Kwanini Rais Samia Hassan hadi sasa hajatoa tamko rasmi kuhusu mkataba wa DP World

umetumia nini kupima wananchi walio wengi?

 
Ni mmoja wao
 
Si mlisema wananchi walipewa muda mdogo kujadili DPW. Sasa amewaachia wananchi wajadili mpaka waseme imetosha ndio mkuu atatoa tamko lake. By the way, nilimsikia akiwashangaa baadhi ya watanzania wakirumbana wakati Kenya wakiwapa DPW bandari zote mpaka za mito na visimani.
Sijui takwimu unezipata wapi za kusema wananchi walio wengi wanapinga mkataba. Mimi sijawahi kuziona takwimu, bali mwenyewe nilijaribu kupita mjini na vijijini na kuwauliza juu ya DPW. Vijijini kati ya 20 niliowauliza ni 4 tu ndio walifahamu DPW ni nini. Wengi wao walidhani ni aina mpya ya mbolea ya Ruzuku.
 
Alisha waagiza chawa wake watoe elimu Kwa wananchi juu ya mkataba
 
1. Haki ya kisiasa imemchanganya
2. Nchi ya fedha za kigeni hakuna
3. Hazina pametakata
4. Mikataba imevuja kabla dili halijakaa sawa
5. CCM imemshinda ha kiuongozi
 
Kwanza anajua kuwa kuna makosa kwenye mkataba huo. Pili yeye hana uhakika na ukweli wa mkataba huo kwamba ni makubaliano au mkataba, uhalali wa Dubai kuingia mkataba, nk.

Hivyo vyote ndio anajifunza sasa na hata yeye anashangaa kumbe kuna hili, kumbe kuna lile?!

Unajua viongozi wetu wavivu sana na hapo ndipo Africa inapoangukia. Hata mkataba muhimu kama huu utakuta hajausoma wote yeye kapewa abstract tu. Ni viongozi wangapi wanaoweza kuandika hotba zao wengi hupenda kukuta zimeandikwa na huja kuzisoma tu.
 
Kazi ya Serikali ni kushawishi siyo kulazimisha. Serikali inapochagua mkabala wa kulazimisha ni sawa na kuchagua kushindwa. Mradi mkubwa wa programu ya vijiji vya ujamaa haukufanikiwa ukiachilia mbali mipango ya wataalamu wa Serikali waliyoiweka ambayo haikuangalia mahitajibhalisi ya jamii.

Sakata hili la Bandari limebeba sura tofauti sana kwani linaonekana kupingwa siyo tu na wapinzani bali pia viongozi waasisi wa Serikali iliyopo madarakani. Elimu inayotolewa na viongozi wa Chama na Serikali kujenga ushawishi juu ya hili bado inakanganya sana kwani maelezo yao wenyewe wenyewe yanapingana.

Wananchi hatuwezi kukataa maendeleo ila tunakataa masharti tata yaliyopo kwenye mkataba huu wa maendeleo. Tatizo ni masharti yanayobeba maslahi ya upande mmoja na anayoonesha wajibu na haki za upande mmoja zaidi ya upande mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…