Kwanini serikali imebariki magari ya viongozi wa serikali kuwa namba feki? Mwanzo nilizani ni uhuni wa madereva kumbe wanapewa wabandike feki

Sio kweli..
Gari za Serikali husajiliwa direct kwa namba za Serikali (ST) kwa Serikali Kuu, (SM) kwa Local Gvt, (SU) kwa mashirika ya Umma, yale ya majeshi (JW, UT, PT, MT) na (DFP) kwa miradi/NGO zenye ubia na Serikali. Hakuna double registration. Hizo namba za kiraia zinapachikwa tu kuficha Identity kwa sababu maalum. Hata zile za W, NW, S nk.. zinakuwa ni ST then zinabatizwa tu pale zinapowabeba viongozi hao.
 
Asante sana kwa maelezo yaliyonyoooka sana!
Sasa hili jambo polisi wa usalama barabarani mbona wamelifumbia macho?

Kamanda wa usalama barabarani bara na visiwani mbona hasemi chochote? Nani aliyebariki huo uharifu kuwa halali kila dereva kuwa na namba mbilimbili za mchongo
 
Je zote zinatakiwa kutumika, au ikishanunuliwa na Serikali, ile ya usajili wa mwanzo hufa?
 
Ungekuwa Mshauri wa Masuala ya Usalama kwa Viongozi wa Taifa unadhani hili ni sawa ama si sawa? Kwa upande wa mtazamo fulani unaona ni kitu kibaya lakini kwa upande wa mtazamo wa Nje hii ni SALAMA zaidi. Uwe na uhakika hata hapo kitaani kwako Baadhi ya gari zinazokuwa kwenye msafara wa viongozi wa kitaifa pengine zinapitaga na kupaki sana. Ila tuu huwezi zingatia kwa wakati huo kutokana na kubadilishiwa Number Plate.
 
Aliyekwambia viongozi hawako salama.nani? Ujuaji tu
 
Unataka wakitoka kugawana mikopo uwakabe? Utakesha barabarani.
 
Aliyekwambia viongozi hawako salama.nani? Ujuaji tu
NIlishawahi kuona Magari matatu maeneo ya Mbande ambayo yanatumika kwenye msafara wa Rais yakiwa njiani kurejea Dsm. Lakini kwa wakati huo yalikuwa na Number Plates za kiraia na zilikuwa mwendo wa kawaida. Kiasi kwamba si rahisi mtu kuzizingatia na hii husaidia kuepusha njama ovu pindi yakiwa hayajabeba viongozi.
 
Hili jambo liliwahi kuongelewa na Magufuli wakati akiwa waziri wa ujenzi baada ya taasisi fulani fulani kuamua kusajili kwa namba binafsi(za kiraia) ndipo akaamuru gari zote za serikali lazima kwanza zisajiliwe kwa namba za serikali na baada ya hapo ndipo zile taasisi zinazohitaji kuficha utambulisho wa magari yao ili kurahisisha utendaji kazi/shughuli zao wanaweza kusajili namba za kiraia lakini namba halisi zinakuwa ni zile za serikali.
 
Ujuaji mwingi usiokuwa na tija
 
Gari za viongozi si rahisi kukosa pesa.
 
Nimeambua kitu hapa
 
Yanatumika pia Kutekea Wakosoaji
 
Angalieni hii ng'ombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…