Kwanini Rais Samia hajawahi kumjulia hali Mzee Lowassa?

Kwanini Rais Samia hajawahi kumjulia hali Mzee Lowassa?

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Mheshimiwa Rais Samia ameonekana mara kadhaa akiwatembelea viongozi wakuu wastaafu mbalimbali majumbani mwao au kukutana nao Ikulu kwa mazungumzo na kubadilishana uzoefu wa masuala kadhaa ya uongozi.

Ila sijawahi kumuona akikutana au akimjulia hali mzee Edward Ngoyai Lowassa(waziri mkuu mstaafu).

Je, ni lini Rais Samia atamjulia hali mzee Lowassa kama anavyofanya kwa viongozi wengine?

Asanteni

=====
UPDATE: Waziri Mkuu, Majaliwa amuwakilisha Rais Samia kumjulia hali Lowassa
 
WEWE UNAISHI NCHI GANI? MBONA RAIS ALISHAENDA MPAKA NYUMBANI KWAKE MWAKA JANA KUMJULIA HALI? KWENYE SIASA ZA CCM , UPINZANI NA TANZANIA HUWEZI KUMWACHA LOWASSA NJE. AWE NYUMBANI, HOSPITALINI AU OFISINI. MUNGU AMPE NAFUU MZEE LOWASSA.
 
Alishaenda kumuona muda mrefu tu.

1654582275118.png
 
Labda Kijana wake Fredi huwa anatoa updates za hali ya Mzee.
 
Mheshimiwa Rais Samia ameonekana mara kadhaa akiwatembelea viongozi wakuu wastaafu mbalimbali majumbani mwao au kukutana nao ikulu kwa mazungumzo na kubadilishana uzoefu wa maswala kadhaa ya uongozi.

Ila sijawahi kumuona akikutana au akimjulia hali mzee Edward Ngoyai Lowasa(waziri mkuu mstaafu).

Je, ni lini Rais Samia atamjulia hali mzee Lowasa kama anavyofanya kwa viongozi wengine?

Asanteni
Siyo moja ya majukumu ya rais, wewe ulishaenda kumuona lowassa?
 
Back
Top Bottom