Kwanini Serikali inaacha uvumi unaondelea kwenye mitandao uendelee?

Tatizo, ni mkwara wa Yohana siku ile alipo ongea na kutoa PS imewatisha wahusika wote. Imagine mpaka Paulo kauchuna.

Kitendo cha kushindwa kutoa data kwa week ya pili sasa sijui kina lengo gani hasa.
 
Hiyo mitandao Insta na Twitter, siyo mali ya serikali...
Kwahiyo wewe hapo ni za kwako uchanganye na za kwao, huku ukijifukiza, ukinawa kwa sabuni na maji tiririka na kuvaa barakoa..

Everyday is Saturday........................ 😎
 
Kwanza mtasema uvumi baadae itathibitishwa itajaribu kufichwa mwisho wataachia tu tutaongea kitu kimoja halafu tushirikiane kuwaambia wajiuzulu
Mnaombea mabaya yawafikishe Ikulu, mna laana. Huu ni wakati wa kuhamasishana kuzingatia ushauri kuhusu kinga na kukemea wasio fanya hivyo.

Haya tukubali taarifa hizo ni za kweli, watu wakifa ninyi mnaendelea kushangilia na kulaumu, mtamtawala nani. "Hopeless" kwa fikra za kitoto.
 
Ile Kasi ya uvaaji barakoa imeishia kabisa sikuhizi maeneo ya Kariakoo watu wanajiachia Tu kama kawaida...
Wizara ijitahidi kusisitiza uvaaji barakoa
 
Ndugu yangu hata kama kusoma hujui picha nayo huelewi? Unataka serikali ifanye nini wakati asilimia 90 ya yanayosemwa ni ukweli? Hivi wewe huaminiki kuwa watu wanafariki kwa hawa virus kila uchao? Wiki iliyopita niliambiwa na mtu anayeaminika kuwa jijini Dar kila siku usiku wanazikwa watu si pungufu ya 10. Wiki hii zimeanza kujitokeza clips nyingi za mazishi ya usiku. Na kadiri siku zinavyokwenda ndiyo hali inazidi kuwa mbaya. Huu ugonjwa una tabia moja. Unapoingia kwenye nchi, huingia kwa ukimya sana, na hatua ya kwanza ni kusambaa. Ukishasambaa ndiyo unaanza kusababisha vifo.
 
Daa yule Mzee amefariki?? Poleni wafiwa hasa Naushad na Mdogo wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Ummy si alisema vile kwamba "sasa tumeamua kusema ukweli".
 
Sasa kama huamini video unataka upewe kitu gani ndio uamini ?

Serikali imekataa kutoa taarifa, ngoja hao wawili wazibe hiyo VOID .
 
Mimi nafikiri watawala Bado wanazani tupo Zama za ujima/ enzi za Nyerere kwamba watu hawatafakari. Watambue technology imebadili Mambo leo mtu anaanguka Arusha ndani ya dk 10 Nchi nzima inajua!!!, Watawala waache Mambo haya kuiga ili kuponya watu sio dhambi, hatuwezi kuiga tu kutumia vyombo vya dola kuwadhibiti wapinzani kisiasa tutashindwa kuiga namna yakuwaokoa Raia.
 
Kama unafikiri kuwa una sirikali wewe ni mjinga! Umeshanyang'anywa haki yako tayari ya kuishi kupitia herd immunity ila hata hujui, upo upo tu
 
Kuna ushuhuda wa njiro nimeusikia now bbc dira ya dunia ulichanganya na hao kuna mahali si sawa
Mkuu wa wilaya nako uvumi unaendelea watu wanamashaka walikuwa nao hivi karibuni

Serikali hii inakwenda kujivuruga
 
Kuna jaji mstaafu nae kafa nasikia alikuwa anaumwa kwa muda mrefu, je ikiwa sio korona unatahani atazikwa na watu wengi?

Inategemea kama alikuwa na Corona au hakuwa nayo. Mama wa best friend wangu kazikwa Dodoma kijijini na watu wengi tu na hawakupewa masharti
 
Failure in leadership, per excellence! Haijapata kutokea!

Nadhani kuna hujuma pia, hii sio bure! Inawezekana watu wamechoka, wameamua kuliacha liende kivyovyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…