Kwanini reli ya Kusini ilisitishwa? Kuna jambo tunafichwa?

Kwanini reli ya Kusini ilisitishwa? Kuna jambo tunafichwa?

Kuna kiongozi mkubwa wa serikali aliwahi kusema" yakuambiwa changanya na yako".
Huyo aliyekusimulia yapo mambo alikuwa sahihi na mengine alikudanganya, kwa makusudi au na yeye kushindwa kuchanganya na zake kama ulivyofanya wewe.
Scheme ya zao la Karanga ilikuwa mkoani Lindi wilaya ya Nachingwea zaidi ya 250 kutoka mjini Mtwara(baharini) na siyo Mikindani iliyopo 0 km kutoka Mtwara/baharini.
Uzalishaji wa zao la Karanga ulifanyika Nachingwea na ulipelekea ujenzi wa reli ya Nachingwea hadi bandarini Mtwara kupitia Masasi kwa minajili ya kusafiri pembejeo na Karanga. Mara baada ya uzalishaji kusuasua/ kusimama reli hii haikuwa na faida tena kiuchumi hivyo ilikufa.
Eneo la Mikindani liko kando ya Bahari na Ardhi yake ni ngumu kiasili na wala siyo kwa sababu za matambiko ya mababu ya kukataa kulima zao la Karanga kama ulivyosimuliwa, kukuongezea uelewa eneo la Mikindani kulilimwa zao la Mkonge. Kuthibitisha maelezo yangu kuhusu Ardhi ya Mikindani na maeneo ya jirani yaani Naumbu na Msijute ni Ardhi ngumu ambayo mwekezaji Dangote amejenga kiwanda cha Saruji na anachimba udongo/ madini ya Jasi kutoka kwenye Ardhi hiyo kama malighafi ya kiwandani.
Natumaini nimesaidia kuliweka sawa hili, kwa kauli ile ile ya yakuambiwa changanya na zako, unayo/ mnayo nafasi pia ya kuyafanyia udhibitisho maelezo yangu.
Ahsante.
Ubarikiwe sana
 
Huoni kuwa umemuanika bibi wa watu bure, je wabaya wakitaka kwenda kumdhuru ili asifunue siri zaidi huoni kuwa we ndiye utamsababishia?
 
Kitu ambacho mpaka leo huwa nashangaa ni kuhusu Straregies yao Ya Groundnut scheme ya Huko kongwa Dc..
Sijui walipata wapi mshauri wa hicho kitu maana Kiliumiza wananchi na bado kinaumiza wananchi mpaka leo na serkari huwa imekaa kimya..

Baada ya panya kuzidi kula karanga sana mashambani Badala ya kuweka dawa wao walibalance ecosystem kwa kuweka mashambani Nyoka wa kutosha ...
walifanikiwa kwa kipindi hicho kwani nyoka walizaliana na Walikula panya hivyo mazao yao yalifanikiwa kuwa Salama....
ila walileta Janga la Nyoka Kongwa..Kongwa kuna nyoka wengi sana ambao Wameletwa Tangu kipindi hicho cha scheme...Ukienda ukasauliza wazee wa huko watakusimulia...
Yah ! Ni biological control system .
Nasikia hayo majoka waliyatoa Australia kuja kuyapandikiza hapo kudeal na tatizo la panya waharibifu
 
Back
Top Bottom