Kwanini Serikali inawabagua walimu wenye shahada kwenye ajira?

Huyu wa diploma hana mkato ya NHIF na cwt?
 
Mshahara wa mwalimu wa degree unazidi kiasi ulichokitaja.
Sio kweli mkuu labda kama unazungumzia basic salary. Take home ya mwl degree holder ni laki nne na points. Baada ya serikali kushusha paye ndo angalau wanachukua kilaki tano lakini bado hiachani sana na mshahara wa mwl mwenye diploma..
 
Sio kweli mkuu labda kama unazungumzia basic salary. Take home ya mwl degree holder ni laki nne na points. Baada ya serikali kushusha paye ndo angalau wanachukua kilaki tano lakini bado hiachani sana na mshahara wa mwl mwenye diploma..
Unapozungumzia mshahara wa mtu unakuwa unazungumzia basic salary na siyo take home. Take home inategemea kati ya mtu na mtu kadiri ya makato yake na madeni aliyo nayo. Hata hivyo,basic salary inazidi 720,000/= uliyoitaja wewe.
 
Mkuu mbona unapinga ilikhali hujui kile unachopinga? Mshahara Wa Mwalimu Wa degree anayeanza kaxi kwa sasa ni D1 ambao ni almost 716,00O wakati huo D2 ni almost 740,000 na kuendelea,au unataka nikuwekee salary slip hapa ndo uamini?
Bado haupo sahihi Mkuu! Siyo vizuri kubahatisha mambo. Weka hiyo salary slip niione.
 
Mkuu, mwl mwenye degree anaandaliwa kufundisha wanafunzi wa ngazi zote kuanzia O'level, advance na vyuo vya kati kwahiyo kusema wanatakiwa kufundisha Advance tu sio kweli ni uongo na upotoshaji.
 
We we utakuwa na lako jamboView attachment 1663945
Nadhani Sasa umekubaliana na Mimi kuwa haukuwa sahihi. Maana kiasi unachokiona hapo,ambacho ni D2 kwa huyo muhusika, ndicho kitakachokuwa D1 kwa mwajiriwa mpya.

Nikukumbushe tu kuwa wewe ulisema kwamba, mashahara hauzidi 720,000/= wakati hapo Kuna 733,000/=. Wakati mwingine kuwa makini Mkuu, hata hivyo nakutakia heri ya mwaka mpya Mwalimu, au rafiki wa Mwalimu.
 
Acha ubishi wewe , mshahara Wa D1 ni 7160,000 ukikataa naweka hapa salary slip,I think your are not fine in your head
 
mshahara

Sent from my itel A11 using JamiiForums mobile app
 
Kwani hiyo mikopo wameambiwa walipe kabla ya kupata Ajira ?
 
Walimu wa arts hawahitajiki
 
Kitu ambacho hamjakigusa.
Sababu inaweza kuwa namna walimu hawa wanavyoandaliwa.

Namna wanavyoandaliwa walimu ngazi ya cheti na stashahada ni sawa. Lakini kwa ngazi ya shahada kuna utofauti mkubwa.
 
sio kweli mwajiriwa mpya ananza na D1

hata mwl aliyepandishwa daraja kutoka C kwenda D, anaanza na D1 sio D2

kisheria kila baada ya mwaka 1 mtumishi anatakiwa atoke grade moja ya ngazi aliyonayo kama hajafikia sifa za kutoka ngazi moja ya mshahara kwenda nyingine mfano tgtsc»»»Tgtsd

grade ni hizi c1,c2.... au D1, D2.....

mfano mtumishi kama yupo D1 baada ya mwaka1 anatakiwa awe D2
 
Serikali sasa hivi haitaki watu wenye madegree wanaipa hasara kwa mchanganuo ufuatao.

Graduate degree- ina muajiri kwa mshahara mkubwa halafu anaenda kufanya kazi bila experience then inamlipa mshahara mkubwa .

Diploma holder- anaajiliwa kwa mshahara wa kawaida anaenda kufanya kazi bila experience kwa mshahara wa kawaida then ana gain taratibu na kuweza kuperfom hata majukumu ya graduate kwa kama miaka mitatu hivi anakuwa na experience ya kutosha halafu serikali ina mshawishi akajiendeleze kwa pesa yake mwenyewe anaenda anasoma anarudi haihitaki tena experiences hapo anabadilishwa daraja na mshahara.

Swali. Nani anaepata hasara kati ya mwajili na mwajiliwa?
 
Kitu ambacho hamjakigusa.
Sababu inaweza kuwa namna walimu hawa wanavyoandaliwa.

Namna wanavyoandaliwa walimu ngazi ya cheti na stashahada ni sawa. Lakini kwa ngazi ya shahada kuna utofauti mkubwa.
Kwamba walimu wenye shahada hawaandaliwi vema au unataka kumaanisha nini hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…