Kwanini sisi wapare hatujui football?

Kwanini sisi wapare hatujui football?

Mkuu yaani serikali itenge bajeti kufanya tafiti kwamba kwanini hakuna wachezaji wapare? 😂😂😂😂
Serikali inaweza kutengeneza sera za kujenga viwanja milimani ili watoke watu wenye vipaji hivyo.
 
Hahaha, na kweli sijawahi sikia mchome, mbaga, mndeme. Ila nadhani hata wachaga na wamasai ni wachache, mara chache sana kusikia Lymo, mushi, saitoti, Mollel... Nadhani kaskazini na mpira kidogo ni changamoto.
Wacheze mpira ujambazi na pombe wamuachie nani.
 
Kipaji pia kinatembea kwenye familia, ukoo na jamii kwa kurithi. Uenda mababu wa mwanzoni katika ilo kabila hawakua na kipaji wala phisical favourite yoyote ya kusakata soka.
 
Moto anatakiwa apate muda wa kutosha kuwa huru acheze sana mpira ili awe fundi

Wazazi wengi upareni mtoto ni kazi kazi full under control. Usipofanya kazi za familia unaweza usile

Pwani watoto hawapewi sana kazi na wazazi wao. Mtoto anatafutwa ili ale.
Hivyo anakuwa na muda wa kutosha kujifunza mpira na mengineyo.

Ndio maana vijana wa kiume wa pwani wanna vipaji sana vya nje ya masomo. Na wanafanikiwa sana

Hata mabinti wa pwani ni mafundi KWA vile ukiachana na mafunzo ya unyago,hawabanwi sana katika ukuaji wao
Jibu tosha kabisa , wachezaji wote ni walipata mda utotoni wa kucheza.
Hata hapa mjini bado mtoto wa mpare na mchaga hana mda wa kucheza ni full kulisha kuku na nguruwe
 
Hahaha, na kweli sijawahi sikia mchome, mbaga, mndeme. Ila nadhani hata wachaga na wamasai ni wachache, mara chache sana kusikia Lymo, mushi, saitoti, Mollel... Nadhani kaskazini na mpira kidogo ni changamoto.
Kumbuka Leodgar Tenga anatoka Kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom