Kwanini reli ya Kusini ilisitishwa? Kuna jambo tunafichwa?

Huo ujinga ulioaminishwa na Mwendazake ni scam.

Tazara bei ni nafuu,wanayotumia huo usafiri vs Mabasi ni wangapi? Hakuna mtu atapanda treni za ubabaishaji za Bongo aache basi hayupo

Acha upuuzi,kati ya nauli ya treni na basi na ndege,wapi kuna nauli nafuu katika usafirishaji wa raia na mizigo??
 
Acha upuuzi,kati ya nauli ya treni na basi na ndege,wapi kuna nauli nafuu katika usafirishaji wa raia na mizigo??
Inategemea, baadhi ya nchi basi ndio usafiri nafuu kabisa, huku nchi nyingine treni ndio usafiri nafuu kabisa.
 
Njia mwafaka ya kusafirisha gesi ni pipeline , hayo mahindi na korosho quantity zivunazwo barabara tosha , reli ile haina umuhimu wowote kwa sasa economically , ni deni tu tunaongeza
 
Unaweza kuwa sahihi. Ila hadithi iliyopo baada ya Vita kuu ya dunia serikali ya Uingereza iliamua kuanzisha mradi ili kuwasaidia watanzania waliopigana upande wa Uingereza. Ile miradi ilikufa Ila inasemekana ile reli baadae haikuwa na faida, wengine wanasema sababu ya kuwepo Kambi za wapigania Uhuru serikali iliamua kung'oa reli. Pia Kuna taarifa ambazo umepewa mojawapo inaweza kuwa sahihi.
 
Mpunguze uchawi na ushirikina
 
Kusini sio elimu
Sio miundombinu
Sio kipato cha mtu mmoja mmoja hakuna nafuu(nimefika nimejionea
Wewe ni muongo wa kutupwa huku kusini watu tuna elimu ndio maana hausikii matendo ya kuuwa vikongwe,kuua albino,mauaji ya visa vya mapenzi nk hii yote ni kutokana na kuelimika kwetu au wewe unadhani dhumuni la elimu ni lipi?, na unapozungumzia miundombinu unataka kuniambia sisi kusini tumezidiwa na wapi? Na ukija kwenye upande wa uchumi wa mtu mmoja mmoja sisi tuna nafuu kubwa mno kwasababu tunalima korosho zao ambalo hata wewe taarifa zake unazo
 
Mpunguze uchawi na ushirikina
Bahati nzuri huku si kwetu Mimi ni mtu wa Kilimanjaro ila nipo huku mwaka wa 10 sasa uchawi na ushirikina Kila sehemu upo nacho jaribu kutafakari
Kielimu kusini ipo nyuma
Kimiundombinu kusini ipo nyuma
Kiuchumi kusini ipo nyuma
Kimaendeleo basi mtu moja mmoja bado pia ipo nyuma

Serikali na viongozi kiujumla mikoa ya kusini wamechukulia mikoa ya adhabu Kuna kipindi teuzi zikifanyika utasikia utaenda sehemu flani upate kujifunza kidogo hii kasumba iondoke na serikali iweke mpango mkakati wa maendeleo Kwa mikoa ya kusini

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Kanda zote zimesaulika labda Dar na huko kaskazini kuna upendeleo.
 
Mna elimu wakati maendeleo sifuri tukianza kutafuta shule za mwisho kwa Tanzania bara top 10 kusini inaweza toa shule mpaka 6
 
Mna elimu wakati maendeleo sifuri tukianza kutafuta shule za mwisho kwa Tanzania bara top 10 kusini inaweza toa shule mpaka 6
Hapo ndipo unafeli dogo kwahiyo kipimo chako wewe cha elimu ni matokeo ya shule? Mimi watoto wangu wawili na watoto watatu wa dada zangu wapo shule moja inaitwa wenda ipo mbeya huko ndiko wanasoma na hao watoto kwao ni huku kusini je sasa wakishaandika mitihani na matokeo yakatoka watahesabika ni wawapi?na pia kuna shule inaitwa abbey ipo mwena ndanda hapo kuna mchanganyiko wa wanafunzi kutoka mikoa tofauti ya tanzania ila shule ipo mtwara
 
Acha ubishi mzee kusini sio elimu sio miundombinu sio pato la mtummoja moja hali ni tete unabisha nini sasa, elimh nimetoa mfano maana siwezi andika mengi
 
Msimuliaji aliniambia kuwa kumbe wazee wa eneo hilo walifikisha ujumbe kwa wanyapara kuwa mzungu asifanye lolote eneo hilo mpaka tambiko la ruhusa ya miungu lifanyike.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…