Kwanini RC wa Morogoro anang'ang'ania kupewa Barakoa za Devota Minja ili azigawe yeye?

View attachment 1431642

Taarifa kutoka Morogoro zinadokeza kwamba Mbunge wa Chadema Mh Devota Minja amekamatwa na jeshi la polisi kwa Amri haramu ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , kwa kosa la kufuata muongozo wa kuzuia Corona wa shirika la Afya la dunia ( WHO ) na kugawa Barakoa bora kabisa za viwango vya N 95 kwa Wakazi wa Morogoro ili kuwakinga na maambukizi ya virusi hivyo hatari .

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Mh Mbunge ametakiwa kusalimisha Baracoa zake kwa RC huyo ili ofisi ya RC izigawe kwa wananchi , sasa sisi wafuatiliaji wabishi tumejiuliza kisa cha RC kung'angania barakoa za Mh Mbunge ili azigawe yeye , kwanini Ofisi ya Mkoa isitafute barakoa zake na kuzigawa badala ya kutaka kuchukulia kiki kwenye barakoa za mbunge wa Chadema ?

Bali kinachofahamika ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kabla ya kuteuliwa kuwa RC alikuwa Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Arusha .

Tatizo hili swala la Corona linachukuliwa kisiasa sana yaani mimi inafikia muda siamini kabisa wanasiasa hii inawahusu CCM, CHADEMA na wengine
Hivi hizi barakoa usipo print jina lako zinapungukiwa na nini hichi kitu kina kera sana

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kama waliopulizia dawa jijini Dar wanachunguzwa hawawezi kuachwa wagawa barakoa wagawe hovyo. Tusijesikia kesho watu Waliambukizwa kwa njia ya barakoa Za wanasiasa.
Wapelekewe wahusika wazigawe kadiri inavyofaa kuondoa Lawama mbeleni. Kikubwa nikutoa msaada, niliona wadau kadhaa wamekabidhi msaada kwa wahusika na wahusika ndio wanaogawa kadiri ya mahitaji. Shida ya wanasiasa Kwenye kila Kitu wanatafuta kiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm wacheni kuingiza udwanzi kwenye mambo ya msingi

Roho zenu mbaya zitajibiwa hapahapa duniani
 
Kufuata sheria bila shuruti ni shida kwa wengi hapa nchini. Kuna wadau wenye mamilioni kama siyo mabilioni wametoa msaada kwa kupitia channels zinazohusika. Sasa wengine ili wapate KIKI wanajifanya kufanya yao. Acha wauone mkono wa sheria..
 
Msimu huu hamtapata kitu kudadeki ! twishagundua kwamba mnakula misaada , tutawapelekea walengwa tu .
 
Kama waliopulizia dawa jijini Dar wanachunguzwa hawawezi kuachwa wagawa barakoa wagawe hovyo. Tusijesikia kesho watu Waliambukizwa kwa njia ya barakoa Za wanasiasa.
Wapelekewe wahusika wazigawe kadiri inavyofaa kuondoa Lawama mbeleni. Kikubwa nikutoa msaada, niliona wadau kadhaa wamekabidhi msaada kwa wahusika na wahusika ndio wanaogawa kadiri ya mahitaji. Shida ya wanasiasa Kwenye kila Kitu wanatafuta kiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakati Mangula analishwa sumu kwenye vikao vya ccm alipelekewa barakoa za Chadema ?
 
View attachment 1431642

Taarifa kutoka Morogoro zinadokeza kwamba Mbunge wa Chadema Mh Devota Minja amekamatwa na jeshi la polisi kwa Amri haramu ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , kwa kosa la kufuata muongozo wa kuzuia Corona wa shirika la Afya la dunia ( WHO ) na kugawa Barakoa bora kabisa za viwango vya N 95 kwa Wakazi wa Morogoro ili kuwakinga na maambukizi ya virusi hivyo hatari .

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Mh Mbunge ametakiwa kusalimisha Baracoa zake kwa RC huyo ili ofisi ya RC izigawe kwa wananchi , sasa sisi wafuatiliaji wabishi tumejiuliza kisa cha RC kung'angania barakoa za Mh Mbunge ili azigawe yeye , kwanini Ofisi ya Mkoa isitafute barakoa zake na kuzigawa badala ya kutaka kuchukulia kiki kwenye barakoa za mbunge wa Chadema ?

Bali kinachofahamika ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kabla ya kuteuliwa kuwa RC alikuwa Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Arusha .
CCM NAO WATATENGENEZA ZAO WAZIGAWE NCHI NZIMA
 
"Wakuu huko jamii forum wananiogopa mbaya.Nacomment hovyohovyo tu.Wapinzani nawananga kiama. Tokeni huku WhatsApp comrades njooni JF" Bia yetu(WhatsApp grp sisiem)
Huyo ni mwenyekiti wa usalama wa mkoa

Huyo minja akileta janja anaenda selo
 
Kufuata sheria bila shuruti ni shida kwa wengi hapa nchini. Kuna wadau wenye mamilioni kama siyo mabilioni wametoa msaada kwa kupitia channels zinazohusika. Sasa wengine ili wapate KIKI wanajifanya kufanya yao. Acha wauone mkono wa sheria..
Mabingwa wa kula rambirambi na misaada wamekaukiwa hoja. Mvuto huletwa na imani ya wananchi ambayo hujengwa juu ya haki sio na Polisi wala vitisho.Mtahangaika sana.
 
Huyo ni mwenyekiti wa usalama wa mkoa

Huyo minja akileta janja anaenda selo
Mimi huwa naona akili za aina hii ni za kipumbavu sana kuanzia anaye kataza kugawa barakoa hadi wanao muunga mkono maana wao hawajali watu wanajali siasa ni WAPUMBAVU Akwa herufi kubwa.
 
Sasa na yeye kwa nini aweke jina lake kwenye hizo barakoa??
 
Back
Top Bottom