Kwanini Serikali inawabagua walimu wenye shahada kwenye ajira?

Kwanini Serikali inawabagua walimu wenye shahada kwenye ajira?

Hii hali inakatisha tamaa hata kuomba ajira! Labda kwakuwa utawala umebadilika ngoja tuone mama Atakuja na yapi!
 
Umepotosha mkuu,tofauti ya mshahara kwa Mwalimu Wa diploma na degree ni almost 190,000 kwa uwiano Wa daraja C na D sasa hio ya walimu watano Wa degree kiajili walimu 50 Wa diploma na Cheti inatoka wapi?

Maana hata Mwalimu Wa degree mmoja kwa mshahara wake hawezi kuajiri walimu wawili,maana mwalimu Wa Cheti anaanza na daraja B amabalo linamshahara Wa 400,000+ ,wakati mwalimu Wa degree ananza na mshahara usiozidi 720,000
Upo sahihi Mkuu.
 
Jibu lako ni hili hapa.

Walimu hao wenye degree ni wachache ukilinganisha na wenye certificate na ndio maana katika kuajiri utaona wao wachache kwa idadi ila kwenye ratio ni sawasawa tu...

Watu wanabwabwaja tu.
Mmhhh!!!, Sidhani
 
Kuendelea kusubili ajira za ualimu wa sanaa utasononeka Sana....

Ndio maana nikasema kweny maisha Kuna muda assume kuanza upya....

Assume means: to think that something is true or probably true without knowing that it is true......

Nili ahidi Mwaka huu 2021 inshallah....mwishoni ntakamilisha ahadi yangu ya kuwa andalia VIJANA.... motivational speech.
Unatugeuza fursa sasa

Tumepigwa na govt. na sasa unakuja na motivation speech zako

Mtuache jamani
 
Unatugeuza fursa sasa

Tumepigwa na govt. na sasa unakuja na motivation speech zako

Mtuache jamani
Mkuu BADO naendelea kuwaandalia.....chakula ya ubongo nyinyi vijana....

Kikubwa ni kuwapa experience jinsi unavyo weza na mimi nilivyo weza ku climb all the mountains & kicking the ODDS in my life.....
 
Unatugeuza fursa sasa

Tumepigwa na govt. na sasa unakuja na motivation speech zako

Mtuache jamani
Anaboa na hizo speech zake na usikute ni mwajiriwa wa serikali lakini kwakuwa yupo nyuma ya ID fake ana bwata kinoma
 
Sio kivileeeee!!!![emoji23][emoji23]
Kimsingi walimu wanatakiwa kuwa na degree, hao wenye certificate na diploma ni walimu wasaidizi na hii haijalishi shule ya msingi au sekondari.....sasa serikali badala ya kuajiri walimu, inakomaa kujaza walimu wasaidizi ili kukwepa kulipa mishahara mikubwa, jambo ambalo linadidimiza elimu...
 
Haya yalisababishwa na mwendazake lakini kikwete hadi anatoka madarakani aliacha akiwa ameweka mfumo mzuri wa kuajiri walimu wote bila ubaguzi wa kielimu au upendeleo
 
Kimsingi walimu wanatakiwa kuwa na degree, hao wenye certificate na diploma ni walimu wasaidizi na hii haijalishi shule ya msingi au sekondari.....sasa serikali badala ya kuajiri walimu, inakomaa kujaza walimu wasaidizi ili kukwepa kulipa mishahara mikubwa, jambo ambalo linadidimiza elimu...
Elimu yetu inahitaji mageuzi makubwa sana ili kuzalisha wataalam watakao tumia usomi wao kuendeleza miradi mikubwa ya nchi na kutumia raslimali zetu wenyewe badala ya kuzitapanya kwenda nje ya nchi. lakini yote haya yatabaki kuwa ndoto kama tutaendelea kukumbatia elimu na ualimu wa cheti ambao kimsingi hautambuliki duniani
 
Kimsingi walimu wanatakiwa kuwa na degree, hao wenye certificate na diploma ni walimu wasaidizi na hii haijalishi shule ya msingi au sekondari.....sasa serikali badala ya kuajiri walimu, inakomaa kujaza walimu wasaidizi ili kukwepa kulipa mishahara mikubwa, jambo ambalo linadidimiza elimu...
Sina hakika km unachokisema Kina ukweli kwasababu nimeshuhudia mara kadhaa uwezo wa Walimu ngazi ya Diploma na Cheti kuwa mkubwa kuliko wa degree sasa sijui hilo unalizungumziaje?
 
Sina hakika km unachokisema Kina ukweli kwasababu nimeshuhudia mara kadhaa uwezo wa Walimu ngazi ya Diploma na Cheti kuwa mkubwa kuliko wa degree sasa sijui hilo unalizungumziaje?
Uwezo mkubwa upi unaoongelea, huo uwezo mkubwa ni kwenye ngazi yao ya elimu......vinginevyo degree, Masters na PhD zingeondolewa kwa sababu wenye certificate tayari wana uwezo mkubwa, acha kujifariji nenda shule...
 
Mimi sio mwalimu
 
Kuna kitu hakipo sawa kwenye ajira za walimu.

Kwenye kila kibali cha ajira kinachotoka idadi ya walimu wenye shahada wapatao fursa ya kuajiriwa serikalini huwa ni ndogo sana kulinganisha na walimu wa ngazi zingine za kielimu kama vile cheti na diploma.

Kielelezo kizuri ni ajira zilizotoka juzi ukizichunguza kwa makini utakubaliana na hiki ninachokisema.

Kwani katika hizo ajira, wenye shahada walioajiriwa hawafiki hata robo ya waajiriwa wote(wapo chini ya 1500 kati ya 8000).

Tukumbuke asilimia kubwa ya walimu hawa wamesomeshwa na serikali hivyo wanadaiwa na bodi ya mikopo(HESLB). Lakini cha kushangaza serikali ni kama inatoa kipaumbele kidogo kwa wao kuajiriwa.

Je, ni kipi hasa kinafanya walimu hao waajiriwe kwa uchache kuliko walimu wengine?

Je, watalipaje madeni yao ya mikopo kama serikali itaendelea kuwaacha mitaani?
Serikali haitaki wasomi wazuri,Ili msiende kuwasumbua viongozi.
Inataka vilaza wenye Elimu ya kuunga unga,Ili iwaperekeshe kama bendela,
 
Back
Top Bottom