Kwanini Rais mstaafu Kikwete hakupewa nafasi ya kuongea katika uzinduzi wa Kavazi la Dkt. Salim?


siyo kweli, mtoto wa mjini ni aliyezaliwa na kukulia mjini wengine wote wanaojiita watoto wa mjini huku wamezaliwa na kukulia vijijini ni wannabees…
 


Ili aanze kuzunguka mbuyu wakati watu wanajua aliyesema Dr. Salim sio mtanzania na hizbu ni nani? Mwalimu Nyerere, Mwenyezi Mungu ampe pumziko la amani. Hakuwa ana bahatisha.
Kati ya "Lulu" njema za Tanzania, ambazo alizilinda kwa maarifa na nguvu zake zote ni Dr. Salimu. Wakati ule Dr. Salimu alipokuwa kijana, kama angeachwa akae kule na wale wana mapinduzi, sidhani kama angefika alipofika.
Huyu ni mzalendo wa kweli. Ni Mtanzania haswa. Na anastahili kupewa nafasi yake sababu ya matendo yake. Sio ujanja ujanja, rushwa na maadili mabovu ya uongozi ambayo wengine wengi wanafikiri wanapoyafanya, watanzania hawayaoni.
Ipo siku kila mtu atavuna anayopanda. Kwangu mimi, Salute Dr. Salim Ahmed salim kwa yote uliyoitendea ardhi yetu ya Tanzania.
Mwenye macho haambiwi ona...na mwenye masikio haambiwi sikia...muda utaendelea kutenga pumba na mchele.
 
Alishiriki kumfanyia fitina kuteuliwa kuwa rais wa Jamhuri ya muungano, 2004/2005! Walimpa majina yote mabaya,hizbu, nk,
Hii nchi Ina bahati mbaya Sana, watu Bora huwa hawapati nafasi ya kuwa viongozi wakubwa,
Samia hafai hata kuongoza wilaya, Leo ni Rais!
Biteko na PhD yake ya kuunga Leo, ni deputy PM, hv kwa akili nzuri kabisa, unamchagua vipi biteko, unamuacha vipi Antony Mtaka? Biteko kawekwa pale ili sukuma voting block, ivutiwe, nothing else,
Ma CCM yanachojari ni kukaa madarakani tu.
 
Ha ha ha! Unadhani anamafanikio gani kunishinda? Au unadhani wote tulio humu jamii forum ni waganga njaa. Tuliza akili jamii forum ni watu wa kila aina, kiuchumi, kisiasa, na kijamii. Hujui ukoo wangu wala hunijui.
 
Umesababisha nimuonee huruma Dr Salim
 
..kama dr. Salim angelikua rais kuanzia mwaka ule mkwere amekua rais (2005)..leo ingekua kama singapore......walimfanyia fitma kubwa salim....kwa kumuita si mtanzania...mara mwarabu....waswahili bana....leo tuko hapa ndio wanajifanya kumuenzi Salim...walikua wapi miaka hiyo?..unafiki tu...
 
Protocol ya kawaida sana
Nadhani asingekuwa na la kusema zaidi ya kumuomba radhi Salim kwa maneno ya hovyo waliombaka kupitia wantandao wakiongozwa na kichwa cheupe, kwa ahadi ya kuachiwa kijiti baada ya mbio kumalizika.
Wakati fulani ni bora sana kunyamaza ili yaliyotokea yasikumbukwe.
 
Cha ajabu kichwa cheupe hakuachiwa huo Urais
 
Nilijua huwezi tia neno sababu maslahi kugongana

Ni wazi usio na shaka kundi la mtandao walimchafua Sana DR SALIM
Hata ndugu yetu Zitto aligusia jinsi Salim alivyochafuliwa lakini hakwenda mbali kuogopa kumgusa godfather wake!

Ingekuwa aliyemchafua ni labda JPM sasa, zingeandikwa makala za kila aina wakiwemo rafiki zake waandishi.
 
Watoto wadogo hawawezi kukuelewa master

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Waliomkataa Dr SAS ni Wazanzibar ndani ya NEC kwa tuhuma ni Hizbu

JK na mtandao wana shea yao. Siri ambazo TISS Wamekataa isiwekwe wazi ni hii, ili kumsitiri Jakaya na kundi lake

JokaKuu Pascal Mayalla

..alianza Mzee Mwinyi mwaka 1995.

..Maalim Seif na Salim Salim walimtonya Mzee Mwinyi kwamba akipendekezwa akatae na kubakia Raisi wa Zanzibar, ili njia iwe nyeupe kwa Salim Salim.

..Kufika kwenye kikao Mzee Mwinyi akawageuka wenzake, na kilichobaki sasa ni historia.
 
Kikwete na Salimu walijengeana bifu uchaguzi mkuu 2005 kambi ya Kikwete ikidai Salimu alikuwa Mwarabu akiwa na ndugu Majenerali huko Uarabuni ambao angeweza kuwatumia usalama wa Tanzania kupitia Zanzibar. Kampeni hiyo mbaya iliongozwa na RA na Mhariri mmoja wa gazeti moja la weekly hapa nchini aliyekuja kuteiliwa Msemaji wa Ikulu. Kama ILIKUWA hivyo kwa Salim, mbona JK hajarudia Hilo kwa SSH ambaye Ana wajomba na ndugu tele huko?

Kweli siasa Ni mchezo mchafu, unaotesa Wananchi na nchi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…