Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria?

Syria ni strategic position! Warusi wana kituo kikubwa sana cha meli za kivita kwenye bahari ya mediterania. Kuishambulia Syria ni sawa na kuishambulia Urusi!! Kwa hiyo warusi wanalinda maslahi yao makubwa Sana huko Syria!! Warusi hawakuwa na maslahi makubwa kivile huko Iraq!.
 
Saddam Hussein kavamia Taifa la Kuweit
Syria ilivamiwa...
 
Mrusi kajitanua sana kwa sasa Afrika kaweka base kubwa sana Sudan inaweza kupokea meli kubwa zote na ndege zote kubwa kushuka na kuruka ktk base yake. Kwaiyo anarudi mdogo mdogo Capitalism ishafail kwa sasa ktk kuongoza dunia na Socialism ambayo imechanganywa na Capitalism kidogo inaelekea kushika hatamu
 

upo sahihi on top of that niongeze kwamba afisa mmoja wa CIA aliyetumwa na marekani kumhoji saddam baada ya kumkamata anadai Bush alikuwa pia na sababu zake binafsi dhidi ya saddam kwamba alidai saddam Hussein alitishia uhai wa Bush sr yani aliahidi kumuua
 
Syria kuna Tartus port wanayoitumia Russian navy kama base yao. Its the shortest way to access the mediterania from the black sea. So Russia lazima waitetee Syria otherwise wataipoteza hii
 
Russia asingeweza kumtetea Sadamu kwa sababu wakati huo alikuwa hoi kiuchumi baada ya Sovieti kuanguka! Hata sasa imemchukua takribani miongo miwili kurudi katika hali yake.
 
Russia asingeweza kumtetea Sadamu kwa sababu wakati huo alikuwa hoi kiuchumi baada ya Sovieti kuanguka! Hata sasa imemchukua takribani miongo miwili kurudi katika hali yake.
Russia alikuwa ana maslahi gani ndani ya Iraq ya Saddam Hussein?
 
Nieleze ninacho kijua kuhusu maada hi.

Kwanza lazima tuelewe hasa historia fupi ya Saadamu Hussein; huyu mwamba alijaribu mara kadhaa kuipundua serikali ya Iraq bila mafanikio, mwishoni mwa miaka ya 60 na miaka kadhaa ya 70; jaribio lake la mwisho lingeweza kupelekea kifo chake, mwamba akakimbilia Misry kujificha; mwaka 1978 kama sikosei, Ayatollah Kamenei na mwenzake Hussein Komeini (sijui kama nimepatia spelling za jina lake, na of course huyu ndio Ayatollah wa kwanza Iran ) waliipindua serikali ya rais Shah wa Iran, rais/serikali hi ya Iran iliopinduliwa, walikua ni marafiki wakubwa wa USA na mataifa ya magharibi; again remember those times (hadi mwaka 1989 ) dunia ilikua imegawanyika pande kuu mbili, either upo upande wa Upepari/Ubeberu unaoimbwa sasa hivi au upande wa Ukoministi, Ubeapari uliongozwa na hawa hawa wababe wa dunia hadi sasa, USA while Ukoministi ulikua unaongozwa na USSR (sasa ni Urusi). Baada ya mapinduzi hayo ya Iran, Marekani na rafiki zake hawakupendezwa sana na utawala mpya, wakaona lazima wapinduliwe na kuondoloewa madarakani; USA wakamkumbuka Saadam aliyejificha Misri, wakampa support ya kuipndua Iraq na kumuweka madarakani but kwa sharti 1, lazima aipindue serikali ya kina Komeini iliokua na misimamo mikali ya kidini, of course pia walitaka rasilimali za Iran kuinufaisha Iran; vita ikawa vita, ilikwenda kwa miaka 8, vita iliisha mwaka 1988 baada ya miamba hi 2 kukaa chini na kupatana wao wenyewe, of course Arabs leage ilichangia sana kuwapatanisha hawa watu; kuna kitu ambacho bado hua sikijui vizuri kwa nyakati zile, Komeini na Kamenei walipindua Iran ya Shah wakitokea Ufaransa, Ufaransa na USA ni marafiki, now why Ufaransa iliwahifadhi watu wale hadi wakajijenga vile huaga sijui hasa. Turudi kwa swali lako why Rassia haikum support Saadamu Hussein, mtazamo wangu uko hivi; kufuatia hayo niliyaeleza kwa maana ya historia, Urusi ni kama iliona USA anamtoa mtu waliyemuweka madarakani wao wenyewe, Saadamu Haaminiki, better him leave the regime.

Nawasoma na wengiene kuongeza ujuzi wa kihistoria
 
Russia asingeweza kumtetea Sadamu kwa sababu wakati huo alikuwa hoi kiuchumi baada ya Sovieti kuanguka! Hata sasa imemchukua takribani miongo miwili kurudi katika hali yake.
Kuwa hoi kiuchumi wala haikuwa sababu
ya kushindwa kumtetea SADDAM, kama wangeamua basi wangemtetea na wala hakuna mtu ambaye angeongea chochote zaidi ya kutukana akiwa kwake.

Mwaka 1999 WARUSI walichukua uwanja wa ndege wa Kosovo kibabe huku majeshi ya NATO yakiwa njiani kwenda kuchukua uwanja wa ndege.baada ya kufika wakawakuta WARUSI washafika zamani sana.ikabidi NATO wawe wapole wageuze majeshi nyuma.

Mwaka 2008 Georgia ilivamiwa na wala hakutokea mtu yoyote yule wa kusema kuwa anasaidia Georgia.sasa mwaka gani ndugu URUSI ilikuwa dhaifu ndugu?
 
haikuwa na ubavu huo! Sasa hivi inajitutumua kwa sababu inajua jeshi la marekani lina vita nyingi sana.
 
Historia uliyota haiko sahihi sana, kuna sehemu ni sahihi na nyingine siyo sahihi. Ingawa ni kweli Shah wa iran alipinduliwa na Ayatollah Khomein mwaka huo wa 1978, lakini wakati wa mapinduzi hayo, tayari Saddam alikuwa ni mkuu wa majeshi ya Iraki na mtu mwenye nguvu sana ndani ya siasa za Iraq. Yeye kuchukua uongozi mwaka 1979, siyo kwamba aliwekwa pale na Marekani baada ya mapinduzi hayo ya Iran bali alipindua uongozi wa Iraki kuzuia mipango ya kuungana na na Syria, ambao ungempunguzia nguvu ndani ya nchi.
 
Sawa mkuu
 
Kama hajaelewa basi ...maslahi maslahi maslahi..
 
Naendelea kujifunza mkuu, twende pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…