Kwanini Rais Samia Hassan hadi sasa hajatoa tamko rasmi kuhusu mkataba wa DP World

Kwanini Rais Samia Hassan hadi sasa hajatoa tamko rasmi kuhusu mkataba wa DP World

umetumia nini kupima wananchi walio wengi?

Ningependa kujua sababu za msingi za Rais Samia Suluhu Hassan kutowajibika kama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa tamko lake rasmi kuhusu mkataba tatanishi wa DPW ambao kwa kiasi kikubwa unapingwa na Wananchi waliyo wengi? Nini sababu ya ukimya wa Rais Samia Suluhu Hassan?
 
Ningependa kujua sababu za msingi za Rais Samia Suluhu Hassan kutowajibika kama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa tamko lake rasmi kuhusu mkataba tatanishi wa DPW ambao kwa kiasi kikubwa unapingwa na Wananchi waliyo wengi?

Nini sababu ya ukimya wa Rais Samia Suluhu Hassan?
Ni mmoja wao
 
Si mlisema wananchi walipewa muda mdogo kujadili DPW. Sasa amewaachia wananchi wajadili mpaka waseme imetosha ndio mkuu atatoa tamko lake. By the way, nilimsikia akiwashangaa baadhi ya watanzania wakirumbana wakati Kenya wakiwapa DPW bandari zote mpaka za mito na visimani.
Sijui takwimu unezipata wapi za kusema wananchi walio wengi wanapinga mkataba. Mimi sijawahi kuziona takwimu, bali mwenyewe nilijaribu kupita mjini na vijijini na kuwauliza juu ya DPW. Vijijini kati ya 20 niliowauliza ni 4 tu ndio walifahamu DPW ni nini. Wengi wao walidhani ni aina mpya ya mbolea ya Ruzuku.
 
Simply kwa sababu ni mhusika mkuu, hawezi kutoa tamko analojua litamfunga mwenyewe, zile safari zake za kwenda Dubai kila siku huo ndio mchezo wa hovyo aliokuwa akienda kuwafanyia watanganyika.

Akitegemea ungekuwa siri, bahati mbaya siri imefichuka, sasa hana ujanja, hajui la kufanya, anasubiri msaada wa chawa na wafia dini waje kumsaidia, amefeli, hafai kutuongoza.
Alisha waagiza chawa wake watoe elimu Kwa wananchi juu ya mkataba
 
Ningependa kujua sababu za msingi za Rais Samia Suluhu Hassan kutowajibika kama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa tamko lake rasmi kuhusu mkataba tatanishi wa DPW ambao kwa kiasi kikubwa unapingwa na Wananchi waliyo wengi?

Nini sababu ya ukimya wa Rais Samia Suluhu Hassan?
1. Haki ya kisiasa imemchanganya
2. Nchi ya fedha za kigeni hakuna
3. Hazina pametakata
4. Mikataba imevuja kabla dili halijakaa sawa
5. CCM imemshinda ha kiuongozi
 
Ningependa kujua sababu za msingi za Rais Samia Suluhu Hassan kutowajibika kama Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa tamko lake rasmi kuhusu mkataba tatanishi wa DPW ambao kwa kiasi kikubwa unapingwa na Wananchi waliyo wengi?

Nini sababu ya ukimya wa Rais Samia Suluhu Hassan?
Kwanza anajua kuwa kuna makosa kwenye mkataba huo. Pili yeye hana uhakika na ukweli wa mkataba huo kwamba ni makubaliano au mkataba, uhalali wa Dubai kuingia mkataba, nk.

Hivyo vyote ndio anajifunza sasa na hata yeye anashangaa kumbe kuna hili, kumbe kuna lile?!

Unajua viongozi wetu wavivu sana na hapo ndipo Africa inapoangukia. Hata mkataba muhimu kama huu utakuta hajausoma wote yeye kapewa abstract tu. Ni viongozi wangapi wanaoweza kuandika hotba zao wengi hupenda kukuta zimeandikwa na huja kuzisoma tu.
 
Kazi ya Serikali ni kushawishi siyo kulazimisha. Serikali inapochagua mkabala wa kulazimisha ni sawa na kuchagua kushindwa. Mradi mkubwa wa programu ya vijiji vya ujamaa haukufanikiwa ukiachilia mbali mipango ya wataalamu wa Serikali waliyoiweka ambayo haikuangalia mahitajibhalisi ya jamii.

Sakata hili la Bandari limebeba sura tofauti sana kwani linaonekana kupingwa siyo tu na wapinzani bali pia viongozi waasisi wa Serikali iliyopo madarakani. Elimu inayotolewa na viongozi wa Chama na Serikali kujenga ushawishi juu ya hili bado inakanganya sana kwani maelezo yao wenyewe wenyewe yanapingana.

Wananchi hatuwezi kukataa maendeleo ila tunakataa masharti tata yaliyopo kwenye mkataba huu wa maendeleo. Tatizo ni masharti yanayobeba maslahi ya upande mmoja na anayoonesha wajibu na haki za upande mmoja zaidi ya upande mwingine.
 
Back
Top Bottom