Kwanini Rais Samia asiitake Wizara za Mambo ya Nje na Ndani zihakikishe zinamrejesha aliyekopa Mabilioni?

wakati Raisi hata jina lake ana kigugumizi kumtaja ili apate ushirikiano wa vyombo vya dola ndani na nje na watanzania wa ndani na nje

Ni kweli nchi kama Marekani hawasiti kutoa warrant au wito wa kuhojiwa mtu mkubwa yeyote awe bosi wa TIK TOK, HUWAEI, FACEBOOK, Boss wa Benki au tapeli wa fedha kimataifa n.k Serikali ya Marekani huwa hawaogopi kutangaza jina la mtuhumiwa


Department of Justice (.gov)
www.justice.gov
Cryptocurrency Fraudster Sentenced To 15 Years For Money Laundering ...

8 Jul 2021 — According to court documents, Karlsson ran an investment fraud scheme from 2011 until his arrest in Thailand in June
 
Kwa hio mkuu ulitaka amvimbie mtu anaempa cheque ya Trillion 11 zinazopelekwa kuliwa na wahuni ulitaka anune kabisa? Maana wahuni mate yanawatoka wanazisubiri kwa hamu waanze kuzitafuna hizo Trillion 11 za uwekezaji
Mikipo ambayo inakuja kulipa Pesa ambazo Hili kijamaa lao limechukua, alafu Mtanzania ndio wakulipa
 
Ni kweli nchi kama Marekani wakimtafuate awe bosi wa TIK TOK, HUWAEI, FACEBOOK, Boss wa Benki au tapeli wa fedha kimataifa n.k huwa hawaogopi kutangaza jina la mtuhumiwa
Sasa huyo mwizi ana ukaribu nae unataka ampake kinyesi mkuu yaan yeye rais pia yupo na ukaribu na huyo mwizi, nimekuja kuchukua billion 10 Nani kakuagiza SSH wanaiangalia kweli jamaa ana ukaribu nae walikua pamoja kwenye Royal Tour utagoma kumpa? Kakomba pesa hakuna biashara hakuna nini kasepa huku nyuma bi mdashi anashtuka pesa hazipo anauliza anaambiwa yule Bwana kazichukua anaanza kuwaka na kubwata kwamba wamemuibia nyumbani kwake kumbe alieiba ana ukaribu nae kwanini asimtaje sasa?
 
Kakomba pesa hakuna biashara hakuna nini kasepa huku nyuma bi mdashi anashtuka pesa

Mheshimiwa Rais atoe dokezo kwa taasisi na rasilimali nyingi watu na fedha zilizo chini ya ofisi ya DPP kutoa warranti ya kumsaka awe mtuhumiwa yupo ndani ya nchi au hata nje

MKURUGENZI WA MASHTAKA

Mkurugenzi wa Mashtaka ni mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Mkurugenzi wa Mashtaka ndiye msimamizi mkuu wa Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka, Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Mawakili wa serikali na Waendesha Mashtaka katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Majukumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka yatakuwa ni:

  • (i)Kuamua kushtaki au kutoshtaki kwenye makosa ya jinai;
  • (ii)Kuanzisha, kuendesha na kusimamia mashtaka ya makosa ya jinai katika mahakama zote isipokuwa mahakama za kijeshi;
  • (iii)Kutwaa na kuendelea na mashtaka ya kesi yoyote ya jinai iliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine;
  • (iv)Kufuta mahakamani mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa na mtu au taasisi nyingine katika hatua yoyote kabla hukumu kutolewa;
  • (v)Kutoa maagizo kwa jeshi la polisi au vyombo chunguzi vyoyote kuchunguza taarifa yoyote ya kijinai na kutoa taarifa kwake haraka inavyowezekana;
  • (vi)Kuchukua hatua muhimu kwa jambo lolote lenyetija katika mashtaka ya jinai;
  • (vii)Kutoa miongozo inayohusu uratibu wa upelelezi na uendeshaji mashtaka;
  • (viii)Kuteua na kutenguamamlaka ya waendesha mashtaka wa umma;
  • (ix)Kumshauri waziri mwenye dhamana katika masualaya mashtaka yanayohitaji sera au hatua za kibunge;
  • (x)Kuteuwa maafisa maalum ndani ya taasisi za serikali kusimamia mali zilizozuiliwa au kutaifishwa na mahakama katika mazingira ambayo ni vigumu kuteua wasii;
  • (xi)Kufanya kazi nyingine ambayo zinahusiana na mashtaka ya umma;
  • (xii)Kuwasimamia maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine walioteuliwa au kuajiriwa na ofisi ya taifa ya mashtaka;
  • (xiii)Kusimamia shughuli zote zinazofanywa na maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka;
  • (xiv)Kuita afisa yoyote wa umma kutoa maelezo au taarifa kuhusiana na jambo lolote ambalo linahusu mashtaka ya umma;
  • (xv)Kuandaa na kuwasilishakwa waziri taarifa ya nusu mwaka na nakala kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya taifa ya mashtaka; na
  • (xvi)Kuteua au kuajiri na kuwajibisha maafisa sheria, mawakili wa serikali na watumishi wengine ndani ya ofisi ya taifa ya mashtaka
Source : NPS | Mkurugenzi wa Mashtaka
 
Nchi ngumu hii
Mheshimiwa anaweza akataja alafu haohao waliomletea umbea wakaja tena kusema walikosea na yeye ameshatamka hadharan 😄
 
Mh, mkuu angalia hiyo kauli uliyoikoleza hapo juu, URAIS NI TAASISI. Nakushauri tumia lugha nzuri yenye staha na heshima. Kwa kifupi, jaribu kupunguza munkari na jazba.

Usidanganywe na uhuru wa kujieleza uliopewa kikatiba. Miongoni mwa mapungufu makubwa kwenye katiba ni kukupa uhuru wa kujieleza mkono wa kulia na kukunyang'anya kupitia mkono wa kushoto.

Kwa kifupi hatuna uhuru wa kujieleza!!!!!!!!!!!
 
Haya mambo ya Et Rais ni Taasisi, na hivo Iheshimiwe, ni mambo yanayofanya tuendelee kua waoga .

Anayegombea Urais ni mtu, sio Taasisi, Rais ana Washauri, ambao wanaweza mshauri viaba au vizuri au vizuri lkn akawapuuza.


Hizo Kinga walojiwekea, wameweka Mtu, sio Taasisi, na Rais aanawajibika kwa madhaifu yake na kushindwa kwake, na sio kusingizia Taasisi.


Hamna MANENO mengine yanayoweza chukua nafasi ya Wizi, Rushwa, mambo ya ajabu ajabu yanayofanyika Sasa.


Ni kweli akiwa anaongea anaongea kama vile anaongea na familia yake, kumbe anaongea na Taifa lenye watu Waume na Wanawake zaidi Ya Milion 60 .


Mambo ya ajabu yakifanywa na Rais, aaibiwe kua anafanya mambo ya ajabu Kwa lugha ilonyooka.
 
Ni kweli akiwa anaongea anaongea kama vile anaongea na familia yake
Umesema ?
Mambo ya ajabu yakifanywa na Rais, aaibiwe kua anafanya mambo ya ajabu Kwa lugha ilonyooka.
Ndio kumaanisha kwamba ?
Hamna MANENO mengine yanayoweza chukua nafasi ya Wizi, Rushwa, mambo ya ajabu ajabu yanayofanyika Sasa
Kwa hio hua anaongea na nani pale ?
anaongea na Taifa lenye watu Waume na Wanawake zaidi Ya Milion 60
Sawa mkuu umeeleweka kwa hio wewe sio muoga ?
Haya mambo ya Et Rais ni Taasisi, na hivo Iheshimiwe, ni mambo yanayofanya tuendelee kua waoga
We kwa hio sasa itakuaje ?
Hizo Kinga walojiwekea, wameweka Mtu, sio Taasisi
Hii maana yake nini ?
Rais aanawajibika kwa madhaifu yake na kushindwa kwake, na sio kusingizia Taasisi
Basi sawa mkuu,
 
Mimi nakuomba usiendeshwe na mhemko, hisia, munkari na jazba unapoikosoa TAASISI YA URAIS.

Hujakatazwa kuikosoa na kuishauri ila KUMBUKA ina TARATIBU ZAKE. Mojawapo ni kutumia LUGHA YENYE STAHA. Haimainishi kuwa ukitumia lugha yenye staha utaonekana wewe ni muoga.

Nb 1: URAIS NI TAASISI yenye nguvu kuliko zote ndani ya nchi.

Nb 2 :Kumbuka huna uhuru huo unaouringia bali ni kiini macho tu!!!!!!!!!!!!

Ni ushauri tu unaweza kuuchukua ama kuuacha.
 
Uzi ni mzuri. Upumbavu upo kwenye kumsifia Magufuli
 
Sawa Mkuu!!


Wacha iwe Taasisi yenye Nguvu kuliko zote Ndani na nje lakini yenye Kupigwa na kuibiwa na kuchezewa na kugeuzwa kua shamba la bibi !!.

Wacha iwe Taasisi yenye Nguvu, uku Mtanzania wa chini aliendelea kuumizwa na makodi na matozo ambayo kazi yake ni kwenda kulipia haya mamikipo yanayobebwa ovyo


Wacha iwe Taasisi yenye Nguvu kuliko zote, huku mtoto wa Masikin akiendelea kukaa chini darasani miaka 62 ya uhuru Sasa

Hongera yao sana sana sana ,hakika ni Taasisi yenye Nguvu kuliko zote Ndani na nje !!.
 
Watanzania hawajazoea kujadili vitu vinavyowagusa hapo siku mbili tatu watajadili hili suala halafu wataletewa "connection" watasambaziana wiki mbili nzima story inakuwa imefungwa namna hiyo.
 
Kwani Yusuf Manji hizo mabilioni alikopa lini?

Pili ni sababu gani zilizomfanya awe nje ya Tanzania.? Naomba tuanzie hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…