Kwanini Rais Samia anatumia ndege za ATCL kwa safari zake hata fupi badala ya ndege ya Rais?

Si ndio hapo,wanaropokwa bila kuwa na evidence,too hopeless.
Unajua maana ya evidence lakini, maana hilo neno haliendani na huu mjadala. Kama kuna kitu unajua sema ili kueleweshana maana bila hivyo wewe ndio mropokaji. Sio kila kitu unachojua wewe na wengine wote lazima wajue. Na hata neno hopeless umelitumia vibaya hapa, hata too.

Kwa hiyo unaona, kila mtu ana sehemu anamzidi mwenzake ujuzi, sasa mimi naweza kukufundisha wewe maana ya evidence na hopeless na wapi pa kutumia neno too, na wewe tuambie unachoelewa kwa nini Samia hakutumia ndege ya Raisi kwenda Malawi. Simple.
 
Kaka pole; Rudia kusoma ripoti ya CAG Kicheere utajua hiyo ndege iliko!
Hiyo ripoti ilisemaje, na kama kuna tatizolililotajwa toka ripoti ya CAG itoke, hilo tatizo linapaswa kurekebishwa kwa muda gani?

Ongea ueleweke, sio kulaumu bila kutoa taarifa. Watu tuna mambo mengi ya kufanya sio lazima tusome ripoti za CAG kama ulivyoisoma wewe.
 
Wananchi wanapenda kulalama.
Hiyo Airbus tumempa mama apigie msele ili kuifungua nchi na ile iliyokuwa ya raisi ndiyo tunaianzishia root mpya ya DAR-CHATO
Kwani Kuna tatizo gani?
Tuwe wazalendo na nchi yetu.
 

Hilo ndilo dege la rais sasa. Air force 1.

Tungoje asimamishe uchumi kwanza.

Hiiiiii bagosha!
 
Mbona enzi za hayati haukuuliza kwann alikuwa anna ruka na A220 kutoka Dodoma mpaka tocha ? Au tokaa Dsm to tocha ?

Au mbona hukuuliza ikikuwa waziri fulani enzi zile alisafiri na B787 kwenda kufuata juice ya madagascar ?
 
Malawi lazima wajua tanzania ipo viwango vya juu katika nyanja ua usafiri wa anga
Malawi wanalo la kujifunza kwamba kila kitu kinawezekana katika sekta ya anga
Pia hapo atcl inatangazwa kiana
 
Ni zile akili ukipata tumia.. chochote mradi mkono uende kichwani fanya. Hata ni kuuza mihadarati sawa 😂😂.
 
Malawi lazima wajua tanzania ipo viwango vya juu katika nyanja ua usafiri wa anga
Malawi wanalo la kujifunza kwamba kila kitu kinawezekana katika sekta ya anga
Pia hapo atcl inatangazwa kiana
Acha posti za vijiweni, Malawi imekuwa ikileta ndege ya abiria ambayo marubani na wahudumu ni wanawake watupu.
 
Na report ya CAG haitakaa izungumzie hasara iliyotengenezwa na ATCL mpaka Bimkubwa akitoka madarakani.

Hizi routes za Dar-Dom nazo anapigia hilo hilo pipa.
Yaani bi mkubwa hilo pipa ndio kageuza motorcade yake. Znz dar dom dom dar znz 😂
 
Ndege za Serikali, ATCL haina ndege hata moja, watu mbona hamuelewi
 
Ile ndege ya rais hayati aliwapa ATCL hakuna ndege ya rais sasa ivi.
 
midege kama imejaa mahirizi na mauchawi ya zee la kule kitovuni nani apande , inawezekana maruhani ya kizanzibari hayapatani na makitu yaliyoachwa kule na mwendazake, tupambane tu jamani maisha magumu na sasa kuna kodi ya kwwenye LUKU sinema inaenda vizuri sana na huo ndio UKWERIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
 

Ndege za Rais Tanzania kuanza kubeba abiria​

Friday January 11 2019​



Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Ijumaa ameongoza Watanzania kupokea ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyotokea Canada na kuagiza ndege mbili kati ya tatu za Rais zianze kupakia abiria.






IN SUMMARY​

Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Ijumaa ameongoza Watanzania kupokea ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyotokea Canada na kuagiza ndege mbili kati ya tatu za Rais zianze kupakia abiria.
Advertisement
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema ndege mbili za rais zinapaswa kuanza kutumika kubeba abiria katika siku ambazo hazitakuwa zikitumika.
Amesema ndege hizo zinatakiwa kupakwa rangi kama za ndege za Serikali zilizokodishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), tayari kwa kuanza safari za kupakia abiria.
Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Januari 11, 2019 wakati wa mapokezi ya ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyowasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Amesema badala ya ndege hizo kukaa bila kutumika ni bora zitumiwe kusafirisha abiria kwenda sehemu mbalimbali ili kuhakikisha wigo wa kukuza utalii unaongezeka.
“Kwa kuwa rais mwenyewe hasafiri hovyo sasa zinakaa kufanya nini na moja ina uwezo wa kubeba watu 50. Hii haitabeba abiria pale tu ambako itakuwa inatumika,” amesema Rais Magufuliu.
Akijibu ombi la Askofu mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible fellowship (FGBF) Zachary Kakobe aliyemuomba kuwa na desturi ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kama ilivyo kwa viongozi wa dini, Magufuli amesema anaogopa kukutana na watu ambao wanatukana na kutishia kumkatakata.
“Huwezi kukutana na mtu anayekuambia akikushika atakukata halafu ukutane naye kumbe ndiyo siku yako ya kuchinjwa hivyo ni bora umuache akae mwenyewe huko,” amesema Rais Magufuli.
 
Zilikuwepo ndege 2, ndege moja Magufuli akifanya kuwa ya abiria na ikabaki nyingine ambayo pia kwa sasa haionekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…