Kwanini Rais Magufuli alimfunga Kabendera?

Kwanini Rais Magufuli alimfunga Kabendera?

uko sahihi kabisa. Kuna mambo mengi magufuli alikosea. Na kuna mazuri pia alifanya. Kipindi anaingia madarakan nchi ilikuwa na hali mbaya zaid. Kuna baadhi ya vitu alifanya ambavyo hata ingekuwa wewe ndo uko madarakani kwa wakati ule ungefanya kama yeye alivofanya. Kwa mtawala kuua watu ambao wako kinyume nae ilikuwepo tangu zamani.

Labda utakubaliana na mimi kuwa wakosoaji wengi wamejikita kubainisha mabaya ya magufuli na kumchora vibaya kwa jamii iliyokuwa ikimuona kama kiongozi bora. Jiulize nia yao ni nini hasa?
dawa iliyopo nikuwaletea jiwe lingine zaidi ya Magu..miaka ya usoni
 
Ndugu wanajamvi,

Tumesikia kuhusu kitabu kipya cha Erick Kabendera kinachoitwa "The Name of the President: The Memoir of a Jailed Journalist". Kabendera amefunguka kwa kina juu ya utawala wa Magufuli na madai ya udikteta. Hii inatufanya tujiulize maswali mengi kuhusu sababu halisi za kufungwa kwake.

Ni wazi kuwa Kabendera alikuwa mwandishi wa habari shupavu, lakini je, hatua za kumkamata na kumfungia zilikuwa za haki? Au zilikuwa juhudi za kumnyamazisha kwa sababu ya uandishi wake?

Kwa vile tunafahamu kwamba baadhi ya wanachama wetu hapa ni wafanyakazi wa idara za usalama, jeshi, na ulinzi, tunapenda kupata mitazamo yenu juu ya suala hili:

1. Je, ni nini hasa kilichosababisha Kabendera kuonekana tishio kwa utawala wa Magufuli?

2. Kuna ukweli wowote katika madai kuwa utawala huo ulitumia nguvu za dola kuzima uhuru wa vyombo vya habari?

3. Kwa maoni yenu, je, kufungwa kwa Kabendera kulikuwa na athari gani kwa tasnia ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania?

4. Kwa nini utawala wa Magufuli ulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya waandishi wa habari huru kama Kabendera?

Tunaomba mjadala huu uwe wa kistaarabu, wa kina, na wa kuheshimu maoni tofauti. Ikiwezekana, tusaidiane kupata ukweli ili kuangazia mustakabali wa uhuru wa vyombo vya habari nchini mwetu.

Karibuni!

View attachment 3191541
In the name of the president siyo The name of the president, unapotosha maana ya uandishi,

In the name means something or someone is representing another
 
Tanzania ni nchi maskini bado.

This is how it works kuna kinaitwa DeMPA👇

Kuna taratibu zake kabla nchi maskini ujaenda kuchukua mikopo kwenye private banks.

Kwa sababu nyingi, default risks na cash flow yako. Kabla private banks awaja kukopa wanataka kuona income yako na against current current liability.

Na world bank nao wana monitor, bank itakayopa nchi yenye B rating bila ya kuongea na IMF au WB inanunua ugomvi mkubwa wa irresponsible lending kwa kuchezea amana za wateja wao. Waulize Credit Suisse fines walizochezea EU kwa kuikopa Mozambique bila kufuata DeMPA.

Unadhani unakopeshwa tu na private banks, muulize Mwigulu si alienda kutafuta mkopo NY through private banks (Paris Club), huo mkopo alipata.

Hadi ukoposhwe na banks nchi ya third na IMF/WB wakae kimya maana yake cash flow yako ipo vizuri.

Tatizo lenu tunajazana upepo kwenye story zetu sana humu JF na kudhani, that’s how things work.

Magufuli hakuwa wa mzaha-mzaha

Nimeongelea Exim kwa sababu ni bank ya China na kama ujuavyo, China hainglii sovereignty ya nchi. Hata ufanye nini, wao wanachoangalia ni uwezekano wa kulipa na collateral, kilichowakuta Zambia hadi kuweka uwanja wa ndege rehani nadhani unaujua

Kwa hiyo China na mashirika yake ni mbadala wa IMF au WB bank ambao wanaangalia sana Utawala wa Sheria..

Hapo ndipo point zangu zilipo

Kuhusu credit rating, ni mambo ya kawaida na Tanzania ilikuwa katika position nzuri kwenye hizo ratings zao haswa baada ya Kikwete kwa sababu kikubwa kinachoangaliwa ni uwiano wa deni na thamani ya uchumi au pato la taifa la nchi husika.

Hapo ndipo tunapata kujua kama nchi inakopesheka au hapana.

Kwa hiyo mkuu usitake kutengeneza imagine kuwa Tanzania ishawahi kuwa na bad credit rating na Magufuli alikimbilia exim kutokana kutokukopesheka kwetu. Hapanaaaa, alikimbilia huko kwa sababu mfumo wake wa nchi ulikuwa haukopesheki maana kama trilions zilizokosa maelezo kiasi cha Assad kustaafishwa U_ CAG kinyume na sheria. Ni nani angemuamini na Pesa za wahisani

So msihamishe magoli, ongeeni ukweli
 
uko sahihi kabisa. Kuna mambo mengi magufuli alikosea. Na kuna mazuri pia alifanya. Kipindi anaingia madarakan nchi ilikuwa na hali mbaya zaid. Kuna baadhi ya vitu alifanya ambavyo hata ingekuwa wewe ndo uko madarakani kwa wakati ule ungefanya kama yeye alivofanya. Kwa mtawala kuua watu ambao wako kinyume nae ilikuwepo tangu zamani.

Labda utakubaliana na mimi kuwa wakosoaji wengi wamejikita kubainisha mabaya ya magufuli na kumchora vibaya kwa jamii iliyokuwa ikimuona kama kiongozi bora. Jiulize nia yao ni nini hasa?

Mbona unatetea uuaji?
Ben Saanane hakuwa tishio kwa usalama wa nchi ila alihoji PhD yake ya magumashi tu.
 
Ndugu wanajamvi,

Tumesikia kuhusu kitabu kipya cha Erick Kabendera kinachoitwa "The Name of the President: The Memoir of a Jailed Journalist". Kabendera amefunguka kwa kina juu ya utawala wa Magufuli na madai ya udikteta. Hii inatufanya tujiulize maswali mengi kuhusu sababu halisi za kufungwa kwake.

Ni wazi kuwa Kabendera alikuwa mwandishi wa habari shupavu, lakini je, hatua za kumkamata na kumfungia zilikuwa za haki? Au zilikuwa juhudi za kumnyamazisha kwa sababu ya uandishi wake?

Kwa vile tunafahamu kwamba baadhi ya wanachama wetu hapa ni wafanyakazi wa idara za usalama, jeshi, na ulinzi, tunapenda kupata mitazamo yenu juu ya suala hili:

1. Je, ni nini hasa kilichosababisha Kabendera kuonekana tishio kwa utawala wa Magufuli?

2. Kuna ukweli wowote katika madai kuwa utawala huo ulitumia nguvu za dola kuzima uhuru wa vyombo vya habari?

3. Kwa maoni yenu, je, kufungwa kwa Kabendera kulikuwa na athari gani kwa tasnia ya uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza nchini Tanzania?

4. Kwa nini utawala wa Magufuli ulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya waandishi wa habari huru kama Kabendera?

Tunaomba mjadala huu uwe wa kistaarabu, wa kina, na wa kuheshimu maoni tofauti. Ikiwezekana, tusaidiane kupata ukweli ili kuangazia mustakabali wa uhuru wa vyombo vya habari nchini mwetu.

Karibuni!

View attachment 3191541
Uandishi wa Habari una Maadili yake kama zilivyo kazi nyingine, na chochote unachoandika lazima u balance stori na stori hiyo iwe na ukweli.

Na unapokiuka maadili hayo lazima uonywe.
 
Rais John Magufuli, aliyeongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi kifo chake mwaka 2021, alijulikana kwa sera zake kali na mtindo wa uongozi wa nguvu. Miongoni mwa matukio yaliyosababisha mjadala mkubwa ni kukamatwa na kufungwa kwa mwandishi wa habari, Kabendera, mwaka 2019.

Tukio hili lilikuwa na mizizi ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi, na linaweza kueleweka vizuri kwa kuzingatia mazingira ya wakati huo.

Sababu za Kisiasa

Moja ya sababu kubwa za kukamatwa kwa Kabendera ilikuwa ni kazi yake ya uandishi wa habari. Kabendera alikuwa mwandishi aliyekosolewa sana, akijulikana kwa kuandika makala za uchambuzi kuhusu siasa za Tanzania, hasa katika kipindi ambacho Rais Magufuli alikuwa akifanya mabadiliko makubwa katika nchi. Magufuli alijitambulisha kama kiongozi ambaye alitaka kudhibiti habari na maoni yanayochapishwa, akihofia kwamba yanaweza kuathiri sifa yake na serikali yake.

Udhibiti wa Vyombo vya Habari

Katika kipindi cha utawala wa Magufuli, kulikuwa na sera kali za kudhibiti vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza. Rais alipitisha sheria kadhaa ambazo zililenga kuimarisha udhibiti wa habari, na hii ilikuwa na athari kubwa kwa wanahabari na waandishi wa habari. Kabendera, ambaye alijulikana kwa uandishi wake wa uhakika na ushirikiano na vyombo vya kimataifa, alikabiliwa na hatari ya kukamatwa kutokana na maudhui ya kazi yake.

Kukamatwa kwa Kabendera

Kabendera alikamatwa mnamo Julai 29, 2019, na alishtakiwa kwa makosa kadhaa, ikiwa ni pamoja na uhamiaji haramu na utumiaji wa nyaraka za uongo. Hata hivyo, wengi waliamini kuwa mashtaka hayo yalikuwa na lengo la kumdhibiti kutokana na kazi yake ya uandishi wa habari. Kiongozi wa serikali alikiri waziwazi kuwa Kabendera alikuwa anashughulika na masuala ambayo hayakupaswa kuandikwa, na hivyo kumfanya kuwa kiongozi wa waandishi wa habari wanaopigania uhuru wa kujieleza.

Athari kwa Jamii

Kukamatwa kwa Kabendera kulizua mzozo mkubwa katika jamii. Wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari, na wananchi wengi walijitokeza kupinga kitendo hicho, wakisema kwamba ni hatua ya kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Hali hii ilichochea mjadala kuhusu umuhimu wa uhuru wa habari katika demokrasia ya Tanzania. Wengi waliona kwamba kukamatwa kwa Kabendera ni mfano wa jinsi serikali ilivyokuwa ikitumia nguvu dhidi ya wanahabari na wapinzani wa kisiasa.

Mchakato wa Kisheria

Baada ya kukamatwa kwake, Kabendera alikabiliwa na mchakato mrefu wa kisheria. Alifungwa kwa muda mrefu kabla ya kupewa dhamana, na wakati wa mchakato huo, alikabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo hali mbaya ya kifungo na ukosefu wa mawasiliano na familia yake. Hali hii ilionyesha jinsi mchakato wa kisheria unaweza kuwa na athari mbaya kwa wanahabari, na ikaleta hofu miongoni mwa waandishi wa habari wengine nchini.

Hitimisho

Kukamatwa kwa Kabendera ilikuwa ni tukio ambalo liliweka wazi changamoto zinazowakabili wanahabari nchini Tanzania. Rais Magufuli alitumia mbinu za kudhibiti vyombo vya habari ili kulinda sifa yake na serikali yake, lakini hatua hizi zilisababisha hasira na upinzani kutoka kwa jamii.

Tukio hili linaweza kuwa ni alama ya mapambano ya kudai uhuru wa habari na haki za binadamu, na linaendelea kuwa mfano wa umuhimu wa uhuru wa kujieleza katika jamii za kisasa.

Katika mazingira ya kisiasa yenye changamoto, ni wazi kwamba uhuru wa habari ni nguzo muhimu katika kuhakikisha demokrasia na uwazi wa serikali.
 
Nimeongelea Exim kwa sababu ni bank ya China na kama ujuavyo, China hainglii sovereignty ya nchi. Hata ufanye nini, wao wanachoangalia ni uwezekano wa kulipa na collateral, kilichowakuta Zambia hadi kuweka uwanja wa ndege rehani nadhani unaujua

Kwa hiyo China na mashirika yake ni mbadala wa IMF au WB bank ambao wanaangalia sana Utawala wa Sheria..

Hapo ndipo point zangu zilipo

Kuhusu credit rating, ni mambo ya kawaida na Tanzania ilikuwa katika position nzuri kwenye hizo ratings zao haswa baada ya Kikwete kwa sababu kikubwa kinachoangaliwa ni uwiano wa deni na thamani ya uchumi au pato la taifa la nchi husika.

Hapo ndipo tunapata kujua kama nchi inakopesheka au hapana.

Kwa hiyo mkuu usitake kutengeneza imagine kuwa Tanzania ishawahi kuwa na bad credit rating na Magufuli alikimbilia exim kutokana kutokukopesheka kwetu. Hapanaaaa, alikimbilia huko kwa sababu mfumo wake wa nchi ulikuwa haukopesheki maana kama trilions zilizokosa maelezo kiasi cha Assad kustaafishwa U_ CAG kinyume na sheria. Ni nani angemuamini na Pesa za wahisani

So msihamishe magoli, ongeeni ukweli
Aargh

Don’t have time for this, soma kwanza public debt.
 
Kabendera alikuwa anatumika na watu wa nje kumhujumu Magufuli alitaka kupindua utawala wa Magu.
Mwandishi wa habari unaandika artcles 4 kwa mwezi kwenye akaunt yako unalipwa million 300. Unachomoa pesa unazitawanya kwa wakosoaji wa serikali mitandaoni. Hiyo investigative journalism kilikuwa kichaka cha money laundering alikuwa anatumika kwa kazi maalum kazi chafu.
Tuwasikilize na wengine ndani ya kaya wanasemaje?
 
Ina maana walengwa(watumiaji) wa kitabu chake ni jamii gani? Watanzania au? Au hajui kiswahili? Kabendera ni mtanzania kweli?
Unapo andika kitabu inatakiwa ujue watakao kisoma kitabu chako, (the audience), Mimi naandika kitabu mama Cha ujasiriamali kwa kimombo Bado sijakizindua natafsiri kwa kiswahili, nitazindua kwa lugha mbili,

Lazima ujue aina ya wasomaji wa kitabu chako, mimi naandika kitabu ambacho unakisoma unakiweka kwapani na kufanya biashara
 
Back
Top Bottom