumbu zangu jamaa hajawahi kupigana na Tambaza mwenzake, Tambaza walikuwa na spirit ya "one family ndani na nje ya shule kama wana Tambaza".

Ila mtu wa nje alikuwa hagusi hio familia ya Tambaza, hata kama utamuonea mwana Tambaza ukajificha basi utatafutwa mpaka upatikane na ujute.

Nitakukubalia iwapo utasema alimkung'uta form two wa Azania, Jitegemee au Vituka secondary maana enzi hizo hao ndio walikuwa wapinzani wa ile familia.
Tambaza walikuwa watundu sana kwenye mechi mkuu wao anasema "vijana msishindwe ndani na nje ya uwanja" basi taabu tupu. Ila mlikuwa mnawapenda sana Kibasila sijui kwakuwa kina Salvatory Edward walikuwa wanawakosha sana
 
Kipindi hiki wakati kina Puza Wanajivunia ujinga hata mimi nilikuwa O level, ndio kilikuwa kipindi cha kwenda Zenj na passport, kwenda UK bila viza ilikuwa unakata tu ticket unakipa kitu, na walioingia UK kipindi hicho karibu wote sasa hivi wana uraia.
Michongo ya kwenda Marekani ilikuwa kwa summer Camp na Jambo lee kupitia boy scout hakika nimekumbuka zamani.

Kuna walimu waliniwekea bifu za kitoto kisa navaa mokasini za dukani maduka ya samora avenue wao wanavaa bora shoes.

Ila ilinishangaza zaidi kipindi chetu mafisadi walikuwa mafisadi kweli watoto zao walikuwa wanadrive magari kuja nayo shule kuanzia form one mpaka form four.

Kampani yangu ya kutokea mtaani ilikuwa wote wapo Tambaza mimi nilikuwa ni mmoja ya wanafunzi wachache tuliokuwa tunaingia Tambaza na uniform za shule nyingine na tulikuwa powa na msosi wa bure wa shule nilikuwa napiga bila kubaguliwa.

Namkumbuka mshikaji mmoja wanamuita kiuno jina lake nimemsahau alikuwa karibu na kina Saigon wa Diplomats huyu jamaa alikuwa anatisha kwenye kucheza na gari.

Wakati kina Puza wanatamba na usela mavi wao mimi nilijiongeza kwa watoto wa kishuwa tukitoka na mikoko ya madingi zao breki Forodhani secondary school kwa mademu wenye TBS.
Mkuu Matola mi miaka hiyo nilikuwa forodhani, nakumbuka tulikuwa double session
Mkuu
Busanya alikuwa ni mwanamke, yeye alihamishiwa Forodhani kuwa Head mistress.
Huyo mvuta fegi alikuwa anaitwa Hawanga, yeye na Mushi ndio walishindwa kuihimili Tambaza, matokeo yake ndio tunayoyaona leo.
Nadhani wali exchange Mushi alitoka forodhani kuwa headmaster tambaza then Busianya ndo akawa headmaster Forodhani
 
Kama ulivyosema mwenyewe, hakuna anayefahamu hadi sasa ni sababu zipi zilizopelekea jamaa kujiua kwa kunywa na zile dawa (wengine walidai kuwa alipima akakuta ameathirika hivyo hakupenda kushuhudia yale mathila) - maana aliamka akafagia uwanja na kumwambia mother wake kuwa nasafisha/ fagia uwanja maana kesho rafiki zangu watafika hapa kupiga story and ndio akajiua.
hii naikumbuka na inadaiwa alikuwa mtoto mtulivu na mtiifu nyumbani
 
Mkuu
Wewe ni Tambaza family?

Nimemkumbuka Buchiza nimesmile, tulikuwa tunamuita Kisimba "juu mnene chini mwembamba", alikuwa na physic ya kivyake kila akipiga nondo anajaza kifuani chini anaslim!

Anyway, jamaa alikuwa mtoto wa mboga saba anakaa quarters/ maflat ya Bank/ kama siyo Bima pale Kisutu/zanaki, alikuwa akitongoza mademu walikuwa wanamuogopa sababu ya ule mwili, uvaaji wa kaptura kiasi fulani ulikuwa unamexpose na kuharibu haiba yake - miguu ilikuwa mwembamba na juu mnene mno, Ngoja niishie hapo kwanza maana hatufahamu yupo wapi asije kuwa ndiye afisa anayesimamia masuala cyber crime.
Allitwa Buchiza Mtaita, long time sana,
 
Tambaza kitambo enzi hizo kuna walimu kama Juma, Lululindi, etc . Wadogo zetu mtusamehe wakubwa mizuka imetokana.
Umenikumbusha mbali mkuu. Lulindi ticha wa kiswahili. Stori na vichekesho kibao!
 
Mkuu unaikumbuka ile game ya UMISETA ilipigwa pale Azania sec. ground kati ya Azania na Tambaza mwaka 1988? Sikumbuki kama ule mchezo ulimalizika ila iliibuka fujo kubwa sana siku hiyo,tambaza walikimbizwa pale Azania ila mtaani kukawa na msako mkali wa kuwasaka wanafunzi wenye kaptula za kaki (karibu wiki nzima),msako ukiendeshwa na wale wa kaptula za kijivu....nikiwa form one sijasahau kile kizaa zaa cha mabomu ya chupa zilizojazwa petrol na sukari na utambi.....,vijana wa kijivu wakianza fujo walikuwa wanatoa mlio fulani wakiuita "mlio wa tembo"....,ila wakifika shule wanapiga kitabu na kufaulu vizuri tu.
hii game kama kumbukumbu zangu ziko vizuri, ilichezwa 1989. maana naikumbuka vizuri sana na mi nlikuwa mhanga wa kaptura za kaki.
 
Na alikuwa na mapenzi tambaza toka yuko primary Ubungo nakumbuka kulikuwa na tifu kati ta tambaza na wanafunzi wa shule moja ya sec jioni ubungo ambao walikuwa wana tumia majengo ya primary na sisi tulikuwa tuna jisomea jioni pale .
Wale wapuuzi wa za kuungaunga elimu wakawa wanasumbua dogo wa primary akiwemo puza ,wadau wa tambaza wakaingilia kati na kutia discipline kukawa hakuna masomo siku hiyo ,na puza akasema anaombea akifanya vyema awe tambaza na ikawa hivyo.
dah, nilikuwepo hii siku ilikuwa balaa na nilikuwa na kamwili kadogo kadogo ni mbio tu zilinisaidia. nilisoma ubungo, evening class mwaka mzima.
 
Huyu jamaa nilimsikiaga sana sifa zake kipindi nipo darasa la kwanza 1991 pale Mtendeni Primary kutoka kwa bamdogo wng Mwl Daffa aliyekua mwl wa michezo pale Tambaza na baadae akawa mwl wa biashara na alikuwa anasemaga kuwa ile ishu ya kubomoa ukuta wa Muhimbili primary wao walimu ndo walichochea hiyo ishu
 
Tambaza walikuwa watundu sana walimwita mstaafu shemeji aliopoa mototo wa meya Kitwana Kondo
 
....kwa mkwara tu nakumbuka siku moja alikua anampiga biti demu wa jangwani et akajichanja na wembe halaf akailamba damu yake....jamaa alikua nunda sana...sa sijui hio roho ya uoga ya kujiua ilikujaje aisee

What we have to fear is fear itself.
 
Hii ni thread maalumu kabisa kwa wahenga.
 
Niliingia form one AZANIA WAKATI HUO TAMBAZA IMEFUTWA O LEVEL nasikitika kutomjua huyo puza ila nilisikia story zake
 
Back
Top Bottom