Kovu - ishara ya mwili wako kuwa sio fit kwa mazoezi makali jeshini, na hawataki itokee ati kovu limefunguka tena ukiwa training, itakuwa lost of time kwako na pia kwao watatakiwa wakutibu hadi upone, wakati wenzako wenye mko group moja wanaendelea na mazoezi, wewe uko nyuma. Hilo instructors hawali mind. Tena ukumbuke, ukiwa jeshini na bahati mbaya upate jiraha litakalo kufanya kutoendelea na kazi yako, lazma uwe discharged na ulipwe na serikali, kwa mujibu wa sheria za kijeshi, sababu uliumia ukiwa cadet sio raia. Ndio maana hawataki uwe na kovu lolote kubwa alafu iwe mseo baadaye, iwe mambo ya kotini tena, wataka kulipwa ilhali ulikuwa na jeraha kabla hujaingia mazoezini.
Tatoo - upande huu wa michoro ya kwenye miili, huwa naona ni hapa Afrika tu ndio tuna huo utopolo bado. Uwe una tatoo, uwe huna, ukiingia jeshi tu, nidhamu utakuwa nayo, upende usipende. Neno 'ME' litakutoka kwenye mazungumzo yako, utakuwa unasema 'WE', kumaanisha nyote hapo kambini ni madungu kuanzia hiyo siku hadi utakapo iacha dunia, ubinafsi umeuacha uraiani. So hii issue ati mtu kuwa na tatoo hana nidhamu, huwa fikra zetu bado sizielewi. Nafkiri wengi wenyu mnajua nchi zilizoendelea sana, kando na Waarabu, hawaulizi story na tatoo, uwe nayo mwili mzima au la, hawajali, bora wewe ufaulu training na uwe sharp kwa kile unachofundishwa iwe practical ama theoretical. Mfano ;mwanajeshi wa Ufaransa, Amerika, ujerami, Swiss nk vijana wanaojiunga jeshi wamechafuka tatoo vibaya sana lakini hilo sio pingamizi, uwe mrefu uwe mfupi, hilo hawajali, uwe mvaa miwani, dogo unaingia. Sasa angalia mafunzo yao na yetu huku, vita vyao na vyetu, elimu ya jeshini ya kwa na kwetu. Wana 'nidhamu' kutushinda 😂😂😂
Hitimisho - Sheria nyingi za utopolo jeshini, ata kwenye askari polisi, huwa tumezitunga wenyewe ili kupunguza raia wengi kuingia kazi hiyo, lakini ukweli ni nyingi huwa hazisaidii kuongeza wala kupunguza capabilities za mwanafunzi wa jeshini.
Bora uwe physically fit na akili ya u chap chap basi huwa uko sawa tu na usiwe mgonjwa😂
✌️