Kwanini sharti mojawapo la kujiunga na Jeshi ni pamoja na kutokuwa na kovu mwilini?

Kwanini sharti mojawapo la kujiunga na Jeshi ni pamoja na kutokuwa na kovu mwilini?

Hayupo Mbali na ukweli mkuu, wakati tupo mujibu wa sheria tuliuliza hilo jambo. Majibu ni kwamba kovu haliponi so kwenye mambo mengi na mazoezi ya kijeshi kidonda kinaweza kurudia upya ukawa unfit kwa ajili ya jeshi

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Sorry mkuu nilitaka ku-quote comment ya juu yake liyesema kuhusu GPS ambayo si kweli
 
Kuwa na kovu kubwa Ni Kama ulemavu au kasoro inayopunguza ufanisi wa mwili wako kuhimili mazoezi na mafunzo ya kijeshi,

Pia tattoo hairuhusiwi kwa sababu:-

A. Ni ishara kuwa mhusika Hana nidhamu binafsi, moja ya mambo mhimu jeshini Ni nidhamu hivyo kuwa na alama ya tattoo Ni ishara ya kutokuwa na nidhamu.

B. Tattoo Ni alama yoyote ambayo inaweza kutumiwa na watu Fulani Kama utambulisho wa kundi lao hivyo kumuingiza mtu jeshini akiwa na tattoo Ni sawa na kukaribisha makundi au magenge ya wahuni nawahalifu jeshini.

C. Mtu mwenye tattoo hawezi/ Ni vigumu kutoa damu ( blood donation) kwa wengine, lakini jeshini inahitajika kila Askari kuwa tayari kusaidia wengine kwa kutoa damu haraka hasa kwenye uwanja wa Vita iwapo Kuna majeruhi wenye uhitaji.

Nb: watu wengi wa usalama wa taifa wana tattoo (just kidding)
 
Inategemea na aina ya makovu mkuu..wanahofia katika mazoezi yao kovu linaweza likasababisha kidonda tena...

Sasa wewe unashangaa kovu...hata ukiwa unanyanyua vyuma (kupiga nondo) jeshini hauajiriwi..
Hivi nikweli mtu ukiwa mnyanyua vyuma mikono inakua haiwezi kunyooka sawa sawa yn ktk mstari mnyoofu (inakua imetengeneza kama matege flan ivi)kwaiyo ukiambiwa mguu sawa unajikuta unajitahidi kubana miguu namikono lkn bado mikono inaacha madirisha.
 
Huwa wanapima mpaka njia ya haja kubwa,kama imetumika
 
Kovu - ishara ya mwili wako kuwa sio fit kwa mazoezi makali jeshini, na hawataki itokee ati kovu limefunguka tena ukiwa training, itakuwa lost of time kwako na pia kwao watatakiwa wakutibu hadi upone, wakati wenzako wenye mko group moja wanaendelea na mazoezi, wewe uko nyuma. Hilo instructors hawali mind. Tena ukumbuke, ukiwa jeshini na bahati mbaya upate jiraha litakalo kufanya kutoendelea na kazi yako, lazma uwe discharged na ulipwe na serikali, kwa mujibu wa sheria za kijeshi, sababu uliumia ukiwa cadet sio raia. Ndio maana hawataki uwe na kovu lolote kubwa alafu iwe mseo baadaye, iwe mambo ya kotini tena, wataka kulipwa ilhali ulikuwa na jeraha kabla hujaingia mazoezini.

Tatoo - upande huu wa michoro ya kwenye miili, huwa naona ni hapa Afrika tu ndio tuna huo utopolo bado. Uwe una tatoo, uwe huna, ukiingia jeshi tu, nidhamu utakuwa nayo, upende usipende. Neno 'ME' litakutoka kwenye mazungumzo yako, utakuwa unasema 'WE', kumaanisha nyote hapo kambini ni madungu kuanzia hiyo siku hadi utakapo iacha dunia, ubinafsi umeuacha uraiani. So hii issue ati mtu kuwa na tatoo hana nidhamu, huwa fikra zetu bado sizielewi. Nafkiri wengi wenyu mnajua nchi zilizoendelea sana, kando na Waarabu, hawaulizi story na tatoo, uwe nayo mwilini au la, hawajali, bora wewe ufaulu training na uwe sharp kwa kile unachofundishwa iwe practical ama theoretical. Mfano ;mwanajeshi wa Ufaransa, Amerika, ujerami, Swiss nk vijana wanaojiunga jeshi wamechafuka tatoo sana lakini hilo sio pingamizi, (na inategemea tatoo iko sehemu gani ya mwili na ni ya aina gani), uwe mrefu uwe mfupi, hilo hawajali, uwe mvaa miwani, dogo unaingia. Sasa angalia mafunzo yao na yetu huku, vita vyao na vyetu, elimu ya jeshini ya kwa na kwetu. Wana 'nidhamu' kutushinda 😂😂😂

Hitimisho - Sheria nyingi za utopolo jeshini, ata kwenye askari polisi, huwa tumezitunga wenyewe ili kupunguza raia wengi kuingia kazi hiyo, lakini ukweli ni nyingi huwa hazisaidii kuongeza wala kupunguza capabilities za mwanafunzi wa jeshini.
Bora uwe physically fit na akili ya u chap chap basi huwa uko sawa tu na usiwe mgonjwa😂
✌️
 
Kanuni kubwa jeshini ni Order kwa hiyo Disorder yeyote .Haikubaliki mwilini .Mfano.makonde na zile chale zake hawezi ajiriwa jeshini pia ukiwa na tatoo.huajiriwi.Wanataka mwili usiwe na disorder yeyote popote

Hiyo iko.majeshi yote.Mwili.unatakiwa uwe in order wote hakuna sijui kinundu au kitovu kikubwa no
 
Wacha kuhadaa watu kwa uongo wewe, hii order unayoiongelea hapa sio ya dunia nzima. Labda huku Afrika, nchi zetu ndio bado tunatumia hiyo issue kupunguza raia wanaokuja recruitment. Bajeti ya nchi haiwezi kuandika vijana nyie wote jeshini, nani atawalipa mishahara wakati bado nchi zenyewe ni developing countries. Ndio kukawekwa hivyo vikwazo, watu wapunguzwe hadi mwisho wa siku unaweza pata watu wawili au watano mkoa mmoja ndio wamechaguliwa na mlioenda kiwanjani ni mamia. Serikali ina ujanja
Nenda nchi za nje, sanasana bara uropa, Ulaya huko ujione wanajeshi
 
Kujiunga na Jeshi la marekani na Israel lazima mwili wote usiwe na mkwaruzo popote no disorder yeyote mwilini.Wanataka uingie ukiwa na mwili perfect asilimia mia moja

Sisi tume copy tu .

Dis order yeyote haikubaliki
 
Fafanua hizo disorder!
 
Fafanua hizo disorder!
Any .Mwili pefect si unaujua .Ngozi yote iwe vizuri kusiwe na chochote .Vidole vypte viwe sawa nk
mfano una likitovu kubwa hawakuchukua kila kitu kiwe normal.Ngozi normal.hata uume na uke normal .Jikague mwenyewe ukiona una kakitu kasiko ka kawaida popote mwiliniukivua nguo zote usihangaike kuomba kazi jeshini.
 
Fafanua hizo disorder!
hawatafuti disorder wanafuta mtu ambaye yuko order .Ni sawa ns ukiniuliza noti feki ikoje nikuambie Nitakuambia ni yeyote isiyolingana na noti halali.Chochote kisicholingana mwili ulio mzuri.kwenye order kwenye sehemu yeyote hiyo inaitwa disorder liwe kovu etc
 
Upande wa makovu hapo sawa, lazma uwe fit mkuu haipingiki hio. Lakini kuhusu tatoo nchi za nje nyingi hawatilii maanani ka sisi huku.
 
Back
Top Bottom