Kwanini RC wa Morogoro anang'ang'ania kupewa Barakoa za Devota Minja ili azigawe yeye?

Sioni tofauti ya Chadema na CCM kimatendo na kimikakati.
Wote ni wapenda madaraka na umaarufu na kuweka mbele maslahi binafsi.

Chadema mpaka sasa hakijainyesha utofauti na CCM katika kuwaunganisha watanzania bila kujali itikadi zao.

Hivi Devota Minja angepungukiwa na nini kama angemkabidhi Mkuu wa Mkoa Barakoa hizo akiwa na waandishi wa habari ,tena kwa kumwambia azigawe mkoani humo bila kujali itikadi za kisiasa?

Ni lazima mgao kama huo upitie serikalini mana serikali ndiyo kiunganishi kati ya wananchi na wizara ya afya katika kudhibiti magonjwa.
Lakini pia ingewezekana kabisa kumshirikisha hata kiongozi wa CCM mkoa ili washirikiane kuzigawa . Hii ingetupa ladha mpya ya siasa za kizalendo na kistarabu lakini zenye kujali Taifa kuliko vyama vyetu na madaraka yetu.

Chadema fanyeni siasa tofauti na za CCM ili tuone sababu ya kuwachagua .
Kwa sasa hakuna tofauti kati ya CCM na Chadema. Wote wanalipa visasi ,wote wanajenga chuki za kisiasa na mfarakano baina ya vyama.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa na yeye kwa nini aweke jina lake kwenye hizo barakoa??
Lengo la kuandika jina lake nadhani ili kupata recognition na kudhibiti zisiuzwe. Kwenye hilo amefanya poa tu japo kisiasa pia inamsaidia.
 
Hakuna kitu ambacho sikipend kama kutoa msaada na kujianika...........!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una akili timamu wewe?? Ulimsikiliza mwenyekiti wako wa ccm Taifa akiwqhutubia wakuu wa vyombo vya dola?? Alisema Ni Bora watanzania wajishonee barakoa zao kuliko hizo unazozitaka wewe, acha roho ya kike ya wivu au wewe ni wema sepenga Nini?😜
 
Kwa hiyo wewe ni mfuatiliaji mbishi! Alafu kama mkuu wa mkoa anataka kuzuia ugawaji ambao hauzingatii social distancing? Kuna tatizo gani? Sababu wewe ni mbishi basi muda wote ni kubisha tu!
 

Ukileta jambo wewe mwandishi usichague upande kuipa habari yako iwe na nguvu, Sisi wasomaji tuone nani mwenye makosa hapo
 
Ila Devotha nae ndion
Ila Devotha naye ndio nini kuzichorachora hizo barakoa kwa jina lake? Kwani angegawa ambazo hazina jina ingekuwaje? Siasa hizi, msaada na matangazo meeeengi!
 
Kwani yamekuwa ni mashindano?? Mimi naona wote hao ni wapuuzi, huyo Mbunge pamoja na Mkuu wa mkoa..
 
Shida ya Chadema huu ugonjwa wanaufanyia siasa. Ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu..

Rostam ametoa mabilioni na vifaa kinga alikabidhi Mamlaka, kwani alishindwa kusimama Mnazi Mmoja au Ofisini kwake akawa anagawa barakoa??

Huyo Mbunge ni mpuuzi na hata huyo Mkuu wa Mkoa nae mpuuzi..
 
Mkuu wanasiasa wote ni wapuuzi na wajinga tu, sio CCM, CDM, CUF, ACT wote ni wabinafsi na wachoyo. Hata wanaopiga kelele za siasa humu kila siku nao wapuuzi hawana kazi za kufanya..

Mtu unashangaa kila ukiingia humu wanaoanzisha mada ni wale wale na ligi zao ni zile zile. Watu wa ovyo ovyo sana wajinga wajinga wengine ndio hao wanajiita sijui minyoo wengine bia yetu wote ni malofa tu..
 
Halafu
Halafu ukizingatia alikuwa ni mwenyekiti wa mkoa chama cha kijani na njano kabla ya uteuzi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…