Kwanini sensa ya watu na hii ya majengo hazikufanywa sambamba?

Kwanini sensa ya watu na hii ya majengo hazikufanywa sambamba?

Tumeambiwa zaidi ya 600bn/- zimetumika kwenye sensa tuliyoambiwa ni ya watu na makazi. Tungali tunajitafakari wanakuja na jipya:

Hili nalo ni zoezi la bilioni ngapi? Hivi makazi na majengo nini tofauti?

kwanini mawili haya kama ni tofauti na kama ni muhimu hayakuunganishwa ili kufanywa pamoja kupunguza gharama zake za utekelezaji?

Au ni kwa vile kuna tozo zisizokuwa na idadi ziko njiani? Si mtakamua hadi mafahali mkitegemea maziwa?

View attachment 2339509
!!!Et walipi kuweka vibao na kuandika namba kwenye nyumba .Sasa?
 
Moja ya maswali Niliulizwa nyumba Yako inavyumba vingapi vya kulala,namba ya anuani ya makazi ya nyumba,jina la barabara nyumba Yako ilipo,nyumba Yako Ina hati?umepanga au unamiliki eneo hili?na kama unamiliki mnamiliki wengi au peke Yako,Je eneo la nyumba Yako linatumika kwa kilimo au ufugaji?nyumba Yako inavigae au sakafu ya simenti?nyumba ni ya tofali?imeezekwa Kwa Nini? Maswali haya ni ya Nini kama sio sensa ya makazi
 
Kunaandikwa Mwananchi:

"Wakati wananchi wanaandikishwa kwa ajili ya sensa, wengine wanaandikisha wakulima kwa ajili ya kupata mbolea ya ruzuku huku kukiwa na kampeni inayowataka wapangaji kulipa asilimia 10 ya kodi wanayotozwa na wamiliki wa nyumba."

Vikwazo tele sensa mikoani

Mambo lukumba lukumba.
Leo nimepitiwa kwenye sensa ya makazi nimeulizwa jina la.mwenye nyumba, vyumba vingapi vya kula nk. Mwisho nimeulizwa namba ya mita ya LUKU hapo hapo nikapata jibu tozo nyingine inakuja si muda mrefu
 
Back
Top Bottom