Kwanini sensa ya watu na hii ya majengo hazikufanywa sambamba?

Hii nchi viongozi wetu wanatuona sie wananchi wao kama misukule vile
 
Hii sensa ya majengo ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Walishindwa vipi kuijumuisha wakati wanahesabu watu. Nini lengo la hii sensa ya nyumba? Wana lengo la kuongeza kodi, kutujengea nyumba au nini?

Hiyo pesa wanayotupa huko wangeipeleka sehemu nyingine ikafanye maendeleo. Maana hakuna jipya litakalofanyika zaidi ya kuongezewa tozo kwenye vifaa vya ujenzi.

Kupangilia miji mmeshindwa lakini kuhesabu nyumba mnataka ili muanzishe tozo zenu.
 
Nimeshangaa Leo kamisaa wa sensa karudi home anaulizia jengo Tu kwani alishindwa Nini kuuliza Ile siku ya sensa ya watu ni upigaji tu
 
Kwani kazi ya anuani za makazi haikuwa ikichukua taarifa (takwimu)za majengo maana ilikuwa ikiuliza hli ya jengo, either ni
1. Msingi
2.Boma
3. Gofu
4. Jengo kamili
Sasa inakuwaje wanafanya tena hesabu ya majengo?
 
Nchi imejaa walalamikaji hii Yani Kila kitu kulalamika ebu tuacha taaluma za watu zifanye kazi wanajua kwanini havikufanyika pamoja
 
Huenda wametumwa na beberu wakusanye kila aina ya taarifa zinazohusu watu kwa ajili ya maandalizi ya utawala wa yule mpinga Kristo, time will tell...
 
Hii inamaanisha, wakujue kwanza, halafu wajue kwa kukupata iwe rahisi kukutoza kodi.

Na ile ya Mheshimiwa Nape ya kupita na helicopter huko juu kwani haikusaidia?

Hii nchi wasomi ndo wanatuangusha, wanafeli kuishauri Government.

Hao makarani wasikopwe, walipwe haki zao, ikibidi waongezwe posho.
 
Nchi imejaa walalamikaji hii Yani Kila kitu kulalamika ebu tuacha taaluma za watu zifanye kazi wanajua kwanini havikufanyika pamoja

Wadhani hii nchi imewahI kupungukiwa chawa kama wewe mkuu? Ndiyo mliotufikisha hapa tulipo. Hohehahe hakuna mbele wala nyuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…