Kwanini RC wa Manyara, Makongoro Nyerere alimpigia saluti ya kijeshi Rais wakati wa kiapo?

Kwanini RC wa Manyara, Makongoro Nyerere alimpigia saluti ya kijeshi Rais wakati wa kiapo?

Hamjui kuwa Makongoro ni askari Jeshi? Kapigana vita ya Kagera huyu sio sawa na haya makinda yanalelewa kama mayai hata ubunge yanapata kwa nguvu za baba zao!!
Ni mwanajeshinaliyesomea urusi
 
Nafahamu, kwa Afisa wa jeshi (Kuanzia Second Lieutenant) Lazima isipungue 55
Sasa Bwana Mako ka Staafu 1990 akiwa na umri gani ?
Huyu Msanii hakuwa Mwanajeshi pasee, ni wale waliopelekwa vitani na kurudi
Hutokaa uone akiwa katika Military Uniform.
Ni mwanajeshi. Amejifunza mizinga Urusi.
 
Kwa askari yeyote, uwe bado kazini au umestaafu, hiyo ndiyo heshima inavyotolewa kama hujavaa share za jeshi. Unabana mikono, kifua mbele na unainua visigino - kwa ukakamavu. Ni kwamba watu wanapuuzia tu! Lakini mwelekeo ni huo. Zoezi hili ni badala ya kupiga saluti kwa yule ambaye amevaa sare za kijeshi.
Kwa hiyo huyu bwana siyo chizi, bali anafuata miongozo mizuri vema.
 
Kwa askari yeyote, uwe bado kazini au umestaafu, hiyo ndiyo heshima inavyotolewa kama hujavaa share za jeshi. Unabana mikono, kifua mbele na unainua visigino - kwa ukakamavu. Ni kwamba watu wanapuuzia tu! Lakini mwelekeo ni huo. Zoezi hili ni badala ya kupiga saluti kwa yule ambaye amevaa sare za kijeshi.
Kwa hiyo huyu bwana siyo chizi, bali anafuata miongozo mizuri vema.
Kuna kimoja pia lazima ubane na hujakizungumzia mkuu[emoji41][emoji41]
 
Kwa nimjuavyo Kaka yangu huyu najua Nguvu kubwa sana ilitumika Usiku wa kabla wa Tukio Kumzuia asipige ' Gambe ' kisha akaamka nazo hapo Uapishoni Ikulu.

Hata hivyo nilitaka Kuamini kuwa siku hiyo hakuonja ' Gambe ' ili apate ' Stimu ' ila kwa nilivyoiona tu Picha hii na jinsi alivyonyooka na alivyoviinua Visigino vyake huku akiwa ameufumba Mdomo hivyo ili Mama asiisikie harufu ya TBL Mchikichini naanza kuhisi huenda aliwatoroka waliokuwa Wakimlinda na akaenda ' Kuzimua ' zake kidogo.

Kaka yangu nakutakia kila la kheri huko Mkoani Manyara kwa hayo Majukumu yako mapya na ya mwisho mwisho kupewa na Marais wa Tanzania ambao wanaiheshimu Familia yenu hivyo usituangushe Nduguzo ' Wazanaki ' , usimuangushe Mama ( Mheshimiwa Rais ) Samia Suluhu Hassan, usiwaangushe wana CCM Wenzako, usimwangushe Mama yako Mzazi ( Mama Maria Nyerere ) ambaye anakutegemea Kiushauri na Kiusimamizi na pia usiwaangushe Watanzania ambao Wanakupenda na wana imani nawe japo ( Kibinadamu nawe una Mapungufu yako ) ila tutakuombea kwa Mwenyezi Mungu na yatarekebishika japo sasa unaelekea Saa 12 Jioni ( Uzeeni ) hivyo.

Kawe Kiongozi wa Mfano huko Manyara ili ukate Ngebe za wale Watesi wako na pia umuonyeshe Mheshimiwa Rais ( Mama ) Samia Suluhu Hassan kuwa hakukosea Kukuteua kwa Nafasi hiyo. Mdogo wako GENTAMYCINE nitakuwa nakuombea Dua kwa Mwenyezi Mungu na pia nitakuwa nakufanyia na yale Maombi yetu ya Kimila ( ya Kizanaki ) ili usiharibu na manbo yako yakuendee vyema huko Mkoani Manyara.
 
Alinichekesha sana kwenye mahojiano naada ya kuapishwa, alisema watu wanasema yeye anapenda wanawake akasema ndiyo, hata mama samia anampenda ndiyo maana kamteuwa dah.
 
Ka staafu lini ?
Maana 1995 alikuwa Mbunge kupitia NCCR
Hapo alikuwa ameshastaafu. Hata JK alikuwa kanali wa JWTZ akastaafu kwa kuzingatia sheria ya vyama vingi ya 1992 iliyoondoa siasa kwenye majeshi, kwahiyo waliotaka kuendelea na siasa iliwapasa kustaafu kazi ya jeshi kwanza.
 
Back
Top Bottom