Kwanini Rais Samia akienda kijijni kwao anafikia hotelini?

Kwanini Rais Samia akienda kijijni kwao anafikia hotelini?

Mh. Rais wetu tokea juzi yupo kwao Kizimkazi, kanishangaza badala ya kufikia nyumbani kwake au kwao yeye kafikia hotelini! Anatoka hotelini na msafara anaenda kwao.

Je, kwao hajajenga nyumba ya makazi au wazazi wake hawana makazi mpaka yeye alale hotelini, kilomita 7 kutoka kijijini kwao au ndiyo anatumia tozo zetu?!
Husband hayuko huko home
 
Mkuu yeye kalala hotelini tena karibu na kwao alipo zaliwa asubuhi anatoka hoteli anaenda nyumbani kwao hii imekaaje,, mbona Ma Raisi wote waliopita wakienda kwao wanafikia nyumbani kwao mfano Nyerere Butiama kwake kabisa na nyumba yake ilikuwa ya kawaida sana, Kikwete alikuwa akienda kijijini kwao Msoga alikuwa afikii hotelini anafikia kwake, Magufuli tulikuwa tunamuona Chato yupo kwake, nimeshangaa Mama yeye inamaana tokea awe mbunge mpaka makamu wa Raisi na sasa Raisi ina maana haja jenga nyumba nzuri ya yeye kufikia.?
Ndiyo, yeye bado hajajenga, kila Rais na maamuzi yake.
 
Ukiwa Rais palepale unageuka mali ya umma.Halafu,kwa ujenzi wetu huu wa kiaina,ulinzi utakuwa mgumu kufanyika.Idadi ya watu anaoambatana nao ni wengi.Hiyo nyumba itamudu?Kuanzia vyumba,vitanda,sebule kubwa,maliwato na faragha za watakaowakuta.Mengine tuyavumilie tu.Ile ni taasisi.Sasa taasisi ikihamia kwako si itakuwa vurumai?
Waliomtangulia walimuduje??
 
Mh. Rais wetu tokea juzi yupo kwao Kizimkazi, kanishangaza badala ya kufikia nyumbani kwake au kwao yeye kafikia hotelini! Anatoka hotelini na msafara anaenda kwao.

Je, kwao hajajenga nyumba ya makazi au wazazi wake hawana makazi mpaka yeye alale hotelini, kilomita 7 kutoka kijijini kwao au ndiyo anatumia tozo zetu?!
Anamalizia Kwanza Hekalu lake la Mbweni ( ambapo na Hayati we tarehe 17 Machi, 2021 wanapakana ) baada ya Kuwanunua ( Kuwavua ) waliokuwa Jirani nae kisha Ujenzi wa Hekalu lake la huko Kwao Kizimkazi utaanza bila kusahau na lile Hekalu lake jingine ( la Kikatiba ) atakalojengewa na Serikali huko huko Kwao Zanzibar akistaafu ( akimaliza rasmi ) Urais wake mwaka 2030.
 
BWM alikuwa hapati Lupaso na alipachukia sana na akiwachukia watu wa Lupaso ndiyo akupenda kuishi Lupaso kutokana na sababu ya kihistoria ya wazazi wake walivyo fanyiwa.
BWM ametuachia umaskini yaani vumbi mpk barazani ,,hakuwa mtu wa kawaida yule
 
Waliomtangulia walimuduje??
Kutakuwa na sababu maalum.
-ukubwa wa nyumba na eneo husika kutosha.
-hali ya ulinzi kufanyika kwa usalama.
-kutoingilia faragha za mtakaowakuta hapo nyumbani na eneo linalozunguka mtaa.
-miundombinu kupitika kwa urahisi na hata kwa dharula na spidi.(magari au helikopta).Usalama wa Rais na shughuli zake ni first "priorities"!
-kuna kipindi(kwa kupanga au dharula)Rais atatakiwa akutane na "delegetions" za hata nje ya nchi.Panatosha?
NB:Kwa mwalimu Nyerere nyumba ipo sehemu secured ingawa ni ndani kidogo na mji kwa wakati ule.Ulinzi,faragha na utulivu viliwezekana.
Vivyo hivyo Chato kwa Magufuli pamejengwa kwenye eneo kubwa.Sasa,Zanzibar ukitaka uchukue "mahekari" mengi ili ujenge tu makazi ya kawaida utaharibu kama mipangomiji haikuelekeza.
 
Mbona kawawekea lami,wenyewe mmeshindwa kujiendeleza Kwa kumtegemea che nkapa[emoji51]
Mkuu lami kutoka wapi kwenda wapi,,ndani ya mkoa wake wilaya tatu kati ya tano hakuweka lami na maji shida ...yaani ni mbovmbovu tu...ndio maana hakujenga kwao...
 
BWM ametuachia umaskini yaani vumbi mpk barazani ,,hakuwa mtu wa kawaida yule
Watu wa Lupaso mliwaua wazazi wake kwa kuwatuumu wachawi yeye kanisa likamuokoa likamlea na kumsomesha ndiyo maana hakutaka kupasikia wala kuijenga Lupaso na kusini yote aliichukia.
 
Watu wa Lupaso mliwaua wazazi wake kwa kuwatuumu wachawi yeye kanisa likamuokoa likamlea na kumsomesha ndiyo maana hakutaka kupasikia wala kuijenga Lupaso na kusini yote aliichukia.
Ni kweli hii ya wazazi?Basi,nimemsamehe.Kumbe ndiyo maana ...!
 
Kizimkazi kwao Rais Samia
 

Attachments

  • Screenshot_20220904-162605.png
    Screenshot_20220904-162605.png
    106.2 KB · Views: 21
Back
Top Bottom