Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Mimi jengo langu mpaka sasa nimetumia zaidi ya milioni 70! Ila kiukweli nitawaambia nimetumia kiasi kisichozidi milioni 40.Tumeambiwa zaidi ya 600bn/- zimetumika kwenye sensa tuliyoambiwa ni ya watu na makazi. Tungali tunajitafakari wanakuja na jipya:
Hili nalo ni zoezi la bilioni ngapi? Hivi makazi na majengo nini tofauti?
kwanini mawili haya kama ni tofauti na kama ni muhimu hayakuunganishwa ili kufanywa pamoja kupunguza gharama zake za utekelezaji?
Au ni kwa vile kuna tozo zisizokuwa na idadi ziko njiani? Si mtakamua hadi mafahali mkitegemea maziwa?
View attachment 2339509
Maana tayari nafahamu mnachokitafuta. Mateso nipate mimi, halafu mnataka tugawane pasu kwa pasu. Hovyo kabisa.