View attachment 3612033
Hakuna ubishi. Masuala mawilli, kuhusu wabara kuondolewa au hata kutotibiwa visiwani na kutangaza siku ya mwaka wa kiislam kuwa mapumziko ni chembe chembe, chokochoko, na viashilia vya kuuvunja muungano.
Wengi wameandika juu ya upuuzi huu na kulaumu. Ajabu, rais wa muungano yuko kimya!
Je, ameridhika na haya hadi kuyaunga mkono na kuyanyamazia?
Je, ni sehemu ya mkakati huu usio wa kikatiba wala kisheria?
Je, Mwinyi amepata wapi haya mamlaka au wawili wamekubaliana kama siyo mmoja kupoka na kupora mamlaka ya mwenzake?
Je, mhusika mkuu hana uwezo kiakili kulishughulikia balaa hili la kujitakia?
Je, kuna namna anavyofaidika nalo?
Je, ni tukio la bahati mbaya au la makusudi lenye malengo makubwa kulko tunayoona?
Je, wahusika wameuchoka muungano au ni ulevi wa madaraka na kujisahau kuwa wao ndiyo wanufaika wakuu?
Je, nini kifanyike kuwawajibisha wawili hawa?