Kwanini sharti mojawapo la kujiunga na Jeshi ni pamoja na kutokuwa na kovu mwilini?

Kwanini sharti mojawapo la kujiunga na Jeshi ni pamoja na kutokuwa na kovu mwilini?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Inaelezwa kuwa shariti mojawapo la mtu kuruhusiwa kujiunga na Jeshi la Wananchi ni kutokuwa na kovu mwilini na nasikia watu hulazimika kukaguliwa mwili mzima kuthibitisha kuwa hawana kovu/makovu katika mbili yao.

Nachotaka kujua kutoka kwa wanaojua,sababu ya kukataa wenye makofu ni nini?

Mliopita Jeshi la Kujenga Taifa na nyie hamuelewi?

Na je,mtu alisha jiunga na Jeshi,hawezi pata kovu?Na akipata,anakuwa na athari gani kwa Jeshi?

Na je,ni kweli hata wanaojiriwa katika mradi wa ujenzi wa SGR nao nao hatakiwi kuwa na maovu katika mbili yao?

Kama ni kweli,sababu ni nini?

Mwenye kujua naomba atusaidie.
 
Inaelezwa kuwa shariti mojawapo la mtu kuruhusiwa kujiunga na Jeshi la Wananchi ni kutokuwa na kovu mwilini na nasikia watu hulazimika kukaguliwa mwili mzima kuthibitisha kuwa hawana kovu/makovu katika mbili yao..
wanakuja
 
Kwa uelewa wangu, si kila kovu bali ni baadhi ya makovu ambayo katika utabibu ni vigumu mtu huyo au sehemu hiyo kushoneka.
Makovu yatokanayo na kuungua kwa ngozi( inaweza kua moto au tindikali) ni vigumu mtu mwenye makovu aina hii kuhudumiwa pindi apatapo majeraha ukiringanisha na mtu asiye na makovu au kovu.
Si kovu tu wanaangalia ukubwa wa kovu. Kuna askari na wanajeshi wengi tu wenye makovu.
 
Angalau unatupa mwanga.Nakushukuru.
 
Hawataki mwenye makovu makubwa hasa sehemu za miguuni, na makovu makubwa mengine, pia jua jeshi haliajiri mlemavu.

Hivyo ukiwa na kovu, linalokupelekea kuonekana mlemavu, kama walivyokua wameunguzwa wale wa ajari ya moto moro, huajiriwi.
 
Back
Top Bottom