Kwanini Puza wa Tambaza alijiua?

Long time, sana nakumbuka JADIDE,
 
Ulipigiwa kura nyingi za utukutu kwa sababu ya macho yako mekundu!!!!ah ha!!
 
Nyau mkuu
 
"Nafagia uwanja,kesho rafik zangu watakuja kupiga story hapa"
Jamaa kweli alikuwa mtukutu!
 
Umenikummbusha enzi za mwl Banda Ubungo NH
 
Kulikuwa na kikundi kinaitwa Barcelona na Huyu Puza alikuwa member au nachanganya habari?
nimekumbuka mbali sana. Siku moja mchana jamaa walikuja pale azania wakamwaga wali wote ambao tulikuwa tunajiandaa kula
 
Tambaza walikuwa watundu sana kwenye mechi mkuu wao anasema "vijana msishindwe ndani na nje ya uwanja" basi taabu tupu. Ila mlikuwa mnawapenda sana Kibasila sijui kwakuwa kina Salvatory Edward walikuwa wanawakosha sana
 
Mkuu Matola mi miaka hiyo nilikuwa forodhani, nakumbuka tulikuwa double session
Mkuu
Busanya alikuwa ni mwanamke, yeye alihamishiwa Forodhani kuwa Head mistress.
Huyo mvuta fegi alikuwa anaitwa Hawanga, yeye na Mushi ndio walishindwa kuihimili Tambaza, matokeo yake ndio tunayoyaona leo.
Nadhani wali exchange Mushi alitoka forodhani kuwa headmaster tambaza then Busianya ndo akawa headmaster Forodhani
 
hii naikumbuka na inadaiwa alikuwa mtoto mtulivu na mtiifu nyumbani
 
Allitwa Buchiza Mtaita, long time sana,
 
Tambaza kitambo enzi hizo kuna walimu kama Juma, Lululindi, etc . Wadogo zetu mtusamehe wakubwa mizuka imetokana.
Umenikumbusha mbali mkuu. Lulindi ticha wa kiswahili. Stori na vichekesho kibao!
 
hii game kama kumbukumbu zangu ziko vizuri, ilichezwa 1989. maana naikumbuka vizuri sana na mi nlikuwa mhanga wa kaptura za kaki.
 
dah, nilikuwepo hii siku ilikuwa balaa na nilikuwa na kamwili kadogo kadogo ni mbio tu zilinisaidia. nilisoma ubungo, evening class mwaka mzima.
 
Huyu jamaa nilimsikiaga sana sifa zake kipindi nipo darasa la kwanza 1991 pale Mtendeni Primary kutoka kwa bamdogo wng Mwl Daffa aliyekua mwl wa michezo pale Tambaza na baadae akawa mwl wa biashara na alikuwa anasemaga kuwa ile ishu ya kubomoa ukuta wa Muhimbili primary wao walimu ndo walichochea hiyo ishu
 
Tambaza walikuwa watundu sana walimwita mstaafu shemeji aliopoa mototo wa meya Kitwana Kondo
 
....kwa mkwara tu nakumbuka siku moja alikua anampiga biti demu wa jangwani et akajichanja na wembe halaf akailamba damu yake....jamaa alikua nunda sana...sa sijui hio roho ya uoga ya kujiua ilikujaje aisee

What we have to fear is fear itself.
 
Hii ni thread maalumu kabisa kwa wahenga.
 
Niliingia form one AZANIA WAKATI HUO TAMBAZA IMEFUTWA O LEVEL nasikitika kutomjua huyo puza ila nilisikia story zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…