Kwanini Rais Samia Suluhu anasafiri?

Kwanini Rais Samia Suluhu anasafiri?

That totally nonsense.
Tusiendelee kupigia chapuo safari za kipurure kama hizi.
Mtangulizi wake(JPM) hakuwa na tabia ya kusafiri ovyo ovyo kama hivi lakini ndo Rais pekee aliyeweza kufanya mambo makubwa sana katika Nchi kwa kipindi kifupi.
Hapo utatumbia nini?
Kwa kifupi, Nchi yetu imepatwa.
 
Rais Samia Suluhu amefanya safari za nje 19 ndani ya siku 477 tangu ameingia madarakani. Zinaweza kuonekana kama ni safari nyingi sana, lakini shida sio wingi wa safari, bali tija inayoweza kuletwa na safari hizo katika taifa letu.

Rais kusafiri sio jambo la ajabu kabisa, hasa kwa nchi za Afrika. Sababu ya watu kuwa na nongwa juu ya safari anazofanya Rais Samia zinatokana na tabia aliyokuwa nayo mtangulizi wake. Kama mtangulizi wake ingekuwa ni mtu wa kusafiri sana, pengine isingekuwa ajabu kwa Rais Samia Suluhu.

Ila swali la msingi hapa ni kwa nini Rais Samia Suluhu husafiri mara kwa mara, na je safari hizo za nje zina faida?

Ukisoma andiko la Going Global: Assessing Presidential Foreing Travel lililoandikwa na Amnon Cavari na Micah ables utaelewa zaidi kwanini huwa viongozi hasa maraisi husafiri na faida zake ni zipi. Hapa nitakupa kwa uchache.

Sababu ya kwanza, ili kuimarisha mahusiano ya kirafiki, kiuchumi na kuimarisha pia ulinzi wa taifa lako, kuna wakati ni lazima Rais asafiri na afanye kitu kinatwa 'Face to Face Diplomacy'. Mfano, Rais Samia Suluhu alisafiri kwenda Uganda May 10, 2020 na moja ya mikataba iliyofungwa huko, ilikuwa ni mikataba ya kuimarisha ulinzi wa mataifa mawili, Tanzania na Uganda.

Kutafuta mikopo nafuu (concessional loans). Rais Samia Suluhu aliposafiri kwenda makao makuu ya Umoja wa Ulaya Ubelgiji Februari 16, 2022, kule alipatiwa mikopo nafuu ambayo kwa hakika, si aina ya mikopo ambayo kila nchi ina nafasi ya kupatiwa. Mikopo hii haina masharti magumu, haina riba kubwa na hutumia muda mrefu kurudisha fedha. Mikopo hii ni muhimi sana kwa ajili ya kuimarisha huduma za kijamaa nchini.

Kuleta wawekezaji nchini. Mwekezaji akizungumza na Balozi wa Waziri haina uzito mkubwa kama ambapo ataongea na Raisi. Rais ndio Top Diplomat kwenye nchi yeyote. Mwekezaji akipa guarantee ya Rais nchini ni rahisi sana kwa mwekezaji huyo kuja nchini na kufanya uwekezaji. Mfano, Rais Samia Suluhu alipokwenda Marekani April 14, 2022 kule aliweza kuleta uwekezaji wa USD 1 billion (2 trillion shillings) nchini.

Katika wakati kama huu ambao dunia inakumbwa na janga la uhaba wa nishati ya mafuta, safari ya Rais Samia Suluhu Oman ilikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa Tanzania. Omani ni mzalishaji wa 21 wa mafuta duniani, inazalisha pipa milioni moja kwa siku. Tanzania ilisoma mazingira ya kidunia na kuona kwamba vita ya Urusi na Ukraine inaweza kuchukua muda mrefu sana hadi kwisha na tukazidi kuteseka na bei ya mafuta.

Raisi alikwenda kule na Waziri wa Nishati, January Makamba, kwanini? Kule Rais alikwenda kuweka mazingira mazuri ya Tanzania kupata mafuta kwa urahisi wakati dunia inakumbwa na jambo hilo. Rais Samia Suluhu ana watu wanayoisoma dunia na kumshauri cha kufanya kutokana na hali halisi ili kunusuru uchumi wa taifa letu.

Rais Samia Suluhu alikwenda Kenya, Tanzania na Kenya ziliondoleana vikwazo vya kibiashara ambavyo vilisababishwa wakati wa utawala wa John Pombe Magufuli.

Ni lazima Rais asafiri kurejesha imani ya wawekezaji. Pasi na kumumunya maneno, Rais Samia Suluhu alichukua nchi ikiwa na hali mbaya sana hasa kwenye uhusiano wa kimataifa. Haina budi Rais Samia kusafiri sana kusafisha hatua mbaya za mtangulizi wake. JPM alizokorofisha nchi tajiri, zikaacha kutoa misaada na wawekezaji wao kuanza kususa kuja Tanzania. Hii ni awamu ya Samia Suluhu sasa, ili mambo yamwendee sawa, ni lazima atoke kuweka mambo sawa.

Niseme tu, safari za Rais Samia Suluhu zimekuwa na faida nyingi sana kwa Tanzania. Safari za Rais Samia Suluhu zimelutea mikopo nafuu, zimetuletea wawekezaji na pia ujenzi wa miundombinu ya bure kabisa, mfano Uwanja wa Ndege wa KIA na serikali ya Oman. Hivyo basi, Rais akisafiri, mnapaswa kumwombea dua arejee salama kwani ametoka kwenda kutupigania.
Watanzania wanakwambia tuna kila kitu ni wajibu wetu kujitegemea. Kwamba mikopo ikiwa mingi itatusumbua kuilipa.

Wapiga domo wapo wengi sana hapa TZ, lakini kubadilisha hayo maneno kuwa vitendo ndio mtihani ulipo.
 
That totally nonsense.
Tusiendelee kupigia chapuo safari za kipurure kama hizi.
Mtangulizi wake(JPM) hakuwa na tabia ya kusafiri ovyo ovyo kama hivi lakini ndo Rais pekee aliyeweza kufanya mambo makubwa sana katika Nchi kwa kipindi kifupi.
Hapo utatumbia nini?
Kwa kifupi, Nchi yetu imepatwa.
Kushindwa kusafiri kwa JPM hakukuwa eti ni kwa sababu ya kukataa ule ushawishi wa mataifa ya kigeni, hakuwa na uwezo katika masuala ya kimataifa. Na aliujua udhaifu wake akatafuta akina Kabudi na hayati Mahiga ili wamsaidie.

Alikuwa ni mchapa kazi sana hilo halina ubishi lakini huwezi kujitegemea mwenyewe pasipo kushirikiana na mataifa mengine.

Wakati mwingine media zetu zinao mabingwa wa propaganda wanaitengeneza habari mpaka inaonekana ni ya kweli huku rais akipambwa lakini ndani kabisa ni sehemu tu ya yeye mheshimiwa kuwa na mkono mzito ndani ya vyombo vya habari.
 
Hata akikaa hapa nchini ana kazi gani anayoifanya ya maana..mana kila uchwao maisha ya wananchi yanazidi kuwa magumu naye yupo kimya..aende tu akazurure mana ndio kitu anachokiweza.

Tunajua rimoti zote ziko msoga...yeye ni ceremonial leader tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
That totally nonsense.
Tusiendelee kupigia chapuo safari za kipurure kama hizi.
Mtangulizi wake(JPM) hakuwa na tabia ya kusafiri ovyo ovyo kama hivi lakini ndo Rais pekee aliyeweza kufanya mambo makubwa sana katika Nchi kwa kipindi kifupi.
Hapo utatumbia nini?
Kwa kifupi, Nchi yetu imepatwa.
Wtz wengi wajinga hawalioni hili.
 
Hata akikaa hapa nchini ana kazi gani anayoifanya ya maana..mana kila uchwao maisha ya wananchi yanazidi kuwa magumu naye yupo kimya..aende tu akazurure mana ndio kitu anachokiweza.

Tunajua rimoti zote ziko msoga...yeye ni ceremonial leader tu.

#MaendeleoHayanaChama
Mara mia huyu kuliko yule mwendakuzimu,kila mtu aliishi kwa hofuna mashaka yakuuliwa
 
Tumuache aende aisee maana inaonekana mambo ndio yako hivyo.

Mimi aniajiri kupaki nguo na kufunga mabegi ya msafara wake.

I am Ready for my new role as long as napanda ndege na kuzunguka ulimwengu.

Tukiwa angani huko tunawacheki tu namnanavyopambana na tozo.
 
Lazima tujifunze kuwa na hoja za msingi tukitaka kuzungumzia jambo. Sidhani kama unajitendea haki kujadili suala kama hili kwa kutumia akili za kawaida. Kwenye andiko langu nimetoa faida za Rais Samia Suluhu kusafiri nje ya nchi. Hebu onesha safari moja tu ambayo Rais Samia Suluhu amefanya nje nchi na haikuwa na faida, mimi nitakufa faida yake.

Kusema safari Zina tija au kufanya safari ni jambo moja, safari kuleta tija au wananchi kufaidika na hizo safari ni jambo lingine.
 
Rais Samia Suluhu amefanya safari za nje 19 ndani ya siku 477 tangu ameingia madarakani. Zinaweza kuonekana kama ni safari nyingi sana, lakini shida sio wingi wa safari, bali tija inayoweza kuletwa na safari hizo katika taifa letu.

Rais kusafiri sio jambo la ajabu kabisa, hasa kwa nchi za Afrika. Sababu ya watu kuwa na nongwa juu ya safari anazofanya Rais Samia zinatokana na tabia aliyokuwa nayo mtangulizi wake. Kama mtangulizi wake ingekuwa ni mtu wa kusafiri sana, pengine isingekuwa ajabu kwa Rais Samia Suluhu.

Ila swali la msingi hapa ni kwa nini Rais Samia Suluhu husafiri mara kwa mara, na je safari hizo za nje zina faida?

Ukisoma andiko la Going Global: Assessing Presidential Foreing Travel lililoandikwa na Amnon Cavari na Micah ables utaelewa zaidi kwanini huwa viongozi hasa maraisi husafiri na faida zake ni zipi. Hapa nitakupa kwa uchache.

Sababu ya kwanza, ili kuimarisha mahusiano ya kirafiki, kiuchumi na kuimarisha pia ulinzi wa taifa lako, kuna wakati ni lazima Rais asafiri na afanye kitu kinatwa 'Face to Face Diplomacy'. Mfano, Rais Samia Suluhu alisafiri kwenda Uganda May 10, 2020 na moja ya mikataba iliyofungwa huko, ilikuwa ni mikataba ya kuimarisha ulinzi wa mataifa mawili, Tanzania na Uganda.

Kutafuta mikopo nafuu (concessional loans). Rais Samia Suluhu aliposafiri kwenda makao makuu ya Umoja wa Ulaya Ubelgiji Februari 16, 2022, kule alipatiwa mikopo nafuu ambayo kwa hakika, si aina ya mikopo ambayo kila nchi ina nafasi ya kupatiwa. Mikopo hii haina masharti magumu, haina riba kubwa na hutumia muda mrefu kurudisha fedha. Mikopo hii ni muhimi sana kwa ajili ya kuimarisha huduma za kijamaa nchini.

Kuleta wawekezaji nchini. Mwekezaji akizungumza na Balozi wa Waziri haina uzito mkubwa kama ambapo ataongea na Raisi. Rais ndio Top Diplomat kwenye nchi yeyote. Mwekezaji akipa guarantee ya Rais nchini ni rahisi sana kwa mwekezaji huyo kuja nchini na kufanya uwekezaji. Mfano, Rais Samia Suluhu alipokwenda Marekani April 14, 2022 kule aliweza kuleta uwekezaji wa USD 1 billion (2 trillion shillings) nchini.

Katika wakati kama huu ambao dunia inakumbwa na janga la uhaba wa nishati ya mafuta, safari ya Rais Samia Suluhu Oman ilikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa Tanzania. Omani ni mzalishaji wa 21 wa mafuta duniani, inazalisha pipa milioni moja kwa siku. Tanzania ilisoma mazingira ya kidunia na kuona kwamba vita ya Urusi na Ukraine inaweza kuchukua muda mrefu sana hadi kwisha na tukazidi kuteseka na bei ya mafuta.

Raisi alikwenda kule na Waziri wa Nishati, January Makamba, kwanini? Kule Rais alikwenda kuweka mazingira mazuri ya Tanzania kupata mafuta kwa urahisi wakati dunia inakumbwa na jambo hilo. Rais Samia Suluhu ana watu wanayoisoma dunia na kumshauri cha kufanya kutokana na hali halisi ili kunusuru uchumi wa taifa letu.

Rais Samia Suluhu alikwenda Kenya, Tanzania na Kenya ziliondoleana vikwazo vya kibiashara ambavyo vilisababishwa wakati wa utawala wa John Pombe Magufuli.

Ni lazima Rais asafiri kurejesha imani ya wawekezaji. Pasi na kumumunya maneno, Rais Samia Suluhu alichukua nchi ikiwa na hali mbaya sana hasa kwenye uhusiano wa kimataifa. Haina budi Rais Samia kusafiri sana kusafisha hatua mbaya za mtangulizi wake. JPM alizokorofisha nchi tajiri, zikaacha kutoa misaada na wawekezaji wao kuanza kususa kuja Tanzania. Hii ni awamu ya Samia Suluhu sasa, ili mambo yamwendee sawa, ni lazima atoke kuweka mambo sawa.

Niseme tu, safari za Rais Samia Suluhu zimekuwa na faida nyingi sana kwa Tanzania. Safari za Rais Samia Suluhu zimelutea mikopo nafuu, zimetuletea wawekezaji na pia ujenzi wa miundombinu ya bure kabisa, mfano Uwanja wa Ndege wa KIA na serikali ya Oman. Hivyo basi, Rais akisafiri, mnapaswa kumwombea dua arejee salama kwani ametoka kwenda kutupigania.
Inawezekana abawashwa miguuni au ameambukizwa na JMK.
 
Safari nyingi ni za kiwaki tu.
Hazina tija Hadi ifike 2025 safari zitafiki 5000

Wiki nchini wiki nje ya nchi

Akili zangu za kawaida tu
Hivi Baba akikaa ndani tuuu!! kucheza na mkewe na watoto mtakula kweli? nini? lazima aende kazini! akirudi mmpokee!! Dhahabu mnachimbiwa ili mle

hakuna mtanzania anae jua matumizi ya dhahabu zaidi ya mikufu! sasa akikaa tu wachimabaji watajuaje kuwa Mama ardhini kwake ana dhahbu?? Mafuta, Nickel, Almasi nk lazima atembee huko!!

watoto hamana dawa sasa mama lazima atoke akaitafute dawa ya homa!! siyo mtoto ana homa mna kaa tuuu humo ndani km jiwe!...........Jiwe aliwasusa wa nje nao wakamsusa mpaka akajifia humo Bongo lile jamaa halikuwa na Rafiki!

Mnataka Mama nae asiwe na marafiki yeye km Rais akiumia nani atamsaidia na nyie mmechoka mbaya!!! Mama laima asaidiwe kwa level ya uRais! nyambaf
 
Mbali na uwezo mdogo alionao & akili za kitegemezi...Eneo analomudu vizuri ni safari za hapa na pale.
 
Dah....eti mikopo yenye masharti nafuu halafu hamsemi ni masharti gani.....halafu riba nafuu hamsemi ni kiasi gani......Hivi hamuoni Kama mnaandika upuuzi? 😂😂😂😂
 
Safari nyingi ni za kiwaki tu.
Hazina tija Hadi ifike 2025 safari zitafiki 5000

Wiki nchini wiki nje ya nchi

Akili zangu za kawaida tu
Safari nyingi ni za kiwaki tu.
Hazina tija Hadi ifike 2025 safari zitafiki 5000

Wiki nchini wiki nje ya nchi

Akili zangu za kawaida tu
Maskini bana? mnaona Rais akisafiri ni anakula rahaaaaa!! Ni Km mnachukulia mkulima kupanda basi la kijiji ni kwa nadra sana......ile ya mama kwa ma-born town sisi ndo tunaona ni shida mnoo.. Gujidege....lile ni km bus tu air msae!!!
Acheni ushamba banaaa....nyie lazima tuwape polisi hela wavi gonge! gonge vichwa ivo na virungu.. muelewega....shida zooote zile anazo kumbana nazo safarini.....mara Mam alale stand..akisubiri usafiri mwingine usiku... kazi ndogo hiyo??? Wkt huo wewe umelala na mwajuma ndala ndefu!!
Hapa nilipo nawaza jinsi ntakavyo kwenda Australia..Newzealand
.japani halafu nimalizie Canada.asa nawauliza kazi ndogo hiyo??? Mwezi mzima sioni tako la mke wangu..hivi hamuoni??? Haya yoote ni ili mle.....Mama kaza kamba tu hawa ni vilaza hawajijui.
 
Lazima tujifunze kuwa na hoja za msingi tukitaka kuzungumzia jambo. Sidhani kama unajitendea haki kujadili suala kama hili kwa kutumia akili za kawaida. Kwenye andiko langu nimetoa faida za Rais Samia Suluhu kusafiri nje ya nchi. Hebu onesha safari moja tu ambayo Rais Samia Suluhu amefanya nje nchi na haikuwa na faida, mimi nitakufa faida yake.
Baby yasamehe tu...haya matoto ya maskini shida sana...ni zigo hasaa...hayaelewagi somo.
 
Back
Top Bottom