#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Unayeandika hivi, usikute hujawahi hata kuambukizwa hiyo Corona, na pengine unaposema Magufuli hakuwa Sawa katika kushughurikia Corona ukilinganisha na nchi gani ambao kwao wameshughurikia vizuri na Corona kwao haipo mpaka Leo ni Nani na nchi gani??
Naona jinsi watanzania tunavyoanza kuchemka,
Naona jinsi tunavyoanza kujikonfuse,
Nawakumbuka wanna wa Israel ,
Jinsi walipooata ukombozi kutoka misri, njia wakakutana na changamoto Kisha kumnung'unikia Mungu na Musa,
Jambo hili likamkasirisha Mungu, akawaua woote jangwani, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.
Leo hii watanzania tumefika mahali tunabeza uwezo wa Mungu katika kutulinda na kutuponya.
Hatuoni kwamba tupo hai mpaka leo, wangapi wamekufa na corona na sayansi zao na lockdown zao.
Kwanini tusimshukuru Mungu kwa ulinzi na uponyaji aliotupa..
Tunahitaji kugeuzwa Nia zetu tujue hakika yaliyo mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
 
Kila kiongozi wa nchi ni lazima afuate ushauri wa wataalamu wa tiba na afya
Dunia nzima tunaona wakipata ushauri kwa wataalamu

Nae Rais Samia ni lazima apate ushauri pia
Ataamua baada ya wataalamu ingawa imeanza kupungua katika baadhi ya nchi na wengine kudhibiti sana na sasa kupungua kiasi chake
Sidhani kama watu watafungiwa ndani ila tunaweza kutangaziwa tu kuwa ugonjwa upo na tujichunge kwa kuvaa [emoji40] na kupunguza misongamano
Najua Africa haujauwa sana ila vifo vipo
Kwahiyo kumbe hata wewe unajua wataalamu watamshauri nini kama huko kuvaa barakoa na kuepuka misongamano na hizo ndio njia zinazotumika duniani kote,sasa hilo nalo anashindwa nini kulisema sasa hadi asubiri kamati iseme?
 
Watu wangapi wamekufa ghafla kwa changamoto za upumuaji tangu mwaka huu uanze?
Ni wachache, ukilinganisha na wale waliokufa nchi zilizobobea kisayansi.
Watoto wanaendelea kusoma,
Wananchi tunaendelea na harakati za kujitafutia kipato.
Hi ndiyo faida yetu kumyegemea Mungu badala ya wanasayansi.
Maana imeandikwa,:-

Yeremia 17 : 5
BWANA asema hivi,
"Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake , Na moyoni mwake amemwacha BWANA.

Mithali 3 : 5
"Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; "
 
Mtani mimi ninachosema Rais asiseme kuwa hatukuwa na msimamo kuhusu Corona maana itakuwa ni uongo na unafiki...
Hivi kweli unafikiri kamati itamshauri nini cha ziada asicho kijua?
Au ana ajenda zake anataka kuzipenyeza kwenye mgongo wa kamati?

Kwanini avai barakoa? Huo ni msiamo gani?
Ahahahaaaa [emoji16][emoji23][emoji1787]
Huo ni msimamo wa kumuenzi mwendazake . Hata mimi nilistaajabu siku ile baada ya kuapishwa tu , aliliongoza baraza la mawaziri kwenye ukumbi mdogo pale magogoni , wote bila barakoa . Huku kukiwa na fununu kuwa mdudu huyo ndiyo katuchukulia [emoji40]

Vaa barakoa mtani acha longo longo

Odhis *
 
Kwani nani kakataa? Swala hapa ni kwanini Rais anadanganya hatukuwa na msimamo kuhusu Corona wakati hadi sasa havai barakoa? Au ananiogopa?
Kwani wewe unajua msimamo wetu ulikuwa ni upi ?!. Naona kama unalo jibu mfukoni [emoji102]

Odhis *
 
Kwenye suala la Corona lazima tukubali Magufuli alichemka big time.

Hakuna mtu mwenye akili timamu angekubaliana na Magufuli kwa jinsi alivyoishughulikia korona.

Huwezi kuwa dogma ukajifanya Tanzania haina korona wakati Dunia nzima ina korona eti mungu ametusaidia, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia korona isimuue?

Nakubaliana na mama, shughulika na korona kitaalam.
Nchi ipi imelishughulikia suala la covid kwa ufanisi?
 
Wewe usiye mshabiki umewahi fanya nini kwenye ulimwengu wa medicine? Eti unahoji Vaccine wakati hauhoji ARV au Chanjo ya Yellow fever lazima tushangae.

Afu unahoji kwa paper sio kelele.... Njoo na paper uipresent WHO pale kwamba vaccine hazijakidhi standards yaani maprofessor wote wa Epidemiology wa WHO hawajui hilo ila ww tu msomi wa Sociology ndio unalifahamu hilo.

Tuacheni kelele tutengeneze za kwetu... Mbona AU imeomba patent ili tutengeneze wenyewe. Badala mshikilie hilo bango mnaanza kejeli tu wakati kesho tena mnasubiri ARVs zitolewe huko huko kuja kuwatibu!!

Mnayo TFDA ina maana hamuwaamini kupima ubora wa hizo chanjo? Mbona mnatuaibisha.... Mara cjui barakoa za nje zina COVID utadhani hatuna TBS/TFDA kuhakiki hilo!! So funny
Bahati mbaya mie nimesoma vet medicine. So sio kwamba sijui nachoongea.

Kujifanya msomi na mjuaji sana mbele za watu, haitakusaidia sana.
 
Nani kapoteza ndugu sababu ya chanjo?? Watu 20 kati ya million 17 waliodungwa AstraZeneca? Ama watu gani

Swali naomba nikuulize kuna dawa gani ambayo haina side effects!! Hvi unajua madhara ya Insulin au ARVs? Mbona hatupigi marufuku.

Ama madhara ya CT scan/chemotherapy na radiotherapy? Au hizo hujui zina side effects na fatality rate kubwa kuliko AstraZeneca??

Naomba uje na data sio kelele
Mkuu kwan kati ya malaria na covid ipi ni hatari kwetu sisi afrika??

Ningekuona mfuatiliaji mzuri kama ungeanza kuona magonjwa yapi yanapaswa kupewa kipaumbele kwanza.

Wazungu wao covid imekuwa ni hatari sana k.v mafua kuliko sisi.

Sisi malaria imekuwa ni hatari sana kuliko wao.haina maana waafrika hawafi kwa covid, hapana wanakufa kwa uchache sana. Lakini malaria inaua sana.
Wazungu pia wapo wanaokufa kwa malaria. Japo ni wachache mno.

Hapa sasa tulipswa sisi tudeal na magonjwa ambayo hatari sana kwetu.
Na wao wadeal na magonjwa hatari kwao.

Ni sawa leo hii sisi tuanze kupambana na mafua makali kwa kuwa yanaua wazungu.
Hapana.
Corona ipo, ila athari zake afrika ni kidogo kuliko magonjwa mengine
 
Wasalaam wana jamvi!

Nimeshangazwa sana na Mh Rais kusema ataunda kamati kuhusu swala la Corona ili baadae tuwe na msimamo kuhusu Corona!

Mimi kwenye hili nimejiuliza maswali hivi ni kweli Tanzania hatukuwa na msimamo kuhusu Corona? Huyu Rais si alikuwa Makamu wa Rais na Rais wake alishasema wazi kuwa Tanzania hakuna Corona na kama ipo ni ndogo sana?

Hii kamati anayounda anataka imwambie nini kipya asichokijua? Anataka aanze kutoa takwimu za Corona sasa anataka kamati imshauri?

Anataka aweke watu Lockdown sasa anataka kamati imshauri?

Anataka kulazimisha watu kuvaa barakoa sasa anataka kama imshauri?

Anataka kupokea chanjo ya Astrazeneca sasa anataka kamati imshauri?

Rais anaogopa nini kusema alikuwa hakubaliani na jinsi mtangulizi wake alivyo kuwa anaikabili Corona? Rais anaogopa nini kusema wamejiandaa kupokea chanjo ya AstraZeneca hivi karibuni?

Sidhani kama Rais anatakiwa kujificha nyuma ya kamati kwenye swala kama hili ambalo liko wazi!

Kuna kitu gani hajui ambacho anataka kamati imwambie?

Kwanini anajificha nyuma ya kamati anashindwa nini kuwambia watanzania wajiandae kudungwa Astrazeneca?

Kama Tanzania hatuna msimamo kwanini yeye havai barakoa? Hajui huo nao ni msimamo? Anataka ashauriwe nini?

Kwanini Tusiamini ana ajenda zake mkononi anataka azipitishe nyuma ya kamati ili watanzania waamini ni msimamo wa kamati kumbe ni msimamo wake?

Wasalaam!
We malaya tuko kwenye uchambuzi wa ripoti ya CAG tunaangalia jinsi bwana wako mwenda zake alivyokuwa fisadi. Hizo chanjo zije tu tutachanjwa, kama hutaki hulazimishwi. Upo hapo bibie?
 
Work group yangu tupo 6.... Wameuguwa Covid 19 watu watatu.

Mzee wangu aliwekwa ICU

Hapo sijasema kanisani kwetu tumezika wangapi kwa Covid.... Hyo ni mimi tu ssa jiulize kwa watu million 10 tu sample ikoje.

Hzi data ni za mwaka huu tu.
Hao watatu hawajawahi kuumwa magonjwa mengine tofauti na Covid-19?

Mzee wako hajawahi kuumwa ugonjwa mwingine?

unafahamu kwa siku ni watu wangapi wanakufa kwa ajali za Barabarani?
 
Tatizo lake ni kubwa sana hii korona sio ajenda kwakweli angeachana nayo tu
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
 
Kenya wanaofuata COVID19 protocols wako wapi?
Je hamsikii hosptali na mfumo wa afya ulivyozidiwa?
Mbona bongo tunaishi na vizuri tu na maisha yanaendelea kama kawaida?
Tunataka maisha gani zaidi?
Maisha yanaendelea kama kawaida na tumepoteza kiongozi wa juu kabisa wa nchi kwa corona? Achilia mbali hao wa chini yake ambao kea pale ikulu tu ni zaidi ya wanna.
Hebu taja nchi nyingine imepoteza viongozi wa juu kama sisi ndani ya mwaka mmoja.
 
Tatizo lake ni kubwa sana hii korona sio ajenda kwakweli angeachana nayo tu
SSH ni kipaza sauti tu, chochote mabeberu watakachosema atakuja kuropoka tu. Tutegemee masharti ya kijinga kwa jina la kuzuia Corona ili kuwafurahisha mabwana zake.
 
Exposure gani ya kukufunga akili namna hiyo? umeshajiliza kwanini wanaozalisha hizo chanjo wana 'patent' na hawataki ku share uvumbuzi wao kuokoa dunia? Countries obstructing COVID-19 patent waiver must allow negotiations | MSF
Kwani umekatazwa kutengeneza ya kwako? Hvi kwanini ssi ni watu wa kulalamika.... Mnadai ni biashara ya watu mbona China wanatengeneza huko na Russia pia? Si na sisi tutengeneze sasa ili tuuze tupate pesa? Tunalia lia bila counter measures hatutofika popote.
 
Kwenye suala la Corona lazima tukubali Magufuli alichemka big time.

Hakuna mtu mwenye akili timamu angekubaliana na Magufuli kwa jinsi alivyoishughulikia korona.

Huwezi kuwa dogma ukajifanya Tanzania haina korona wakati Dunia nzima ina korona eti mungu ametusaidia, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia korona isimuue?

Nakubaliana na mama, shughulika na korona kitaalam.
Wewe una corona?
Ni utaalam upi huo wa kuishughulikia corona ilhali mataifa mengine yenye utaalam na wataalam wameshindwa?

Acheni uzwazwa....corona ipo na haina dawa so itaendelea kuwepo.
 
Hao watatu hawajawahi kuumwa magonjwa mengine tofauti na Covid-19?

Mzee wako hajawahi kuumwa ugonjwa mwingine?

unafahamu kwa siku ni watu wangapi wanakufa kwa ajali za Barabarani?
Na ww nikuulize hao million waliokufa kwa Covid hawakuwahi kuugua magonjwa mengine ama nchi zao hazijawahi poteza watu wengi kwa magonjwa mengine?

Huwezi justify watu kuugua Covid 19 eti sababu tu wanauguaga magonjwa mengine.

Mzee wangu hakuwahi lazwa ICU licha ya umri mkubwa Ila kwa mara ya kwanza Covid ilimlaza.
 
Wewe una corona?
Ni utaalam upi huo wa kuishughulikia corona ilhali mataifa mengine yenye utaalam na wataalam wameshindwa?

Acheni uzwazwa....corona ipo na haina dawa so itaendelea kuwepo.
New Zealand waliweza kwenye first wave na Taiwan pia ama husomi habari.
 
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
Yaani Mama Samia hotuba yake ya juzi tu ilinifanya niione Tanzania ikirudi 2005 hadi 2015.
Unasemaje kwakuanza ukusanyaji kodi wa kutumia akili kuliko nguvu nchi itayumba kidogo?
Halafu unasema mbele za watu ambao wataitumia hiyo kauli kama njia ya kula rushwa na kuhujumu mapato kwakuwa tu Rais keahasema tutayumba kidogo.

Suala la bando lilikuwa ni suala la kutoa kauli moja tu mambo yarudi kama yalivyokuwa. Unawaambia watu wakaangalie la kufanya na tatizo lisijirudie tena ilhali halijaondoka.

Yaani hii nchi italiwa mpaka basi.
 
Back
Top Bottom