Kwanini RC wa Morogoro anang'ang'ania kupewa Barakoa za Devota Minja ili azigawe yeye?

Kwanini RC wa Morogoro anang'ang'ania kupewa Barakoa za Devota Minja ili azigawe yeye?

Abood ana akili unafikiri kama mbunge wenu huyo wa Ufipa.Abood aliomba kibali.
Ebu peleka ujinga wako huko kuomba kibali ndiyo Akili? Mbunge minja alifuata utaratibu wote lakini RC wako akataka apewe barakoa azigawe mwenyewe ndipo mbunge akaona ni ujinga mkubwa kufanya hivyo wakati Abood kagawa mwenyewe, acheni ubaguzi wa kishamba
 
View attachment 1431642

Taarifa kutoka Morogoro zinadokeza kwamba Mbunge wa Chadema Mh Devota Minja amekamatwa na jeshi la polisi kwa Amri haramu ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , kwa kosa la kufuata muongozo wa kuzuia Corona wa shirika la Afya la dunia ( WHO ) na kugawa Barakoa bora kabisa za viwango vya N 95 kwa Wakazi wa Morogoro ili kuwakinga na maambukizi ya virusi hivyo hatari .

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Mh Mbunge ametakiwa kusalimisha Baracoa zake kwa RC huyo ili ofisi ya RC izigawe kwa wananchi , sasa sisi wafuatiliaji wabishi tumejiuliza kisa cha RC kung'angania barakoa za Mh Mbunge ili azigawe yeye , kwanini Ofisi ya Mkoa isitafute barakoa zake na kuzigawa badala ya kutaka kuchukulia kiki kwenye barakoa za mbunge wa Chadema ?

Bali kinachofahamika ni kwamba Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kabla ya kuteuliwa kuwa RC alikuwa Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Arusha .
CCM kwao kila jambo ni siasa, ni ujinga uliopitiliza kiwango lakini ni utamaduni wa kiafrika pia. Tazama alichofanya Mseven katika ugawaji wa vyakula.
 
Back
Top Bottom