Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Dah nikiwa Airwing nilikua naskia story zake mpaka alipofariki
 
Mkuu
Busanya alikuwa ni mwanamke, yeye alihamishiwa Forodhani kuwa Head mistress.
Huyo mvuta fegi alikuwa anaitwa Hawanga, yeye na Mushi ndio walishindwa kuihimili Tambaza, matokeo yake ndio tunayoyaona leo.
 
Mkuu
Busanya alikuwa ni mwanamke, yeye alihamishiwa Forodhani kuwa Head mistress.
Huyo mvuta fegi alikuwa anaitwa Hawanga, yeye na Mushi ndio walishindwa kuihimili Tambaza, matokeo yake ndio tunayoyaona leo.
Sawa kaka majina yalinichanganya kidogo, umri nao umeenda haya tunayoyaongea yametokea miaka 27-30 iliyopita, ni vile nafsi haizeeki tu, maana nikifumba macho nayaona matukio kama yametokea jana tu, kweli bwana alikuwa anaitwa Hawanga na baada ya hapo Tambaza nadhani aliendaga Navy Kigamboni
 
Nakumbuka group iliyoletwa Kwiro boys kutoka Tambaza tuliwapokea getini kwa kuwapiga kwenzi Na kuwarusha vichura sana, hatukutaka ujinga kabisa!!!
 
Huyu ni rwegoshora ambaye siku hizi ni mkaguzi hapo st Anne Marie? Maana naskia alifundisha Azania maths na Physics
 
Kweli kaka

Ni muhimu kurekebishana - maana nasikia kwenye uhakiki wa vyeti unaulizwa hadi walimu wako waliokufundisha.
 
Mkuu uko vizuri sana kumbu kumbu!
 
Wababe wa enzi hizo na kichwani zilikuwemo. Walichofanya ni mambo ya umri wao na mazingira yao. Yasemekana katika shule hizo kulikuwa na watoto wa kishua na watoto wa kitaa pia na kila mmoja alijiona ni sehemu ya familia hiyoo. Kulikuwa na tofauti kati ya shule hizo za wagumu na zile za mchanganyiko kama Forodhani na Kibasila. Ni watu wa maana katika jamii yetu na wala si wa hovyoo! !
 
Hapo Juma Bios na Lulindi Swahili, unamkumbuka mwalimu wa Siasa Manyasi?
Huyu Lulindi alikuwa burudani sana watu walikuwa wanazamia hadi kipindi chake anapokuwa darasa jingine!
 
Tambaza na KINONDON Muslim hapo palikuwa hapatoshi kabisa miaka hyo nikiwa muslim pale
 
Nimesoma comments zote maana kipindi cha vurugu za Tambaza nilikua shule ya msingi.
Tulikua tunalindwa na Polisi getini.
90-94 nilikua la pili hadi la 6

Mwalimu Lulindi mzee wa Porojo kanifundisha Civics O'level
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…