Kwanini reli ya Kusini ilisitishwa? Kuna jambo tunafichwa?

Kuna wakati nafikiria Mwenge wa Uhuru unatugeuza mazombi kiaina
 
Asante kwa kutufahamisha, ila baadhi ya wachangiaji hawaoni umuhimu wa reli hiyo ila kiuhalisia upo

Na upo kwa ajili ya kufika Mbamba Bay na kuunganisha na watu wa Malawi, pia kuchukua makaa ya Mawe , chuma na madini mengine ukiachalia mbali mazao ya kilimo ambayo yapo kule Songea na Mbeya

,haya bado yanahitajika japo mataifa ya Ulaya vitu kama makaa ya mawe wameanza kuacha kuyatumia kisa uharibifu wa mazingira
 
Uishi maisha marefu mkuu
 
Ila watu wa kusini wazushi sana, hata mpaka leo hii, wako hivyo hivyo yaani full kurogana.

Ukichukua mtu wa kusini ukamuweka awe mlinzi kwenye mradi wako wa ujenzi, fahamu kwamba huo ujenzi hutamaliza na hilo eneo lako litageuzwa eneo la ngoma, biashara ya gongo na bangi. Na hata ukiamua kuliuza hutaweza.
 
Kusini uchumi wao tu upo chini upeleke reli utasafirisha nini
Kusini wana kila kitu sema tu dini ndiyo imewarudisha wananchi wa kule nyuma sana. Wengi wao kusoma tu ni issue, hawakutaka kusoma kabisa na mpaka leo hii wapo wapo tu wakijifanya Waarab koko wakati hawana lolote. Mtu ukienda kutaka kuwapelekea maendeleo wanakupinga na kutaka kukusomea albadr.
 
Kuna kiongozi mkubwa wa serikali aliwahi kusema" yakuambiwa changanya na yako".
Huyo aliyekusimulia yapo mambo alikuwa sahihi na mengine alikudanganya, kwa makusudi au na yeye kushindwa kuchanganya na zake kama ulivyofanya wewe.
Scheme ya zao la Karanga ilikuwa mkoani Lindi wilaya ya Nachingwea zaidi ya 250 kutoka mjini Mtwara(baharini) na siyo Mikindani iliyopo 0 km kutoka Mtwara/baharini.
Uzalishaji wa zao la Karanga ulifanyika Nachingwea na ulipelekea ujenzi wa reli ya Nachingwea hadi bandarini Mtwara kupitia Masasi kwa minajili ya kusafiri pembejeo na Karanga. Mara baada ya uzalishaji kusuasua/ kusimama reli hii haikuwa na faida tena kiuchumi hivyo ilikufa.
Eneo la Mikindani liko kando ya Bahari na Ardhi yake ni ngumu kiasili na wala siyo kwa sababu za matambiko ya mababu ya kukataa kulima zao la Karanga kama ulivyosimuliwa, kukuongezea uelewa eneo la Mikindani kulilimwa zao la Mkonge. Kuthibitisha maelezo yangu kuhusu Ardhi ya Mikindani na maeneo ya jirani yaani Naumbu na Msijute ni Ardhi ngumu ambayo mwekezaji Dangote amejenga kiwanda cha Saruji na anachimba udongo/ madini ya Jasi kutoka kwenye Ardhi hiyo kama malighafi ya kiwandani.
Natumaini nimesaidia kuliweka sawa hili, kwa kauli ile ile ya yakuambiwa changanya na zako, unayo/ mnayo nafasi pia ya kuyafanyia udhibitisho maelezo yangu.
Ahsante.
 
Usisikilize maneno ya kuambiwa, fanya Utafiti.
 
Amedanganywa pakubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…