Kwanini Rais amepoteza mvuto kabla ya kutimiza siku 100?

Nchi Nzima mwanaume alikua ni yeye tu, akisema kitu kinakua, nchi ilikua na adabu, nchi ilikua inaenda kunakostahili, dunia nzima ilitamani uongozi wake, hakuyumbishwa wala kuogopa chochote, roho inaniuma sana Jaman , Ina maana watu haya yote hawayakuona kutoka kwa magu kweli??
 
Magu alikua jembe bwana, akisema leo watu wote hakuna kuvaa nguo utaona jiji zima liko uchi[emoji23], c mtoto sio mzee, Mungu amuweke panapostahili, baba wa watu kazi aliifanya kwa kweli
Kwa udikiteta ule ulitaka wafanyeje?
Watanzania ni watu waungwana,walichagua kuwa wapole lakini mioyoni walikuwa wanabubujika machozi kwa huzuni!
 
Hii shida iko kwa wale waimba nyimbo wa Jiwe. Mama aliposema yeye na jiwe ni kitu kimoja walishangilia sana, sasa anawaonyesha kwa vitendo kuwa yeye siyo.

Awe kama jiwe aringe? Usitufananishie jiwe wetu na utopolo mxieew toka ukome
 
Kiongozi hafokei watu mbele ya makamera, ni ushmba, anaotoa maagizo, maagizo yasiopofanyika anachukua hatua kama kuondoa hao wazembe n.k, ndio nchi zilizostaarabika zinaenda hivyo. viongozi wanaingia na kuongoza mtaifa makubwa na kuyapaisha kiuchumi huwaoni wakifokea watu hovyo hadharani

Samia kwenda Uganda alienda kusaini mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta, asingetakiwa kwenda? Magufuli baada tu ya kupata Urais hakwenda Rwanda? Samia kaenda Kenya tayari mahindi ya TZ yaliyokuwa yamekwama mpakani yameruhusiwa, ulitka akajifungie kama mzee wa chato?

Kuweka sheria nzuri kwa ajili ya uwekezaji kuna shida gani? unajua hata faida za uwekezaji au ndio jiwe kawakaririsha tu kuwa hawafai?
 
Magu alikua jembe bwana, akisema leo watu wote hakuna kuvaa nguo utaona jiji zima liko uchi[emoji23], c mtoto sio mzee, Mungu amuweke panapostahili, baba wa watu kazi aliifanya kwa kweli
Labda jiji hilo ni lile la kusadikika
 
Unaumwa na kichaa!

Na kazi iendelee!

Chato gang members tafuteni kazi za kufanya nyingine ...

Mlitaka apayuke ovyo na kuonekana kila siku kwenye mativii na matamko ya kipuuzi puuzi kama baba yenu marehem?
Mataga ndani ya siku hizo hizo 100 zikifika utawasikia tena ,hawa ni zao la kipindi cha (wenye akili wanyamazapo wapumbavu uongezeka ) kina musiba hao
 
Watu wa CCM mmepoteza dira sasa mnasema amepoteza mvuto, poleni sana watu mliozoea kufokewa na kuitwa Wanyonge. Rais wetu Samia ni Mama. Toka lini mama akapoteza mvuto kwa watoto wake.

Sent from my vivo 1915 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ni kazi ya ccm tumechoka.
 
Kinachomuangusha ni kutoa maagizo ambayo hayatekelezwi. Alianza na vifurushi vya simu akafeli, wizara ya fedha hailipi kwa wakati kama walivyoagizwa, bot hatujasikia kitu....
 
Ukiona mama amepoteza mvuto ujue umeanza kuachwa mbali sana ongeza spidi otherwise utakuwa mnyonge mpaka ufe na kizazi chako kitakulaumu sana.

Nchi imefunguliwa, fursa zinaletwa, wewe umebaki kuwaza vicoba shauri yako. Tafuta fursa, mabenki yameanza kukopesha upya sasa, miradi inaanza kurudi, private sector imeanza kurudishwa kwenye uchumi na inarudisha confidence kwa wawekezaji na financiers wewe unabaki kuangalia tu unavyoachwa.

Mlizoea kila kitu kifanywe na serikali,. Wadau wa uchumi wa nchi wapo wengi sana Ila kuna Shana iliyojengeka tu kwamba uchumi unaendeshwa na serikali hapo ndipo tulipokaribisha umasikini unaotucost sana mpaka mmeamua kuridhika na jina la wanyonge.

Amka changamkia fursa la sivyo utaachwa kweli na utapotea kwenye ramani.
 
Ngoja nibebe mzingo wa kumpigania rais wangu kila baya mtakalosema naligeuza nzuri hata kama linaniumiza hata mfanyaje kwa sasa ndio mke aliyechaguliwa na baba yetu (Tanzania) atulee hivyo ukubali usikubali ndo mama aliyekuwepo hivyo mwacheni apige kazi.
by the way siku mia kitu gani wewe unakumbuka siku mia za kuzaliwa kwako ulifanya nini?
au kila baada ya siku mia unaweza kutupa mabadiliko yako?
hata hivyo saa ni kwa wazungu zaidi ndo maana hakuna kiwanda cha saa afrika ila kulikuwa na mafundi saa ambazo zilikuwa zinaharibika kwa kuwa waafrika hawajui kuzitumia na baada ya waafrika kuacha kuvaa saa mafundi saa wengi wamekuwa mafundi simu kwa kuwa tatizo ni lilelile lililokuwa kwenye saa.
mpeni muda tafadhari na tufikirie ni kwa kiasi gani tunaweza kumsaidia na sio kumwangamiza hii nafasi sio ndogo inawapotoshaji wengi kuliko waongoza njia.
 
Amepoteza mvuto kwa wasiojulikana,sukuma gang na chatorism empire.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…