Kwanini serikali imebariki magari ya viongozi wa serikali kuwa namba feki? Mwanzo nilizani ni uhuni wa madereva kumbe wanapewa wabandike feki

Ni vile hamjui kuwa magaidi huogopa kufanyiwa ugaidi
 
Pokeeni ushauri,acheni kuona ninyi ni vichwa,panapohitaji mabadiriko fanyeni mabadiriko.

Kwani magari ya serikali yakipokelewa yakapewa namba za serikali moja kwa moja kuna shida gani?
kama issue ni kutaka kujua nchi imeingiza au ina magari mangapi ni kuchukua idadi ya yanayomilikiwa na serikali ukaongeza uliyoyasajiri kwa namba za kawaida.
Ila kama ni ule mfumo wa mbuzi kula kwa kamba yake hapo nitaelewa,lakini kusema hili lipo kwa manufaa ya nchi nakataa mpaka kesho.
 
Watakuambia acha unoko. Unafikiri watafanya vipi mambo yao ya chobingo.
 

Kama ni mzoefu barabarani, hebu jiulize ni kwanini hao madereva wa magari ya serikali huwa hawaheshimu sheria. unakuta kuna foleni , taa zimewaka yeye anakuja anakatiza. Cha kushangaza traffic wala hawachukui hatua. Yaani ni kwamba jamaa wana sheria zao tofauti na raia.
Mimi ningekuwa Rais, yaani kuongozi, waziri ambaye gari yake inakiuka sheria za bara barani na yeye yumo ndani, basi hana kazi.
Hii iko mpaka kwa magari ya majaji wetu ambao ndio husimamia sheria, acha wabunge na mawaziri.
Yaani ni nuchafu mtupu.
Akikugonga au kufanya kosa lolote ana badirisha namba hujui ni nani.
 
Huw
1. Kwahiyo ukibadilisha plate namba unaruhusiwa kubaki na ya zaman ikiwa inasoma usajili?
2. Kwanini magari ya serikali yakipigwa mnada ukilinunua unapewa usajili mpya namba mpya?
Huwezi kupewa namba ile ya mwanzo... coz usajili wake ni wa kiserikali. Lazma tujue kila gari la serikali husajiliwa kwa namba mbili purposely
 
Huw

Huwezi kupewa namba ile ya mwanzo... coz usajili wake ni wa kiserikali. Lazma tujue kila gari la serikali husajiliwa kwa namba mbili purposely
Kwann namba hizo feki ukiangalia kwrnye usajili zinasoma majina ya watu binafsi ambao ni feki, yaani namba iko kwenye landcruser usajili unasoma toyota CAMI?
 
Shangaa
 
Kweli. Likitokea tatizo mfano ajali, tutaanzia wapi kureport.

Kuna watu wanajiona miungu watu, bila huruma wala nn wanabandika kwa clippers flani izo number plate.

Usalama wa viongozi na mali za Serikali unalindwa na watu maalum.

Siyo lazima kujua kiongozi kapanda gari ipi, na siyo kazi ya kila mtu bali watu maalum.
 
Ndio umejibu nini ? STL na etc maana yake nini kwanzi pale inapoanza kutuma
 
Hichi kitu sio sahihi, ni uongo kwa 100%.
Kila gari (haijarishi ya binafsi, jeshi, serikali) huwa na usajiri wa namba moja tu katika wakati mmoja, gari moja haiwezi na haipaswi kuwa na namba mbili za usajiri kwa wakati mmoja.

Kama gari ilikuwa ya serikali halafu umiliki ukahamia binafsi, ile namba ya awali ya usajiri ya serikali hufa ili kuzaliwa namba mpya ya binafsi, na haitafufuka tena. Vice versa ni sawa.

Kinachoweza kubadilika katika gari za serikali ni vibao vya utambulisho ili kuficha vibao vya namba husika. Kwa mfano gari yoyote ya serikali inaweza kutolewa kibao cha namba ya asili (mfano STH 892) ili kuwekwa kibao chenye utambulisho wa ufupisho kwa viongozi wa juu mfano waziri, naibu waziri, makamu wa rais, waziri mkuu nk. Na wahusika wakiwa hawajabebwa kwenye hayo magari na hayo magari kwenda kutumika kwa shughuli zingine vibao vya utambulisho wa viongozi hung'olewa na namba halisi (asili) za serikali (STK, STJ, STH) kwa gari husika hurejeshwa. Lakini kamwe hauruhusiwi gari ya serikali kuwekwa namba binafsi. Ni uhalifu. Ni mchezo mchafu umeanza kuzoeleka katika jamii yetu. Haipaswi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…