Kwanini sharti mojawapo la kujiunga na Jeshi ni pamoja na kutokuwa na kovu mwilini?

Kwanini sharti mojawapo la kujiunga na Jeshi ni pamoja na kutokuwa na kovu mwilini?

Wengi mnachangia kwa kukisia tu, hizo hisia tayari tushazisikia mtaani... hoja ijibiwe kijeshi.

Je, ukipata kovu ukiwa kazini utaachishwa?
 
mbona ukiwa na tatoo pia huruhusiwi kujiunga na jeshi?
Hawataki mwenye makovu makubwa hasa sehemu za miguuni, na makovu makubwa mengine, pia jua jeshi haliajiri mlemavu.

Hivyo ukiwa na kovu, linalokupelekea kuonekana mlemavu, kama walivyokua wameunguzwa wale wa ajari ya moto moro, huajiriwi.
 
Inategemea na aina ya makovu mkuu..wanahofia katika mazoezi yao kovu linaweza likasababisha kidonda tena...

Sasa wewe unashangaa kovu...hata ukiwa unanyanyua vyuma (kupiga nondo) jeshini hauajiriwi..
 
Wengi mnachangia kwa kukisia tu, hizo hisia tayari tushazisikia mtaani... hoja ijibiwe kijeshi.

Je, ukipata kovu ukiwa kazini utaachishwa?
Inategemea na mafunzo ya aina gani...ukishapata nafasi ya kufanya mafunzo ya awali ya Jwtz achana na yale ya jkt...haya ya jwtz ikitokea umeumia mafunzoni wanakuajiri hivo hivo..
 
Inaelezwa kuwa shariti mojawapo la mtu kuruhusiwa kujiunga na Jeshi la Wananchi ni kutokuwa na kovu mwilini na nasikia watu hulazimika kukaguliwa mwili mzima kuthibitisha kuwa hawana kovu/makovu katika mbili yao....
Kovu ni ulemavu
 
Inategemea na aina ya makovu mkuu..wanahofia katika mazoezi yao kovu linaweza likasababisha kidonda tena...

Sasa wewe unashangaa kovu...hata ukiwa unanyanyua vyuma (kupiga nondo) jeshini hauajiriwi..
Tunazidi kuyajua mengi.
 
Kovu NI ulemavu
Mazoezi makali ya jeshi yanawwza kusababisha maumivu upyaaa kwenye Hilo kovu
Mwili unapopata kovu kiasi Cha kovu Hilo kashindwa kufutika ina maana tatizo hapo lilikuwa kubwa na lilisogea mpaka ndani ya mwili
 
Kovu ni kwa maana ya Tatto, ile michoro ya mwilini, kovu la ndui linaruhusiwa...



Cc: mahondaw
 
Duuu mbona naonaga wamekata ina maana hawapigi nondo
Inategemea na aina ya makovu mkuu..wanahofia katika mazoezi yao kovu linaweza likasababisha kidonda tena...

Sasa wewe unashangaa kovu...hata ukiwa unanyanyua vyuma (kupiga nondo) jeshini hauajiriwi..
 
Sio kovu michoro mwilini kama tatuu manake ukifuta tatuu inakuwa kovu ,,io ni kwasababu ule mchoro mwilini wa tatuu ukipata joto mda mrefu unakuwa kidonda hasa fikilia jeshini watu miezi miwili au zaidi watu wanaweza wasivue lilegwanda kwaio kidonda kinapata bacteria inakuwa shida tena ..
 
Albinism, makovu makubwa, operation tumboni, tattoo, ulemavu wowote mfano kdole kmekatika, mguu mfupi/umepinda, jicho moja.... Yan ukiwa na kasoro kwenye mwili wako majeshi yote hayakuajiri wanakuita unfit nafkr ni kwaajil ya mazoez yanahitaj uwe fit majeraha ukiyapatia kazn unaendelea na kazi
 
Duuu mbona naonaga wamekata ina maana hawapigi nondo
Miili mikubwa tu kutoka na mazoezi ya ka viungo pamoja na afya njema yaani kama unene flani hivi..lakini sio uwe na mwili wa kupiga nondo..yaani juu umejazia chini upo upo kama ufunguo... Hapo huajiriwi..kwasababu miguu yako inakuwa haina nguvuu huwezi kusimama muda mrefu.
 
jeshi kovu wanaamini uliwai vunjika sasa kwenye mtiti wa mazoezi kule wanaweza kukuludishia ulemavu ndio mana kuepusha ilo wenye kovu hawachukuliwi na kama mguu hauna uvungu huchukuliwi yote ya yote chagua magufuli mitano tena
 
Sio makovu yote hayatakiwi, kuna aina ya makovu. Ni yale makovu makubwa sana, yenye moto, alama yoyote paji la uso,tatoo n.k
Kwa upande Wa makovu ni kwaajili ya mazoezi maana unaweza kupata matatzo hasa hvyo vidonda vitakavyotokana na kuchubuka kwa makovu hayo. Mengne ni siri ya kambi. Sio kila kitu ukijue

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom