Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria?

Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria?

Saddamu alikuwa kibaraka wa marekani,,lakini tatizo ni kuwa iraq ilikuwa inakuja juu na kuwa tishio kwa israel kipindi hicho kuanzia miaka ya 90,iraq ilikuwa na uhusiano mzuri na marekani,lakini ilikuwa haijawa na amani na israel,kwani bado ikiwasaidia wapalestine,
Ilitakiwa ipatikane njia ya kuipunguza speed iraq,kwani ilikuwa ikija vizuri,kiuchumi na kijeshi hivyo kuwa tishio kwa israel,.
Saddam alikuwa na mgogoro na kuwait,,waarabu wenzie walimpiganisha na iran,vita ya miaka 8 na hawakuwa tayari kumu compensate,,saddam akataka kuvamia kuwait,,marekani wakamtega,,kisiri siri wakamoa ok,saddamu avamie kuwait mwaka 1991,first gulf war,
Alipovamia tu,saddamu kashangaa marekani wanamgeuka,
Wakamtwanga,japo hawakutaka kumpindua,,wakamwekea vikwazo ili kuua kabisa speed ya iraq kupiga hatua,,
Vikwazo vikadumu miaka 12,,lakini sardamu akaendelea kutawala,
Ndiposa 2003,likaja swala la WMD,
Hivyo tokea mwanzo,saddamu hakuwa swahiba mkubwa wa Russia.
Hivi bwana elungata kazi ya laser kwenye makombora ni nini?
 
Mkuu, kumbuka kwamba UN Resolution ilipitishwa baada ya ushahidi mzito kuletwa mbele ya baraza la usalama (UNSC) juu ya Saddam Hussein kushambulia wananchi (The Halabja chemical attack)...
We jamaa bhana! Yaani tukio lililotokea 1988 halafu resolution itolewe 2002?! Are you serious?

Kwa kukusaidia, tafuta mwenyewe UN Resolutions #612, #620 zilizokuwa zimetolewa mwaka 1988, na pia unaweza kuongezea #687 ya mwaka 1991. na kwa upande mwingine tafuta UN Resolutions #1441 ya mwaka 2002!

FYI, nchi kama US kwa mfano mwanzoni wao msimamo wao ulikuwa kwamba both Iraq and Iran walitumia chemical weapons against each other. Wakaendelea kudai kwamba wananchi waliouawa (Halabjal) hawakuwa target bali walikuwa at a wrong place at a wrong time kwa sababu waliokuwa wamekusudiwa ni askari wa Iran!!

And remember, kama nilivyosema hapo awali kwamba, Iran-Iraq war Saddam alikuwa anapigana Vita ya US against Iran, that explains why US walikuwa wanajitoa ufahamu!!

Baada ya Saddam kuigeuka US na kupelekea Gulf War in 1991, ndipo mwaka 1998 US wakatengeneza sera kabisaaa ya kuhakikisha wanamuondoa Saddam Hussein madarakani!

Jiongeze mwenyewe kwa kutafuta The Iraq Liberation Act of 1998. Kupitia Act husika, US wakaorodhesha 12 Findings za kuhalalisha kwanini Saddam anatakiwa kuondolewa madarakani, na moja ya hizo findings ni Iraq kutumia chemical weapons kwa raia wa Kikurdi, huku shitaka #1 likiwa Iraq kuivamia Iran mwaka 1980... yaani vita ile ile ambayo US na Maswahibu wake walikuwa wanamsaidia Iraq kumpiga Iran huku 1982 Ronald Reagan akiiondoa Iraq kutoka kwenye list ya nchi zinazounga mkono ugaidi!!

Kufuatia The Iraq Liberation Act of 1998, ndipo US akaanza kutumia ushawishi wake including kuibua tena suala uchunguzi wa WMD dhidi ya Iraq na ndiyo Act iliyozaa UN Resolution #1441 ya mwaka 2002 ambayo pamoja na mambo mengine ilisema Iraq MUST BE DISARMED, na Bush ndo akatumia hiyo fursa ku-implement kwa vitendo The Iraq Liberation Act of 1998.
 
Kwa mawazo yangu Russia ya mwaka 2003,2002, mpaka 2011 ilikuwa dhaifu kiuchumi na kijeshi kushiriki Vita ya nje ya taifa lao. Hebu fikiri miaka ya 98-2000 Russia haikuwa na ndege Vita zilizo tayari kwa Vita ya anga japo kwa asilimia 30. Wangewezaje kupambana? Alipoingia Putin ndo akafanya modernization nzito kuzifanya tu 160,tu 95 nk kua oparational. Lakini wakiwa weak kabisa kuwasaidia wengine.
Huko Iraq wangeendaje?
Hakuna mwaka ambao Russia ilikuwa dhaifu kijeshi ndugu.

*Mwaka 1999 Warusi waliingia kosovo na kuchukua uwanja wa ndege wa kosovo huku majeshi ya Nato nayo yakiwa njiani kwenda kuchukua uwanja wa kosovo.

Majeshi ya Nato yalivyofika karibu na uwanja wa ndege wakakuta tayari Warusi wamechukua uwanja .General wa majeshi ya Nato akamwambia General wa Urusi kuwa vi vizuri mkaondoka na vikosi vyako uwanjani ili kuepusha mtafaruku,General wa Urusi akamwambia General wa Nato kuwa kama mnataka uwanja basi hamna budi kuanzisha vita na Urusi.General wa Nato akapiga simu Kwenye Makao makuu ya Muungano akaeleza kinachoendelea, akaambiwa arudishe majeshi nyuma.

* Mwaka 2008 Warusi walivamia Nchi ya Georgia na kuchukua baadhi ya maeneo ndani ya Georgia.

Sasa ni kipindi gani Warusi walikuwa dhaifu ndugu?
 
*Mwaka 1999 Warusi waliingia kosovo na kuchukua uwanja wa ndege wa kosovo huku majeshi ya Nato nayo yakiwa njiani kwenda kuchukua uwanja wa kosovo.

Majeshi ya Nato yalivyofika karibu na uwanja wa ndege wakakuta tayari Warusi wamechukua uwanja .General wa majeshi ya Nato akamwambia General wa Urusi kuwa vi vizuri mkaondoka na vikosi vyako uwanjani ili kuepusha mtafaruku,General wa Urusi akamwambia General wa Nato kuwa kama mnataka uwanja basi hamna budi kuanzisha vita na Urusi.General wa Nato akapiga simu Kwenye Makao makuu ya Muungano akaeleza kinachoendelea, akaambiwa arudishe majeshi nyuma.
Mkuu, hiki kisa nilikuwa sikifahamu kabisa hapo kabla. Asante sana kwa taarifa...
 
Kulikuwa hakuna sababu yoyote ya russia kumsaidia sadam,
Putin ana akili sana hawezi tu kuingilia mambo yasiyo muhusu ujue sadam alivyokuwa anapigwa aliomba msaada kwa putin kipindi iko jamaa hana hata miaka mitano russia akapiga hesabu zake akaona hafaidiki chochote akamtupilia mbali.

Upande wa syria ni tofauti putin na assad wamesign mkatabata assad kamwachia port nzima ya mediterranean sea putin aweke navy bases zake kwa exchange ya securityover assad. Ukiangalia vizur hapo utaona umuhimuwa hio port kwa russia since its the only warm naval water base in the Mediterranean
 
situation ya Syria ni tofauti na ya Iraq, Iraq alivamiwa moja kwa moja na Marekani wakati Syria nio vikosi vya ndani ya nchi ndio vilikuwa vinamtoa Assad na Marekani kuuunga mkono vikosi hivyo baada ya Russia kuunga mkono vikosi vya serikali, wanaitaga proxy war
 
Sina hakika, lakini nishawahi kusikia kuwa Russia na Syria wana mkataba wa kiulinzi na usalama ambao ulitiwa sahini kipindi cha Baba yake Assad.

Pia kimaslahi, nilisoma sehemu kuwa territory ya Syria kama akichukua kibaraka wa West inaweza kuleta shida kwenye biashara ya mafuta na gasi ya Russia.
Hiyo ndiyo sababu...Syria ikichukuliwa Kuna makampuni yatajenga bomba la gesi kwenda Europe na hivyo kuua biashara ya gesi ya Russia
 
Hivi bwana elungata kazi ya laser kwenye makombora ni nini?
Laser inatumika kana guidance,,kuna makombora yanakuwa na laser guidance,,maana yake likifyatwatuliwa tusema toka katka ndege,,kuna mtu aridhini anakuwa na laser kit ambacho anamulika kuelekea target ilipo,au kuna drone karibu inamulika target,wenyewe wanaita kupaint target,
Hivyo lile kombora litafata ule mwanga wa laser ambao actualy haunekani kwa macho na kwenda kuhit target,
Makombora ya hivyo huwa hayakosi,yanaitwa laser guided missiles
 
Laser designator
7793f993b82e3922aed6ef4d0d249fa8.png
 
Kama miaka mitano tu Rais Magufuli ametupeleka uchumi wa kati je tukimpa miaka kumi mingine itakuwaje?
 
Chadema Siasa za kihuni zimepitwa na muda ombeni msamaha kwa Rais Magufuli.
 
Wazungu huwa siwaamini, kipindi saddam anavamiwa tetesi zilisikika kwamba Russia ataingilia kati kumsaidia saddam, na haikuwa hivyo. Hao mabeberu wanatuzuga tu ila lwao ni moja tu. Tangu lini kuffaar akawa rafiki nasi isipokua kwa maslahi tu! Kwanini China na Russia wasisimame kidete kumsaidia palestina dhidi ya mayahudi kwa unyama wanaoufanyiwa!!! Je ingetokea palestina ndio awafanyie unyama huo wayahudi unadhani nini kingetokea, dunia isingekaa kimya!!

Ni unafiki tu, hawana lolote.
 
kipindi saddam anavamiwa tetesi zilisikika kwamba Russia ataingilia kati kumsaidia saddam, na haikuwa hivyo.
Hizi tetesi zilivuma sana tena kipindi hicho ni mwendo wa Magazeti tu na hakuna social media platforms...
 
Back
Top Bottom