Kwanini Rais Samia analindwa na mabunduki mengi hivyo?

Kwanini Rais Samia analindwa na mabunduki mengi hivyo?

Kwa nini huyu mama yenu mpendwa analindwa na askari wengi wenye mabunduki kama ilivyokuwa kwa dikteta Magufuli?

Anaogopa nini? Anamwogopa nani?


Ule umagufulification bado upo na utachukua muda kuondoka. Pia wakuu wa vyombo vya ulinzi wanajipendeza kwa Rais kutafuta fadhila za uteuzi katika nafasi za kisiasa.
 
Kagame ni miongoni mwa Marais wenye ulinzi mkali lakini huwezi kuona kazingirwa hovyo kama Hangaya
 
Tukumbusheni kwa mwendazake mlisemaje?
Sikuwahi kuhoji. Nadha raisi yeyote alindwe, sasa namna wata kavyo fanya waamue wao mfano marekani sionagi raisi ana futwa na hayo mabunduki
 
She is a queen .A queen has to be protected by any means necessary
Sikumbuki kuona hivyo kwa mwenye jina hilo halisi, na ni mzee sana pia ukiacha nguvu ya kiutawala aliyonayo ulimwenguni hapa.
 
Kwa nini huyu mama yenu mpendwa analindwa na askari wengi wenye mabunduki kama ilivyokuwa kwa dikteta Magufuli?

Anaogopa nini? Anamwogopa nani?


Anawaogopa CCM wenzake,wamemjaza hofu ajione bila wao hayupo salama.Mojawapo ya strategy ya Chieftain Gang maana wanakula kwa urefu wa kamba zao.
Kuongoza wanafiki kunahitaji nawe uwe bingwa wa unafiki na huko CCM wanafiki sio wa kutafuta,ni ngumu kumpata asiye mnafiki miongoni mwao na ndizo maana waona maigizo tofauti tofauti.
Adui yetu mkubwa sana hapa Tanzania ni Hofu.
 
Sema mimi napenda tu mama anavyolindwa na wanaume vile kwa nguvu..ina nipa feeling fulani amaizing..
 
Tanzania tuko na surplus ya mibunduki & mirisasi kwahiyo tumeamua mungine itumike kumlinda mama wakati akila kwa urefu wa kamba yake
 
Gharama ya kumpoteza rais kizembe Ni kubwa kuliko huo ulinzi alionao mama yetu.by the way ni ulinzi wa kawaida Sana huu
True..

Gharama za kumpoteza Rais kizembe ni ghali sana kuliko hizi za kumlinda in my opinion too.
 
Sikuwahi kuhoji. Nadha raisi yeyote alindwe, sasa namna wata kavyo fanya waamue wao mfano marekani sionagi raisi ana futwa na hayo mabunduki
Sasa Marekani teknolojia yao ya ulinzi utailinganisha na hii ya Tanzania?..

Kuwa serious aisee.
 
Kwa nini huyu mama yenu mpendwa analindwa na askari wengi wenye mabunduki kama ilivyokuwa kwa dikteta Magufuli?

Anaogopa nini? Anamwogopa nani?



Tanzania inazidi kuwa nchi ya “intrigues”. Hasa baada ya mwendazake mambo yanazidi kwenda kimafiosi.

Kiujumla, viongozi by design, wanazidi kuwaogopa wananchi wao. You surely need not ask why.

Halafu kumbuka zile tetesi za awali kuwa kuna “genge” la watu ambalo halikutaka mama akalie hicho kiti hadi intervention ya CDF. Then vile vichokochoko vya “serikali ya mpito” na vineno neno vya “hatagombea 2025”.

Hakuanza na ulinzi modeli hiyo lakini, apparently, watu fursa wakamtonya asifanye ujinga. Siasa is grave business. Ana tishio kila kona hasa huko kwa wavaa kijani wenzake. Ustaarabu wa kikojani hautakiwi kabisa.
 
Back
Top Bottom